SEAL Team 6
JF-Expert Member
- Jun 10, 2011
- 655
- 118
Mbona wabunge wengi tu wa CDM wamefanya hivyo lakini hawajajitangaza. Amefuata nyayo za CMD lakini hata hivyo bado anahali ngumu jimboni kwake.
Kama rushwa ndio hivi, basi sioni tatizo lake, maana kila jimbo lingekuwa na ambulance, au visima vya maji.
Milioni tisini ni madawati mangapi? Solar panels ngapi?
Pamoja na majukumu yoote ya Kibunge anayopaswa kuyafanya, tukumbuke pia kuwa alipewa Tsh. Million 90 za walipa kodi kwa ajili ya matumizi yake binafsi, kama Regia Mtema alivyowahi kukiri kuwa hiyo ni pesa ndoogo sana isiyotosha ata kwa matumizi ya wiki mbili.Sina ugomvi na yeye kukabidhi gari ila ugomvi wangu ni pale viongozi wetu wanapotumia misaada ikakwa ajili ya faida za kisiasa?...kama gari ni kwa ajili ya matumizi ya hospitali ya wilaya kwann asingemkabidhi mkuu wa wilaya au daktari wa wilaya??
.....kazi ya mbunge sidhani kama ndo hii, anatakiwa kuzunguka huko na huko kumobilize wadau wa kiuchumi na kusimamia vema matumizi ya hela za halmashauri, ila kwa staili hii ya kutumia hela zao kutoa misaaada sidhani kama tutafika
Tanzania tunahulka ya kuchagua chama na rangi yake bila kuangalia uwezo wa mtu. Mbunge kijana Deo Filikunjombe Haule wa Ludewa anafanya makubwa jimboni mwake na hivyo kuwafunika wabunge wote waliomtangulia na wamekiri hivyo. Hayo ndiyo maendeleo tunayotaka kama alivyofanya Godbless Lema wa Arusha. Kama posho wanazolilia wabunge zingekuwa zinafanya kazi kama hiyo ingeeleweka.
Hata hivyo Mbunge huyo amesema kuwa ,katika kulipa fidia kwa wananchi wake amelazimika kuzitumia kiasi cha shilingi milioni 90 alizopata bungeni kununua gari ya wagonjwa katika jimbo hilo.
Alisema kuwa hadi sasa amepata kukabidhi gari la wagonnjwa katika kata ya manda ,Rupingu na sasa katikata ya Mlangali ambako pia rais Jakaya Kikwete amepata kuahidi gari katika kata hiyo ya Mlangali .
Filikujombe alisema kuwa Rais Kikwete alipata kuahidi gari katika kata hiyo na kuwa iwapo itafika gari hilo la Rais basi wao wataangalia matumizi ya gari hii ya sasa.
Mbunge ananufaika na wanajimbo wananufaika. hii ikifanywa majimbo yote tanzania itakuwa ahueni.Kuhusu kilimo na afya bora,nadhani wengi wanajua ila tatizo ni fedha.Hata wilaya yao ikiwa na madini, wachina ndio wanafaidi, amelalamikia makaa ya mawe angalau.... hao wengine wanakariri vifungu vya vkanuni za bunge na kulamba posho.Kwanza kabisa lazma ujue kuwa rushwa ni adui wa haki na haijawahi kuwa nzuri kwa jamii yoyote ile isipokuwa mtoaji na mpokeaji rushwa. Pili naona kunadhana potofu ambayo imejengenga kuwa mbunge ni mfadhili. Hii si sawa kabisa. Mbunge makini ni yule anayefundisha watu wake namna ya kujikwamua kiuchumi na kuhamasisha maendeleo ya jamii yake etc. Tanzania haitaki mbunge anayewapa watu samaki e.g kugawa mahindi, bali anayewafundisha watu kuvua e.g kufundisha kanuni za kilimo bora/kuwapa elimu ya biashara ili wawe na maendeleo endelevu na sio maendeleo yanayomtegemea fulani, hivyo huyo fulani asipokuwepo basi hakuna maendeleo. So afanyecho Filikunjombe so far anajitahid ila aende beyond ili maendeleo ya wana Ludewa yawe endelevu na sio yategemee uwepo wa Filikunjombe ie. kugawiwa magari, kutoa sadaka kubwa, kulisha makutano wengi, etc
Kodi yote ya tanzania haiwezi hata kulipa mishahara ya watumishi. Wameomba ambulance wakaletewa bajaji kila wilaya. Watanzania hatuko productive na hatuko innovative, tunaishi kwa misaada ya wafadhili.Hii nchi tutaendelea kuwa masikini mpaka tutakapojuwa mipaka ya kimajukumu
Sasa kama mbunge ananunua ambulance hii maana yake ni kuwaambia wananchi "nimeshindwa kuisimamia serikali" sasa inabidi posho zangu ndio niwanunulie nyie............sasa mbunge kama huyu wa nini
Hii ni hulka mbaya ambayo imekaa kwa wanasiasa wote na inabidi tufike mahali wananchi tuwasaidie kufahamu tunataka wabunge wakuisimamia serikali na mambo ya kuletea ambulance iwe ni serikali (labda atoe kama mtu binafsi na sio kama mbunge kisha aje kutuambia kanunua ambulance kama mafanikio).
Lets not think ndani ya box
Watanzania thamani yetu ni ndogo sana. Kagari ka wagonjwa. Iwe ni mbunge wa CCM au chama kingine chochote, si kazi yake kununuwa gari la wagonjwa na kutangaza, ili iweje?
Rushwa ni za aina nyingi sana, hii ni mojawapo.
Nilitegemea wabunge wasimamie mambo mazito ya kubadilisha maisha ya watu.
1. Majukumu ya mbunge ni yapi?
2. Kuna umuhimu gani wa kujitangaza anapotoa msaada?. Hilo gari ni msaada, wala sio sehemu ya majukumu yake.
Hii nayo ni Rushwa!
Watanzania thamani yetu ni ndogo sana. Kagari ka wagonjwa. Iwe ni mbunge wa CCM au chama kingine chochote, si kazi yake kununuwa gari la wagonjwa na kutangaza, ili iweje?
Rushwa ni za aina nyingi sana, hii ni mojawapo.
Nilitegemea wabunge wasimamie mambo mazito ya kubadilisha maisha ya watu.