Ndugu zanguni,
Kama wote mjuavyo kuwa kama unataka uwe padri ni lazima uwe na moyop wa kusamehe, kusikiliza na Upendo. Kama ukishindwa kuwa nayo hayo matatu basi wewe huwezi kuwa mtumishi wa Mungu tena na inabidi ufukuzwe kwenye mafunzo ya upadre
Dr Slaa alisomea upadre na akashindwa, wengi hatujui ni kwa nini alishindwa hii kazi ya kutumikia kanisa na kuamua kuingia kwenye siasa . Lakini leo sote tumejua
Dr Slaa sio mtu wa kusamehe bali ni mtu wa visasi
Dr Slaa sio mtu wa kusikiliza maoni ya wanachama wake bali anapenda kusikia neno NDIO MZEE!
Dr Slaa sio mtu mwenye upendo kwani ameonyesha wazi jinsi anavyowachukia wanaompinga kwa kuwafukuza kama kuku. (Anasahau amri inayosema mpende adui yako)
Dr Slaa ni dikteta ndio maana maamuzi yake na ya Mbowe huwa ni ya kibabe zaidi biloa hata kujali demokrasia ya chama inasema nini.
Dr Slaa hawezi kuyafanyia matendo maneno anayohubiri ya kupiga vita ufisadi kwani yeye mwenyewe ni Fisadi namba moja.
Dr Slaa Mbowe na Lema ni hatari kwa Chadema na taifa kwa ujumla kwani wao ndio watakaoua upinzani ndani ya nchi kwa kusababisha migawanyiko kwa sababu ya tabia zao za kibinafsi na kikabila.
Ni wakati sasa kwa vijana wa Chadema kusimama na kujitambua.
Msikubali kuendeshwa kama misukule.
Dr utanisamehe, lakini nadhani ni wajibu wangu kusema ukweli kwani kama ulivyosema unafiki na uoga ni dhambi mbaya sana.
JITAMBUE!