Dereva wa Bolt, Uber au Tax ni siri gani alishawahi kukwambia abiria hutakuja kusahau

torosi

JF-Expert Member
Aug 12, 2020
788
1,308
Great thinker

Kama kichwa kinavyosema, ni siri/stori gani hutasahau uliyokutana nayo ukiwa kazini.?

Hiki kisa kilimtokea mdogo wangu alikuja nihadithia kama mwezi baada ya kutokea

Miaka kama miwili nyuma, alimbeba dada mmoja kutoka club, alikua kalewa ila kwa nje alionekana mtaratibu sana, alivyoingia tu akaomba samahani kuwa kaingia kwenye ndani ya gari kalewa

Anasema hakuoneka kama mtu wa club, wakati wako njian akamuuliza usiku wake ulivyokua, alichomjibu ndio kilichomtoa machozi.

Yule dada alimwambja kuwa ile ndio ilikua siku yake ya kwanza kwenda club, na ni rafiki zake ndio waliompeleka sababu alikua ameacha kazi siku iyo, kwa hiyo wakaamua kumfanyia goodbye party na kumtoa. Sabab ya yeye kuondoka aliwaambia kuwa anaenda abroad kuongeza masomo, lakini ukweli ni kuwa aligundua kuwa ana brain cancer na tayari ilishavuka kiwango kiasi hata chemo isingemsaidia na hakutaka kuwaambia wafanyakazi wenzie.

Dogo anasema siku hiyo machozi yalimtoka pamoja na kuwa hakuwa anamjua mpaka alipomfikisha

Duniani watu wanapitia mengi
 
Jitahidi kutunza siri za watu wewe kijana na hiyo kazi yako ya uber au bolt.

katika kazi za tax huwa kuna siri nyingi hivyo yakupasa uwe na kifua usipende kuweka weka mambo ya watu hadharani nakumbuka miaka ya nyuma madereva tax walikuwa wakiuwawa hasa kwa kuvujisha taarifa za watu.
 
Atayetoa siri za mteja wake hapa ni very unprofessional.

Kesho ukija na uzi wa madaktari na manesi kutoa siri za wagonjwa wao unishtue.
 
Kuna mmoja alinipa siri kwamba kuna Tajiri anataka kuinunua Tanzania halafu sisi wanatuhamishia Marekani..

Hii siri usimwambie mtu mwingine Mkuu.
 
Sisi madereva bodaboda hatutoagi kabisa siri za wateja wetu.
Na tunawajua IN/OUT wateja wetu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom