Dereba Abood asomea mashtaka 51 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dereba Abood asomea mashtaka 51

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Jan 7, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Dereba Abood asomea mashtaka 51


  Na John Gagarini, Kibaha

  DEREVA Maulid Mohamed (36) wa basi la Kampuni ya Abood ambalo lililosababisha ajali Januari 5, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu wawili na majeruhi 49 amefikishwa mahakama ya wilaya ya Kibaha akishtakiwa kwa
  makosa 51 ilikiwa ni pamoja na kuendesha gari kwa uzembe.

  Dereva huyo mkazi wa mkoani Morogoro alisomewa mashtaka hayo kwa hakimu mkazi wa wilaya, Bi. Bahati Ndesarua, mbele ya mwendesha mashtaka, Bw Silas Jonas.

  Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa katika eneo la TAMCO Mjini Kibaha, dereva huyo aliendesha gari kwa uzembe na kusababisha ajali iliyosababisha vifo vya mwendesha pikipiki na abiria wake.

  Ilielezwa kuwa mwendesha pikipiki ambaye kwa sasa ni marehemu ni Bw. Hamis Dadi na abiria wake, Bi. Lucy Mageuza ambaye alikuwa mfanyakazi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Idara ya Ardhi.Dereva huyo alikana mashtaka hayo na kesi yake imepangwa kutajwa tena Januari 24, mwaka huu.

  Ajali hiyo ilitokea Januari 5 mwaka huu baada ya basi la Abood lenye namba za usajili T 588 AYM lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Morogoro liliigonga pikipiki yenye namba za usajili T 616 BLF iliyokuwa ikikatisha kwenda Halmashauri ya Mji wa Kibaha baada ya harakati ya kutaka kuikwepa pikipiki hiyo kushindwa.

  [​IMG]
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  hivi unapomshitaki mtuhumiwa mashtika mengi hivyo huoni haki zake za kujitetea umesigina.........................attanzia wapi kujitetea kwenye mashitaka hayo yote?
   
 3. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  hivi chenge alishitakiwa makosa mangapi?maana naona huyu amepewa makosa mengi sana
   
 4. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Amtafute wakili wa Chenge.....mkuu hebu edit hiyo heading ya post
   
Loading...