Demokrasia inavyodumaza Maendeleo Afrika

Kazi juu ya viuno ndo mnaziweza wabongo! mkiambiwa fanyeni kazi za kuongeza kipato mnataka kuandamana eti OPERESHENI KATA FUNUA? Bashite piga kazi.
 
Kazi juu ya viuno ndo mnaziweza wabongo! mkiambiwa fanyeni kazi za kuongeza kipato mnataka kuandamana eti OPERESHENI KATA FUNUA? Seriously!! Diamond bora wewe umenyamaza!.
 
Adolf + Bismarck leo tunaona matokeo ya uchumi imara

George Washington leo tuonaina USA

B Munsolin leo tunaona brands za Italy

Mao Tsetung leo tunaiona China kama mkombozi wa Afrika

Sasa mtoa mada itabidi utupe reference za nchi gani ambayo afrika tunaweza kuitumia kama reference baada ya kutoa demokrasia

Tuanze na Uganda ilipoondoa demokrasia leo kuna legacy gani??
 
Fikiria kinchi kimepata uhuru miaka 50 iliyopita leo hii bado ni tegemezi kwa zaidi ya 50% ya bajeti yake na bado watu wake wanataka demokrasia, ipi? Napendekeza yafuatayo;
1. Kufuta Uchaguzi ili kutumia pesa zinazotengwa uchaguzi kujenga miundo mbinu, vituo vya afya na mashule.
2. Futa vyama pinzani maana hivyo ndivyo vinapummbaza watu (miluzi mingi....)
Afrika bado kufikia mambo ya demokrasia, wananchi wetu ni maskini sana hivyo kwa sasa wanahitaji maji, elimu, afya, barabara na si eti inayoitwa DEMOKRASIA, hivi mtu wa huko Lindi vijijini demokrasia yeye ya nn?
** USA imepata uhuru 4 july 1776 na bado demokrasia ya kweli (true democracy) hawajaifikia, wewe na SACCOS yako unadai eti unataka Demokrasia. Piga chini.
NB: Pia hizi imani zinaleta umaskini zaidi, watu wanadanganywa kuwa kuna muujiza katika kufanikiwa (maendeleo) wakati wengine wanakamuliwa pesa ya Hijja na wanabebeshwa mawe toka Afrika kwenda kumtwanga shetani huko umangani (ukihoji eti uhuru wa kuabudu).
Hebu niambie uhusiano wa demokrasia na bei ya sukari kuwa 2800/kg au sembe kuuzwa 2000/kg.
 
Bila demokrasia hakuna maendeleo ya kudumu na ya kuendelea.Hitler alifuta demokrasia ikawa amri kwa kwenda mbele akajenga viwanda na Ujerumani likawa Taifa lenye nguvu,nini kilifuatia?Libya ya Gadaf ilitoa mpaka pesa ya kuolea na kupewa nyumba,kusoma mpaka upeo wako,leo iko wapi?Saudi Arabia na nchi nyingine za kifalme ni suala la muda lakini madam demokrasia hakuna italipuka tu,second Arab spring itatokea.
Kuna wanaomuiga Kagame lakini madamu hajengi mfumo na anaibana demokrasia akiondoka Rwanda haitakuwa hiyo tunayoipigia mfano.
Hapa kwetu awamu ya tano baada ya joto la uchaguzi kutulia watu wangeendelea na demokrasia aliyoiacha Kikwete mambo yasingekuwa haya.
Wataalamu wa elimu jamii wanatufundisha kuwa unaweza kupeleka kitu kizuri lakini madam kinawanyima watu uhuru wao wanaweza kukichukia.
Funga macho na tafakari siku itakapokubaliwa mkutano wa upinzani katika jiji la Dar ni nini kitatokea?
 
Hebu niambie uhusiano wa demokrasia na bei ya sukari kuwa 2800/kg au sembe kuuzwa 2000/kg.

Uko tayari kweli kuambiwa na kutafakari uhalali ama ubatili wa utakachoambiwa? Kisha kuchukua hatua sahihi tokeo la Tafakari yako Huru?

Tumia muda wako kuitafakari dhana ya Soko Huria, kuihusisha na bidhaa zetu sokoni, na nafasi ya Serikali na Nguvu/uwezo wake halisi ulipo katika kusimamia hilo.

Wakati unatafakari hilo usisahau kuwa, Serikali kama Ofisi/Taasisi si mshindani katika biashara, ILA WALE WA NDANIYE NDIO VINARA KATIKA HUO USHINDANI, NAO NDIO WARATIBU NA WASHINDANI PIA. Huo ni Uhuru na Haki yao, Mnaita HAKI YETU KIKATIBA, mmesahau kuwa hatuna meno...

Anaita sasa.
 
Unajua nini maana ya nchi ya kidemokrasia.lazima nianzie hapo kwanza maana uliyoyaandika inaonekana hujui unachokiongea ndo maana umekazana na kufuta uchaguz,vinginevyo umekariri maana ya neno demokrasia bila kujua wenzako walimaanisha nn..Ngoja nikupe tafsiri nyepesi ya demokrasia.Demokrasia maana yake ni watu kusikilizana nakutenda vile walivyokubaliana kwa pamoja.Sasa niambie ni nchi gani iliwahi kuendelea kwa mawazo ya mtu mmoja.Tuanzie hapo.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Fikiria kinchi kimepata uhuru miaka 50 iliyopita leo hii bado ni tegemezi kwa zaidi ya 50% ya bajeti yake na bado watu wake wanataka demokrasia, ipi? Napendekeza yafuatayo;
1. Kufuta Uchaguzi ili kutumia pesa zinazotengwa uchaguzi kujenga miundo mbinu, vituo vya afya na mashule.
2. Futa vyama pinzani maana hivyo ndivyo vinapummbaza watu (miluzi mingi....)
Afrika bado kufikia mambo ya demokrasia, wananchi wetu ni maskini sana hivyo kwa sasa wanahitaji maji, elimu, afya, barabara na si eti inayoitwa DEMOKRASIA, hivi mtu wa huko Lindi vijijini demokrasia yeye ya nn?
** USA imepata uhuru 4 july 1776 na bado demokrasia ya kweli (true democracy) hawajaifikia, wewe na SACCOS yako unadai eti unataka Demokrasia. Piga chini.
NB: Pia hizi imani zinaleta umaskini zaidi, watu wanadanganywa kuwa kuna muujiza katika kufanikiwa (maendeleo) wakati wengine wanakamuliwa pesa ya Hijja na wanabebeshwa mawe toka Afrika kwenda kumtwanga shetani huko umangani (ukihoji eti uhuru wa kuabudu).
bangi tupu hivi weee mzeee afrika bara lenye utajiri usiomalizika mpaka kiyama na mijitu inakufaa njaa hapo demokrasi ya husu nini
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Afrika tunahitaji kunyooshwa zaidi. Tumezidi uvivu chini ya kivuli cha demkorasia. Fikiria vyama kama CHAGADEMA wanakula ruzuku ya mabilioni ya pesa/kodi za wanyonge kisha kutwa kuiponda serikali!!!
 
Utumwa na ukoloni ulitupora identity yetu. Leo hii Afrika haina dini wala model ya utawala wake. Sisi tunageza kila kitu cha watawala wetu. Navyofahamu mtu anaegeza hata siku moja hawezi kumshinda alieanzisha. No wonder wazungu na waarabu wanatawala akili zetu kama wanyama wao kupitia dini na tamaduni zao.
Asante mkuu kwa kulitambua hilo.
 
Democracy is an illusion. It is neither here nor there. It is just a way used by stronger nations to force their ideas down the throats of weaker nations. True democracy should be homegrown taking cultural, social and traditional aspects of a given society/nation into account.
Tumia lugha ya taifa kama mleta mada wote tukuelewe.
 
Huo ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka na wizi serikalini unafanywa na vyama vya upinzani? Na haya yanahusiana vipi na demokrasi?

Kwa Mobutu hakukuwa na demokrasi, kwa Mugabe hakuna demokrasi mbona nchi hizo hazikuwa/ hazina maendeleo yoyote yale!?

KAMWE demokrasi haiwezi kuwa kisingizio cha kukosa maendeleo nchini. Tunakosa maendeleo nchini kutokana na kuwa na viongozi wezi, mafisadi, wenye kuweka maslahi yao mbele badala ya Taifa, wenye kusaini mikataba isiyo na maslahi kwa Taifa chini ya uvungu, wasioshaurika, wenye kupindisha sheria mbali mbali za nchi, wenye kudharau Bunge na wakati mwingine kuwatisha Wabunge wa CCM kama ilivyotokea juzi baada ya mkutano wa Wabunge wa CCM na pia 2002 ambapo Wabunge wa CCM walikuja juu kutaka waione na kuijadili mikataba ya uchimbaji dhahabu.

Fisadi Mkapa akaamua kusafiri kwenda kuwanyamazisha sijui kwa kuwaambia nini na Wabunge wale hawakudai tena kutaka kuiona na kuijadili ile mikataba.

Toka mfumo wa vyama vingi kuanza ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na wizi serikalini umeongezeka kwa asilimia 1000
 
Fikiria kinchi kimepata uhuru miaka 50 iliyopita leo hii bado ni tegemezi kwa zaidi ya 50% ya bajeti yake na bado watu wake wanataka demokrasia, ipi? Napendekeza yafuatayo;
1. Kufuta Uchaguzi ili kutumia pesa zinazotengwa uchaguzi kujenga miundo mbinu, vituo vya afya na mashule.
2. Futa vyama pinzani maana hivyo ndivyo vinapummbaza watu (miluzi mingi....)
Afrika bado kufikia mambo ya demokrasia, wananchi wetu ni maskini sana hivyo kwa sasa wanahitaji maji, elimu, afya, barabara na si eti inayoitwa DEMOKRASIA, hivi mtu wa huko Lindi vijijini demokrasia yeye ya nn?
** USA imepata uhuru 4 july 1776 na bado demokrasia ya kweli (true democracy) hawajaifikia, wewe na SACCOS yako unadai eti unataka Demokrasia. Piga chini.
NB: Pia hizi imani zinaleta umaskini zaidi, watu wanadanganywa kuwa kuna muujiza katika kufanikiwa (maendeleo) wakati wengine wanakamuliwa pesa ya Hijja na wanabebeshwa mawe toka Afrika kwenda kumtwanga shetani huko umangani (ukihoji eti uhuru wa kuabudu).
uko sawa kabisa, 100%
 
ndio maana nchi kama china hawataki huo ujinga, eti democrasia, what is democracy? democrasia sio vyama vya siasa. Democrasia ya kweli ni pale selikali inapokuwa na ewezo wa kuhudumia watu wake.full stop. democrasia sio makanisa, sio misikiti, sio vyama vya siasa, Piga china makanisa, piga chini misikiti, piga chini mavyama, wote hawa ni wahuni tu wanaotumikia matumbo yao kwa gharama wa wananchi wajinga na walio masikini.
 
Huo ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka na wizi serikalini unafanywa na vyama vya upinzani? Na haya yanahusiana vipi na demokrasi?

Kwa Mobutu hakukuwa na demokrasi, kwa Mugabe hakuna demokrasi mbona nchi hizo hazikuwa/ hazina maendeleo yoyote yale!?

KAMWE demokrasi haiwezi kuwa kisingizio cha kukosa maendeleo nchini. Tunakosa maendeleo nchini kutokana na kuwa na viongozi wezi, mafisadi, wenye kuweka maslahi yao mbele badala ya Taifa, wenye kusaini mikataba isiyo na maslahi kwa Taifa chini ya uvungu, wasioshaurika, wenye kupindisha sheria mbali mbali za nchi, wenye kudharau Bunge na wakati mwingine kuwatisha Wabunge wa CCM kama ilivyotokea juzi baada ya mkutano wa Wabunge wa CCM na pia 2002 ambapo Wabunge wa CCM walikuja juu kutaka waione na kuijadili mikataba ya uchimbaji dhahabu.

Fisadi Mkapa akaamua kusafiri kwenda kuwanyamazisha sijui kwa kuwaambia nini na Wabunge wale hawakudai tena kutaka kuiona na kuijadili ile mikataba.
Ni kweli unachoongea maana yangu ni kwamba wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere hapa Tanzania ufisadi ulikuwa mdogo sana, akaja Rais Mwinyi akawa ni weakness ya kutokusanya kodi. Mambo yaliharibika wakati wa Rais Mkapa ubinafsisaji wa nyumba za serikali, NBC, mikataba mibovu ya serikali kwa migodi ya madini, shirika la posta na air tanzania kufa, alipokuja Rais Kikwete ndio mambo yakawa worse. Maana yangu ni kuwa wakati wa chama kimoja Tanzania haikuwa kama Zaire ya Mobutu ama Afrika ya kati ya Bokassa. Ukiangalia hata matumizi ya serikali wakati wa chama kimoja yalikuwa mazuri elimu na afya ilitolewa bure na nzuri.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom