Deo Filikunjombe: Mbunge anayefanya makubwa jimboni mwake

Msukule kazini! Una criticise bila kufanya critical analysis kupitia post ya candid scope.

Watanzania thamani yetu ni ndogo sana. Kagari ka wagonjwa. Iwe ni mbunge wa CCM au chama kingine chochote, si kazi yake kununuwa gari la wagonjwa na kutangaza, ili iweje?

Rushwa ni za aina nyingi sana, hii ni mojawapo.

Nilitegemea wabunge wasimamie mambo mazito ya kubadilisha maisha ya watu.
 
Jamaa kichwani yuko sawasawa na binafsi sikuelewa kwa nini alikuwa polisi!
 
Yeye aliamini angepewa uwaziri au unaibu uwaziri kama angekuwa mbunge!
 
Kwa nini wanaume wa maeneo anayaotoka Deo huwa hawatahiriwi? Pale kasita ilikuwa huwezi kuoga na jamaa bathroom moja na akifanya hivyo basi lazima aoge na chupi!

Are you He or She?
 
amefanya kitu kizuri lakini that ambulance is not a 90 million worth. Hapo umetupeleka mramba.
 
Jamani ametumia sehemu ya 90mil au yote 90mil kununua Hiace,maana najua piga ua galagaza iyo Hiace haifiki 40mil pamoja na vikolokolo vya uambualance.
Kazi unayo baba Liganga na Mchuchuma hakikisha yao madini yanawafaidisha watu wako wako pia!
 
Kwanza kabisa lazma ujue kuwa rushwa ni adui wa haki na haijawahi kuwa nzuri kwa jamii yoyote ile isipokuwa mtoaji na mpokeaji rushwa.

Pili naona kunadhana potofu ambayo imejengenga kuwa mbunge ni mfadhili. Hii si sawa kabisa. Mbunge makini ni yule anayefundisha watu wake namna ya kujikwamua kiuchumi na kuhamasisha maendeleo ya jamii yake etc. Tanzania haitaki mbunge anayewapa watu samaki e.g kugawa mahindi, bali anayewafundisha watu kuvua e.g kufundisha kanuni za kilimo bora/kuwapa elimu ya biashara ili wawe na maendeleo endelevu na sio maendeleo yanayomtegemea fulani, hivyo huyo fulani asipokuwepo basi hakuna maendeleo.

So afanyacho Filikunjombe so far anajitahid ila aende beyond ili maendeleo ya wana Ludewa yawe endelevu na sio yategemee uwepo wa Filikunjombe ie. kugawiwa magari, kutoa sadaka kubwa, kulisha makutano wengi, etc

Very well said. Sawa gari katoa msaada, gharama za uendeshaji je? Maana linahitaji mafuta, vipuri na kadhalika. Hizo pesa zinatoka wapi? Tanzania inahitaji kuwa na MWONGOZO. Yaani hata Mbunge akiachia ngazi yule anayekuja anafuata tu yale yaliyomo kwenye mwongozo huo. Mwongozo huo unatakiwa kutoa picha halisi ya nini kinatakiwa kufanyika ndani ya miaka mitano, kumi, kumi na tano hadi hamsini.

Siyo kila mtu akiibuka tu anakuja na mbwembwe zake zisizokuwa na tija. Inasikitisha sana tunapoona wabunge wamekwenda majimboni kwao halafu anatoa vifaa vya kufundishia shule kama msaada. Kazi yake ni nini? Na kwanini uwe ni msaada? Na kama ni msaada kwanini uite waandishi wa habari wakupige picha na utoke kwenye TV na magazeti?

Inawezekana kabisa Watanzania tukawa hatujui tatizo letu ni nini. Tatizo letu si rasilimari, hiyo inajulikana. Tatizo letu kubwa ni ''mind-set''. Yaani tumeshindwa kabisa kujitambua sisi ni nani, tuna nafasi gani katika kuleta mabadiliko katika jamii zetu na tunakwenda wapi. Matokeo yake mtu kama mimi leo hii nikienda kijijini kwetu likizo baada ya kutokwenda kwa miaka 10, nikafika pale nikachinja ng'ombe wawili wanakijiji wale kwa kuwa tu hatujaonana muda mrefu na ndugu zangu; basi tayari watanishauri nigombee ubunge....Na hata wapambe wa mbunge wa jimbo hilo watampigia simu kumwambia kwamba kuna mtu anataka kuchukua ''jimbo lako''. Seriously, we have gone that LOW!!

Tutafakari!
 
Kwa mtazamo wangu PCCB wanatakiwa kufanya uchunguzi kwa Mbunge huyu maana hii ni Rushwa kutokana na kuwa posho wanayopewa wabunge ni kwa ajili ya kujikimu wakiwa bungeni sasa kama inatokea Mbunge anatumia fedha hizo kununua ambulance, je, alikuwa anaishi vipi pale Dodoma? je, ndo kazi ya posho anayopewa? na nafikiri hata CAG anatakiwa kuliangalia hili maana ni mic use of fund! lengo la kutolewa kwa posho hiyo c kununua ambulance! niwashauri wabunge wasaidie wananchi waweze kujikwamua katika maisha maguni kwa kuwajengea uwezo wa kufikiri mambo ya kufanya ya maendeleo kuliko kuwaonga kama alivyofanya Deo!

Kama Hosea anafumbia macho vitendo kama hivi ni dhahiri PCCB hawana ufahamu wa kutosha kuhusu tafisiri ya Rushwa!
 
Hiyo kama ni rushwa imekaa vizuri ukizingatia hakuna uchaguzi mdogo kule,gari lile litasaidia maskini wasioweza kukodi hata hat bajaji, rushwa ni zile za kugawa unga,maji yenye viluilui na minyoo kibao wakati kampeni,uchaguzi ukiisha wananchi wanabaki wanaharisha na kuteseka kwa typhoid, mbunge akiwa nakula bata mjengoni.Siwapendi magamba lakini kitendo cha Filikunjombe kinaashiria kuwajali wapiga kura,ndo maana jamaa wakati wa kampeni alipiga magoti kwa wapiga kura na si kugawa sukari.
Kijana inabidi ahamie....

ff, hilo hujaliona zito? jana kuna mmama kajifungulia kwenye taxi. huko kijijini ndo wanajifungulia njiani kabisa! walau ameonesha nia,kuna mbunge hata kupita jimboni kwake hapiti hadi uchaguzi ufike! nilishuhudia mbunge wa ccm in 2005 akigombea tena mufindi akapopolewa mawe mbele ya jk!
 
Jamani ametumia sehemu ya 90mil au yote 90mil kununua Hiace,maana najua piga ua galagaza iyo Hiace haifiki 40mil pamoja na vikolokolo vya uambualance.
Kazi unayo baba Liganga na Mchuchuma hakikisha yao madini yanawafaidisha watu wako wako pia!

Watanzania kwa ku-inflate vitu uutawaweza? Ushabiki umepitliza utesema kaleta Landrover brand new kumbe ni ka-used ka Dubai.
 
Jamaa kichwani yuko sawasawa na binafsi sikuelewa kwa nini alikuwa polisi!
Wewe kweli ndyoko,kwa akili yako unadhani polisi ndio sehemu ya watu ambao hawana akili..no research no right to speak...another crap
 
Kweli you guys you are great thinkers. Kuna milioni 90 kwenye hiyo Hiace chakavu hapo kweli??

NB: Hebu wadau mliopo huko ludewa rusheni registration number ya huo mkangafu tuwape actual cost zake mara moja.

Kagari kenyewe ni ka milioni 10 - 12, halafu mnadai katumia milioni 90 za mkopo wake! Huu ni upotoshaji. Haya na huyo Lema kafanya nini?

amefanya kitu kizuri lakini that ambulance is not a 90 million worth. Hapo umetupeleka mramba.

Jamani ametumia sehemu ya 90mil au yote 90mil kununua Hiace,maana najua piga ua galagaza iyo Hiace haifiki 40mil pamoja na vikolokolo vya uambualance.
Kazi unayo baba Liganga na Mchuchuma hakikisha yao madini yanawafaidisha watu wako wako pia!

Duh..Kaazi kwelikweli.

Ebu someni maelezo hayo vizuri, hajasema amenunua Ambulance moja kwa Tsh. Million 90 BALI AMETUMIA FEDHA ALIZOZIPATA KWENYE MKOPO WA MILLION 90 kununulia Ambulance, kwa hesabu alizonifundisha Mwalimu Mnyawasa, jumla ya pesa zilizotumika kununulia hiyo Ambulance ni Less or Equal to TSH MILLION 90, ni Tsh. ngapi hasa hajasema....

Je Deo atanufaika kwa kutoweka bei halisi ya hizo Ambulance SIJUI, je wananchi maskini wa Manda, Rupingu na Mlangali wanahitaji kuijua bei ya hizo Ambulance HAPANA, simple...
 
Very well said. Sawa gari katoa msaada, gharama za uendeshaji je? Maana linahitaji mafuta, vipuri na kadhalika. Hizo pesa zinatoka wapi? Tanzania inahitaji kuwa na MWONGOZO. Yaani hata Mbunge akiachia ngazi yule anayekuja anafuata tu yale yaliyomo kwenye mwongozo huo. Mwongozo huo unatakiwa kutoa picha halisi ya nini kinatakiwa kufanyika ndani ya miaka mitano, kumi, kumi na tano hadi hamsini.

Siyo kila mtu akiibuka tu anakuja na mbwembwe zake zisizokuwa na tija. Inasikitisha sana tunapoona wabunge wamekwenda majimboni kwao halafu anatoa vifaa vya kufundishia shule kama msaada. Kazi yake ni nini? Na kwanini uwe ni msaada? Na kama ni msaada kwanini uite waandishi wa habari wakupige picha na utoke kwenye TV na magazeti?

Inawezekana kabisa Watanzania tukawa hatujui tatizo letu ni nini. Tatizo letu si rasilimari, hiyo inajulikana. Tatizo letu kubwa ni ''mind-set''. Yaani tumeshindwa kabisa kujitambua sisi ni nani, tuna nafasi gani katika kuleta mabadiliko katika jamii zetu na tunakwenda wapi. Matokeo yake mtu kama mimi leo hii nikienda kijijini kwetu likizo baada ya kutokwenda kwa miaka 10, nikafika pale nikachinja ng'ombe wawili wanakijiji wale kwa kuwa tu hatujaonana muda mrefu na ndugu zangu; basi tayari watanishauri nigombee ubunge....Na hata wapambe wa mbunge wa jimbo hilo watampigia simu kumwambia kwamba kuna mtu anataka kuchukua ''jimbo lako''. Seriously, we have gone that LOW!!

Tutafakari!

Gharama za uendeshaji zinapaswa zitoke kwenye pesa za halmashauri, Mbunge na madiwani wenzake wanapaswa kuhakikisha kuwa fungu hili linapatikana kwenye bajeti yao ya huduma za afya.

Hayo mengine, tupo pamoja sana...
 
Amefanya vzuri kutoa msaada huo,lkn wabunge washughulikie zaidi na mfumo mzima wa usimamizi wa rasimali zetu uwasaidie wananchi kwa ujumla kuzifaidi na si kuishia kutoa vijimisaada ambavyo ni kama kuwapumbaza tu, wawafundishe namna ya kuvua samaki na si kuishia kuwapa vipande vya samaki. Ndio mambo aliyokuwa anayafanya rostam jimboni kwake kuwasaidia watu kwa hela binafsi akiondoka kila kitu kinarudi zero ground.
 
nakubali kwa hilo, lakini sikubaliani na gari kuandikwa "denoted by Deo Filikunjombe" huu ni udhaifu mkubwa kwa mtu kuwa kiongozi wa watu. nahisi anapenda sifa sana ingawa simjui. ludewa ninayoijua hizo ambulance zitapeleka wagonjwa katika hospitali gani? au ile ya Ludewa mjini ambayo huduma ovyo. lakini ameshawaloga wadanganyika. ee mola lini utaiokoa Tanzania?
 
Mie nilikuwepo kwenye ule mkutano. Filikunjombe kasema amestumia sehemu ya tshs 90 alizopewa na bunge kwaajili ili kuwannulia gari wananchi wa mlangali. Ikumbukwe kuwa Rais Jakaya Kikwete aliahidi kuwapelekea wananchi wa Mlangali toka mwaka 2008 na hajafanya hivyo mpaka leo. Filiknjombe, kwenye mkutano huo, kasema "tumieni hii gari mpaka hapo JK atakapotekeleza ahadi yake" baada ya hapo mtakuwa huru kuamua nyie mlipeleke wapi. Mie nadhani hili ni jambo jema. Ndege mmoja mkononi ana thamani kuliko tisa walioko mwituni.
 
Which is better btn the two bajaji za wagonjwa au hii gari alotoa Filikunjombe? Hivi kuna watanzania wangapi leo wananunua brand new cars kwa ajili ya matumizi yao binafsi? Asilimia 90 ya wabongo tunatumia used. Kutoa ni moyo, I think.
 
Watanzania thamani yetu ni ndogo sana. Kagari ka wagonjwa. Iwe ni mbunge wa CCM au chama kingine chochote, si kazi yake kununuwa gari la wagonjwa na kutangaza, ili iweje?

Rushwa ni za aina nyingi sana, hii ni mojawapo.

Nilitegemea wabunge wasimamie mambo mazito ya kubadilisha maisha ya watu.

Serikali inawajibika kufanya huduma hizo kwa wananchi wake, na sasa miaka 50 ya uhuru vituo vya afya havina magari ya wagonjwa, na hata kuwa na mpango wa kata kuwa na gari ya huduma za umma hakuna. Anayeelemewa na malalamiko ni mbunge, na mwenye nafasi ya kuwasikiliza wananchi ni mbunge. Sasa tusishangae wabunge kufanya kazi za kimisionari kutokana na uchungu walionao kwa waliowachagua. Huu umisionari si vizuri kuutafsiri kwamba ni rushwa, vinginevyo yafanyike hayo wakati wa uchaguzi, lakini kwa sasa ubunge alio nao ni hamasa tosha kuwahudumia wachaguliwa wake.
 
Sina ugomvi na yeye kukabidhi gari ila ugomvi wangu ni pale viongozi wetu wanapotumia misaada ikakwa ajili ya faida za kisiasa?...kama gari ni kwa ajili ya matumizi ya hospitali ya wilaya kwann asingemkabidhi mkuu wa wilaya au daktari wa wilaya??

.....kazi ya mbunge sidhani kama ndo hii, anatakiwa kuzunguka huko na huko kumobilize wadau wa kiuchumi na kusimamia vema matumizi ya hela za halmashauri, ila kwa staili hii ya kutumia hela zao kutoa misaaada sidhani kama tutafika

Your are wrong. Msaada wa gari kwa wagonjwa umetolewa na mbunge binafsi na wala si serikali imetoa. Serikali ingetoa hapo viongozi wa serikali wangehusika, kwa hili uko nje ya uringo tayari. Na hilo gari alilotoa si la kwanza ameshatoa misaada kadhaa na hili huenda ni gari la pili au la tatu. Na ameamua kumwajiri mhudumu wa afya katika kituo cha mwmbao wa ziwa Nyasaa kwa gharama zake sababu serikali haichukulii uzito. Acha afanye umisionari, maana serikali imelala usingizi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom