Deo Filikunjombe: Mbunge anayefanya makubwa jimboni mwake

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,877
6,830
Tanzania tunahulka ya kuchagua chama na rangi yake bila kuangalia uwezo wa mtu. Mbunge kijana Deo Filikunjombe Haule wa Ludewa anafanya makubwa jimboni mwake na hivyo kuwafunika wabunge wote waliomtangulia na wamekiri hivyo. Hayo ndiyo maendeleo tunayotaka kama alivyofanya Godbless Lema wa Arusha. Kama posho wanazolilia wabunge zingekuwa zinafanya kazi kama hiyo ingeeleweka.


DSCF7201.JPG
DSCF7109.JPG
  • Picha ya 1: Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akikabidhi gari ya wagonjwa kata ya Mlangali kwa mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ludewa gari lalilonunua kwa posho yake milioni 90
  • Picha ya 2: Wabunge wa zamani waliomtangulia Filikunjombe Bibi Baraka, Simalenga, Mathias Kihaule na Kolimba.


DSCF7122.JPG
DSCF7167.JPG

  • Picha ya tatu: Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (kushoto) akisakata dansi na paroko wa parokia ya Kifumbe Mwamengele Ngole
  • Picha ya nne: Mbunge mstaafu Matias Kihaule ambaye alishawahi kuwa naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
DSCF7044.JPG
DSCF7018.JPG

  • Picha ya 5: Paroko Mwamengele Ngole akimkaribisha mbunge Filikunjombe na babake mzazi kusalimia
  • Picha ya 6: Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (kushoto) akishiriki ibada

DSCF7025.JPG
DSCF7073.JPG

  • Picha ya 7: Waumini wa kanisa la RC Ludewa wakimpongeza mbunge wao Filikunjombe kwa mchango wake wa maendeleo jimbo la Ludewa leo
  • Picha ya 8: Wadau wa wilaya ya Ludewa Bw.Nkwera na wenzake wakiwa nje ya kanisa la RC leo

Akiwahutubia wananchi hao Filikunjombe alisema kuwa mkakati wake katika jimbo hilo ni kuhakikisha anaendelea kupigania maendeleo ya jimbo hilo na katika kuanza amepania kuanza na ujenzi wa lami katika wilaya hiyo ya Ludewa lami ambayo itaanza Ludewa mjini kwenda wilaya ya Njombe.

Hata hivyo Mbunge huyo amesema kuwa ,katika kulipa fidia kwa wananchi wake amelazimika kuzitumia kiasi cha shilingi milioni 90 alizopata bungeni kununua gari ya wagonjwa katika jimbo hilo.

Alisema kuwa hadi sasa amepata kukabidhi gari la wagonnjwa katika kata ya manda ,Rupingu na sasa katikata ya Mlangali ambako pia rais Jakaya Kikwete amepata kuahidi gari katika kata hiyo ya Mlangali .

Filikujombe alisema kuwa Rais Kikwete alipata kuahidi gari katika kata hiyo na kuwa iwapo itafika gari hilo la Rais basi wao wataangalia matumizi ya gari hii ya sasa.
 

WA-UKENYENGE

JF-Expert Member
Oct 1, 2011
2,921
1,226
Hivi ni vitu ambavyo vilitakiwa vimeshakamilika tangu miaka 10 - 20 iliyopita, lakini wazee wetu wanatamaa za ajabu. Utadhani wao ndo viumbe pekee ndani ya tanzania. Ndiyo maana nasema, acha hiyo 2015 CCM wakae pembeni ila waendeleee kuwepo ili washuhudie mabadiriko yatakayoletwa.

Tunahitaji nchi yenye wachapa kazi siyo porojo za kuoneana aibu kuambiana ukweli. Wazee wetu wapumzike, waachie vijana! sawa kuna kazi tunahitaji misimamo yao lakini hii kasi ya sasa wazungu wataendelea kutufanya shamba la bibi. Mark my words.
 

Entare3

Member
Aug 4, 2011
29
7
Deo ukimtazama kwa jicho la tatu utagundua sio kiongozi mwenye fitina na itikadi za wana magamba...ana mtazamo na maono tofauti na wana magamba wengi..
Lkn kuna wakati huwa anapitiwa na kuwadhihaki wabunge wenzake wa CDM....akijirekebisha ktk hili atakuwa na nafasi kubwa mbeleni...ktk serikali hata ya mseto tunayoitarajia baada ya 2015
 

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,877
6,830
Deo ukimtazama kwa jicho la tatu utagundua sio kiongozi mwenye fitina na itikadi za wana magamba...ana mtazamo na maono tofauti na wana magamba wengi..
Lkn kuna wakati huwa anapitiwa na kuwadhihaki wabunge wenzake wa CDM....akijirekebisha ktk hili atakuwa na nafasi kubwa mbeleni...ktk serikali hata ya mseto tunayoitarajia baada ya 2015

Nakubaliana na hoja yako, kwani sijaona mmbunge anayewafuata wabunge waliomtangulia kuwataka shauri. Lakini Filikunjombe amewatafuta wote kuanzia mbunge wa kwanza jimboni mwake na sasa wako bega kwa bega kuleta maendeleo jimboni mwake. Kuna kitu cha kujifunza kwa kijana huyu.


Mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni
 

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,877
6,830
Pamoja na jitihada anazofanya, kuna kitu ambacho wengi wanamagamba hawafanyi. Deo Filikunjombe haionei aibu serikali kuikosoa pamoja na viongozi wake wanapoonekana kumkera na kuharibu jitihada zake. Huo ndio mfumo wa uongozi uliotukuka badala ya kufunika funika tu na wanaoumia na wananchi waliowachagua.
 

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
73,743
74,358
Watanzania thamani yetu ni ndogo sana. Kagari ka wagonjwa. Iwe ni mbunge wa CCM au chama kingine chochote, si kazi yake kununuwa gari la wagonjwa na kutangaza, ili iweje?

Rushwa ni za aina nyingi sana, hii ni mojawapo.

Nilitegemea wabunge wasimamie mambo mazito ya kubadilisha maisha ya watu.
 

King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,802
24,505
ff, hilo hujaliona zito? jana kuna mmama kajifungulia kwenye taxi. huko kijijini ndo wanajifungulia njiani kabisa! walau ameonesha nia,kuna mbunge hata kupita jimboni kwake hapiti hadi uchaguzi ufike! nilishuhudia mbunge wa ccm in 2005 akigombea tena mufindi akapopolewa mawe mbele ya jk!
 

Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,467
1,164
ff, hilo hujaliona zito? jana kuna mmama kajifungulia kwenye taxi. huko kijijini ndo wanajifungulia njiani kabisa! walau ameonesha nia,kuna mbunge hata kupita jimboni kwake hapiti hadi uchaguzi ufike! nilishuhudia mbunge wa ccm in 2005 akigombea tena mufindi akapopolewa mawe mbele ya jk!

Mkuu unakufahamu Ludewa? Unafahamu barbara za huko? Mvua ikinyesha kule hutoki bila 4 X 4
 

majata

JF-Expert Member
Oct 7, 2010
430
179
Watanzania thamani yetu ni ndogo sana. Kagari ka wagonjwa. Iwe ni mbunge wa CCM au chama kingine chochote, si kazi yake kununuwa gari la wagonjwa na kutangaza, ili iweje?

Rushwa ni za aina nyingi sana, hii ni mojawapo.

Nilitegemea wabunge wasimamie mambo mazito ya kubadilisha maisha ya watu.

Hizo ni rushwa tu, kazi yake nikuhakikisha anaibana serikali ihakishe inatumia kodi
Za wananchi vizuri na sio yeye kuwahonga wananchi kwa pesa zake, hizo mil90 atakuwanazo mara ngapi?,

"MTANZANIA KAAZI NI KWAKO."
 

Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
12,855
10,360
Nami nampongeza sana Ludewa jamani njia ni hatari sana wakati mvua na wagonjwa watapata shida kubwa sana!!kama hao viti maalum wangekuwa na uzalendo nao wange changia kusaidia maendeleo ila wanaishia kununua nguo kibao
 

Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,536
5,642
1. Majukumu ya mbunge ni yapi?
2. Kuna umuhimu gani wa kujitangaza anapotoa msaada?. Hilo gari ni msaada, wala sio sehemu ya majukumu yake.
Hii nayo ni Rushwa!
 

Patriote

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
1,718
1,046
Kama rushwa ndio hivi, basi sioni tatizo lake, maana kila jimbo lingekuwa na ambulance, au visima vya maji.
Milioni tisini ni madawati mangapi? Solar panels ngapi ?
Kwanza kabisa lazma ujue kuwa rushwa ni adui wa haki na haijawahi kuwa nzuri kwa jamii yoyote ile isipokuwa mtoaji na mpokeaji rushwa.

Pili naona kunadhana potofu ambayo imejengenga kuwa mbunge ni mfadhili. Hii si sawa kabisa. Mbunge makini ni yule anayefundisha watu wake namna ya kujikwamua kiuchumi na kuhamasisha maendeleo ya jamii yake etc. Tanzania haitaki mbunge anayewapa watu samaki e.g kugawa mahindi, bali anayewafundisha watu kuvua e.g kufundisha kanuni za kilimo bora/kuwapa elimu ya biashara ili wawe na maendeleo endelevu na sio maendeleo yanayomtegemea fulani, hivyo huyo fulani asipokuwepo basi hakuna maendeleo.

So afanyacho Filikunjombe so far anajitahid ila aende beyond ili maendeleo ya wana Ludewa yawe endelevu na sio yategemee uwepo wa Filikunjombe ie. kugawiwa magari, kutoa sadaka kubwa, kulisha makutano wengi, etc
 

Massenberg

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
1,173
1,370
Watanzania thamani yetu ni ndogo sana. Kagari ka wagonjwa. Iwe ni mbunge wa CCM au chama kingine chochote, si kazi yake kununuwa gari la wagonjwa na kutangaza, ili iweje?

Rushwa ni za aina nyingi sana, hii ni mojawapo.

Nilitegemea wabunge wasimamie mambo mazito ya kubadilisha maisha ya watu.

FF umenena. Nauliza swali hilohilo kwamba je, gari la wagonjwa inakuwaje jukumu la mbunge kununua au Rais kuahidi? Hii michezo imeshazoeleka kiasi kwamba watu wanaona mtatuzi wa shida zao ni mbunge wao na matokeo wapo wabunge ambao hii imewakuza vichwa mpaka wanaona majimbo ni mali zao binafsi.
Huku ni kukosa elimu ya uraia. Gari la wagonjwa ni jukumu wa serikali ya eneo hilo kama vile magari ya kuzoa taka yalivyo. Ikiwa wabunge wataendelea na hizi rushwa serikali za halmashauri zitaendelea kula fedha na kulala usingizi.
 

ndetichia

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
27,770
6,521
hii inakuwa sawa na ile ya mb kufanya wajibu wake halafu yeye anasema katoa msaada..
hii kitu ni muhimu sana kuifikria..
 

Patriote

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
1,718
1,046
Wakuu just for brainstorming, hivi kazi za mbunge ni zipi???????????
Yah hili ni swali zuri sana kujiuliza maana wengi wetu tunadhana potofu kuwa mbunge ni mfadhili wa jimbo na hivyo anapogawa Ambulance basi huyo ndo hasa Mbunge. Nionavyo mimi mbunge makini ni muhamasishaji washughuli za maendeleo na kiongozi wa mapambano dhidi ya ujinga, maradhi na umaskini. Na sio mbunge anayejipambanua kama mfadhili.

Mbunge ni coordinator wa shughuli za kimaendeleo jimboni kwake, na pia mbunge ni muwakilishi wa kero na hoja mbalimbali za wananchi kwa Serikali na mfwatiliaji wa karibu wa kero hizo ili zitatuliwe na serikali kutokana na Kodi zinazochangwa na wananchi kwa serikali yao.
 

hashycool

JF-Expert Member
Oct 2, 2010
6,568
2,803
yasiwe kama yale aliyotufanyia hainess ya ku show off na ku put off,mpaka leo lile gari halijulikani lilipo....na ule mjina wake mkuuuuubwa ubavuni mwa gari
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

3 Reactions
Reply
Top Bottom