Demokrasia inavyodumaza Maendeleo Afrika

Fikiria kinchi kimepata uhuru miaka 50 iliyopita leo hii bado ni tegemezi kwa zaidi ya 50% ya bajeti yake na bado watu wake wanataka demokrasia, ipi? Napendekeza yafuatayo;
1. Kufuta Uchaguzi ili kutumia pesa zinazotengwa uchaguzi kujenga miundo mbinu, vituo vya afya na mashule.
2. Futa vyama pinzani maana hivyo ndivyo vinapummbaza watu (miluzi mingi....)
Afrika bado kufikia mambo ya demokrasia, wananchi wetu ni maskini sana hivyo kwa sasa wanahitaji maji, elimu, afya, barabara na si eti inayoitwa DEMOKRASIA, hivi mtu wa huko Lindi vijijini demokrasia yeye ya nn?
** USA imepata uhuru 4 july 1776 na bado demokrasia ya kweli (true democracy) hawajaifikia, wewe na SACCOS yako unadai eti unataka Demokrasia. Piga chini.
NB: Pia hizi imani zinaleta umaskini zaidi, watu wanadanganywa kuwa kuna muujiza katika kufanikiwa (maendeleo) wakati wengine wanakamuliwa pesa ya Hijja na wanabebeshwa mawe toka Afrika kwenda kumtwanga shetani huko umangani (ukihoji eti uhuru wa kuabudu).

Demokrasisa haiji kwenye sahani. Ni lazima kuifanyia kazi. Maendeleo = 1) kupanuka kwa uhuru (watu kuendesha mambo yao kwa uhuru bila kuingiliwa na vyombo vya dola) na 2) uchumi (kuwa na maendeleo ya watu na vitu). Kwenye demokrasia kuna checks na balances ili serikali iwajibike zaidi kwa wananchi wake kwa kuwaletea maendeleo (kuboresha huduma za jamii). Kwenye demokrasia kuna pia ushirikishwaji wa wananchi katika maendeleo yao na pia serikali na viongozi wake inawajibika kwa wananchi. Kinyume cha demokrasia ni utawala wa mtu mmoja au kikundi kidogo cha watu, ambao wao ndio kila kitu na kila kitu ni wao. Kwenye utawala wa namna hii wananchi ndio wanaowajibika kwa serikali/watawala wao.
 
Mkuu kwa afrika hii tusidanganyane, demokrasia bado ina safari ndefu sana.

Mfano wa karibu ni CDM ya Mbowe, yupo kwenye uongozi kwa miaka 13 sasa, kama kweli ni chama cha demokrasia kwanini asitafutwe kiongozi mpya mwenye maono na malengo mapya?.

Hata hizi taasisi za kupigania demokrasia na masuala ya haki za binadamu, ukizitupia jicho la karibu utaubaini ukosefu mkubwa wa demokrasia.
Mkuu mbona hushangai CCM tuna miaka zaidi ya hamsini imeshindwa kutuondolea umasikini watanzania?
 
Mtoa hoja una fikra fupi juu ya demokrasia. Umasikini wa Africa huletwa na viongozi
 
Tanzania ya Viwanda yaja na haina nafasi kwa wanademokrasia.
 
Mkuu mbona hushangai CCM tuna miaka zaidi ya hamsini imeshindwa kutuondolea umasikini watanzania?
Umasikini unaanza kuuondoa kwanza kabisa nyumbani kwako. Kwenye kaya inayokuhusu.

Halafu baada ya hapo ndio unazungumzia mambo ya kisera. Kuuondoa umaskini imewachukua wamarekani miaka 240 wewe nguchiro mmoja kutoka Tanzania unataka kuuondoa umasikini ndani ya miaka 55, huo sio uhayawani kweli???.
 
Ungeniuliza mpaka nimefikia kusema hivi nilikuwa na maana ipi. Kuna pimbi mmoja kama wewe amenihoji kuwa chadema haijabadilisha kiongozi wa chama kwa muda sasa je imefikia maendeleo yapi?
Siku nyingine usikurupuke
 
Fikiria kinchi kimepata uhuru miaka 50 iliyopita leo hii bado ni tegemezi kwa zaidi ya 50% ya bajeti yake na bado watu wake wanataka demokrasia, ipi? Napendekeza yafuatayo;
1. Kufuta Uchaguzi ili kutumia pesa zinazotengwa uchaguzi kujenga miundo mbinu, vituo vya afya na mashule.
2. Futa vyama pinzani maana hivyo ndivyo vinapummbaza watu (miluzi mingi....)
Afrika bado kufikia mambo ya demokrasia, wananchi wetu ni maskini sana hivyo kwa sasa wanahitaji maji, elimu, afya, barabara na si eti inayoitwa DEMOKRASIA, hivi mtu wa huko Lindi vijijini demokrasia yeye ya nn?
** USA imepata uhuru 4 july 1776 na bado demokrasia ya kweli (true democracy) hawajaifikia, wewe na SACCOS yako unadai eti unataka Demokrasia. Piga chini.
NB: Pia hizi imani zinaleta umaskini zaidi, watu wanadanganywa kuwa kuna muujiza katika kufanikiwa (maendeleo) wakati wengine wanakamuliwa pesa ya Hijja na wanabebeshwa mawe toka Afrika kwenda kumtwanga shetani huko umangani (ukihoji eti uhuru wa kuabudu).
Wazungu walileta huu upuuzi ili wapumbavu wote wadumbukie humo, hujiulizi kwanini US na UK wana vyama viwili tundo vinapishana kwa hawamu. Ila nyinyi huku akina kapuku mna vyama mpaka vya mfukoni na vyote eti mnàvitunza. Vya kazi gani, huu upuuzi kwa faida ya nani?
 
Porojo na kucheza kwaito ndo matunda ya demokrasia uchwara za afrika. Paundwe makambi wananchi wapelekwe huko kulima na kufuga ili malighafi zitumike kuzalisha viwandani
 
Ungeniuliza mpaka nimefikia kusema hivi nilikuwa na maana ipi. Kuna pimbi mmoja kama wewe amenihoji kuwa chadema haijabadilisha kiongozi wa chama kwa muda sasa je imefikia maendeleo yapi?
Siku nyingine usikurupuke
Sihitaji kujua maana zilizo kichwani kwako, maelezo yako mafupi tu yanatosha kuonyesha ni jinsi gani upeo wako ulivyo.

CHADEMA na wewe wana tofauti gani?, mwenyekiti wa chama ana rundo la kashfa halafu mnajaribu kumtetea kijinga tu.

CHADEMA ina maendeleo gani ikiwa mwenyekiti anaambiwa akapime mkojo pale kwa mkemia mkuu wa serikali halafu anaingia mitini?.

Kuongea na wa aina yako wala haihitaji kukurupuka, mmeja humu ndani halafu kama kawaida huwa hamjielewi.
 
Vyama vingi viliingia kwa shinikizo LA weupe kwa madhumuni ya kulegeza umoja tuliokuwa nao. Na ukiangalia vizuri wamefanikiwa sana ktk hilo. Africa imeyumba sana chanzo ni ugonjwa unaoitwa democrasia
Mbona umekwepa kujikita kwenye swala la kuingiza familia za kifalme? maana hakuna uchaguzi, na pia kunapokua na utawala wa kifalme kunakua na watawala na watawaliwa, acha ujinga najua huelewi impact ya unachokisema pia unazungumza hicho kitu wakati nchi kama Tanzania haijaweza kujitegemea...always anaekupa kitu ndio anae amua wewe ufanye nini na nini usifanye? sasa civics ya form two ulisoma au uliacha shule from one?
 
Huyu ndugu mtoa mada hata kama watu mtamtukana lakini yuko sawa kwa asilimia 200..ukweli Tanzania na Africa nzima tunahitaji mambo makubwa mawili tu

1.Kufanya kazi kwa bidii na uchungu wa nchi zetu mpaka tufanikiwe

2.Kukataa kushikiwa akili na wazungu

Kama miaka mia moja hivi tutajikuta na wao wanakuja kutubembeleza wakitaka hiki na kile,wakiomba kujifunza kutoka kwetu,ukweli wa wazi hakuna maisha eti ya miujiza.kuna kufanikiwa kwa kupiga kazi tu kwa bidii na kua wazalendo.hebu fikili kitu hiki

Mtu anashinda kanisani au msikitini muda wote anaomba.mwingine anakosa pesa anauza mpaka alichonacho ili apeleke sadaka kwenye nyumba ya ibada,its ok kuamini MUNGU hatukatai.lakini tunaamini kitumwa na kufinywa kwa mawazo huku tukitiwa uoga mwingi wa eti siku ya mwisho itakua ya kusaga meno...alafu waliotuletea hizo dini wamekazana kulawitiana na masinagogi yao wameyageuza sehemu za starehe.nchi iliyopiga hatua kubwa kiuchumi hiyo ndiyo inayoweza kua na Demokrasia na siyo sisi..sisi ni mfano wa mtu masikini anaejaribu kunyoosha nguo zake za mitumba na akishazivaa anatembea kwa mikogo akijifananisha na mtu tajili ilihali amejaa shida
 
Fikiria kinchi kimepata uhuru miaka 50 iliyopita leo hii bado ni tegemezi kwa zaidi ya 50% ya bajeti yake na bado watu wake wanataka demokrasia, ipi? Napendekeza yafuatayo;
1. Kufuta Uchaguzi ili kutumia pesa zinazotengwa uchaguzi kujenga miundo mbinu, vituo vya afya na mashule.
2. Futa vyama pinzani maana hivyo ndivyo vinapummbaza watu (miluzi mingi....)
Afrika bado kufikia mambo ya demokrasia, wananchi wetu ni maskini sana hivyo kwa sasa wanahitaji maji, elimu, afya, barabara na si eti inayoitwa DEMOKRASIA, hivi mtu wa huko Lindi vijijini demokrasia yeye ya nn?
** USA imepata uhuru 4 july 1776 na bado demokrasia ya kweli (true democracy) hawajaifikia, wewe na SACCOS yako unadai eti unataka Demokrasia. Piga chini.
NB: Pia hizi imani zinaleta umaskini zaidi, watu wanadanganywa kuwa kuna muujiza katika kufanikiwa (maendeleo) wakati wengine wanakamuliwa pesa ya Hijja na wanabebeshwa mawe toka Afrika kwenda kumtwanga shetani huko umangani (ukihoji eti uhuru wa kuabudu).
Una umri gani? Vyama vya upinzani toka vianzishwe katika bara la afrika ni miaka 20 iliyopita, wakati tumeshajitawala miaka 40 tuonyeshe hayo maendeleo ya miaka 40 bila upinzani we bata.

Sent from my HTC One M9PLUS using JamiiForums mobile app
 
G'taxi umeeleza pweinti tupu. Afrika uvivu uliochagizwa na imani za dini ndo anguko letu.
 
Mbona umekwepa kujikita kwenye swala la kuingiza familia za kifalme? maana hakuna uchaguzi, na pia kunapokua na utawala wa kifalme kunakua na watawala na watawaliwa, acha ujinga najua huelewi impact ya unachokisema pia unazungumza hicho kitu wakati nchi kama Tanzania haijaweza kujitegemea...always anaekupa kitu ndio anae amua wewe ufanye nini na nini usifanye? sasa civics ya form two ulisoma au uliacha shule from one?
Hongera kwa elimu yako ya form 2. Ila jitahidi walau kuweka sawa maandishi. From = Form
 
Fikiria kinchi kimepata uhuru miaka 50 iliyopita leo hii bado ni tegemezi kwa zaidi ya 50% ya bajeti yake na bado watu wake wanataka demokrasia, ipi? Napendekeza yafuatayo;
1. Kufuta Uchaguzi ili kutumia pesa zinazotengwa uchaguzi kujenga miundo mbinu, vituo vya afya na mashule.
2. Futa vyama pinzani maana hivyo ndivyo vinapummbaza watu (miluzi mingi....)
Afrika bado kufikia mambo ya demokrasia, wananchi wetu ni maskini sana hivyo kwa sasa wanahitaji maji, elimu, afya, barabara na si eti inayoitwa DEMOKRASIA, hivi mtu wa huko Lindi vijijini demokrasia yeye ya nn?
** USA imepata uhuru 4 july 1776 na bado demokrasia ya kweli (true democracy) hawajaifikia, wewe na SACCOS yako unadai eti unataka Demokrasia. Piga chini.
NB: Pia hizi imani zinaleta umaskini zaidi, watu wanadanganywa kuwa kuna muujiza katika kufanikiwa (maendeleo) wakati wengine wanakamuliwa pesa ya Hijja na wanabebeshwa mawe toka Afrika kwenda kumtwanga shetani huko umangani (ukihoji eti uhuru wa kuabudu).
Hatuwezi kufikia malengo yetu ya kiuchumi kwa kasi kama tutaendelea kutoelewa aina ya democrasia tunayoiitaji.Hatuitaji democrasia ya kila mtu akubaliane na nchi inavyoendeshwa.Tufunge mkanda, tuwe na kiu ya maendeleo ya kiuchumi zaidi ya yale ya kisiasa.Siasa ndo kikwazi kikubwa africa.Bila kukontrol Mahakama,habari, na watumishi, maendeleo kwa kasi itakuwa ndoto.
 
hizi nchi za kiafrika Bila ku-control bunge, mahakama, vyama vya upinzani, watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla hatuwezi kutoka katika nchi maskini na zenye madeni lukuki zaidi duniani (Highly Indebted Poor Countries, HIPC)
 
Fikiria kinchi kimepata uhuru miaka 50 iliyopita leo hii bado ni tegemezi kwa zaidi ya 50% ya bajeti yake na bado watu wake wanataka demokrasia, ipi? Napendekeza yafuatayo;
1. Kufuta Uchaguzi ili kutumia pesa zinazotengwa uchaguzi kujenga miundo mbinu, vituo vya afya na mashule.
2. Futa vyama pinzani maana hivyo ndivyo vinapummbaza watu (miluzi mingi....)
Afrika bado kufikia mambo ya demokrasia, wananchi wetu ni maskini sana hivyo kwa sasa wanahitaji maji, elimu, afya, barabara na si eti inayoitwa DEMOKRASIA, hivi mtu wa huko Lindi vijijini demokrasia yeye ya nn?
** USA imepata uhuru 4 july 1776 na bado demokrasia ya kweli (true democracy) hawajaifikia, wewe na SACCOS yako unadai eti unataka Demokrasia. Piga chini.
NB: Pia hizi imani zinaleta umaskini zaidi, watu wanadanganywa kuwa kuna muujiza katika kufanikiwa (maendeleo) wakati wengine wanakamuliwa pesa ya Hijja na wanabebeshwa mawe toka Afrika kwenda kumtwanga shetani huko umangani (ukihoji eti uhuru wa kuabudu).
Wazo zuri.....how about check and balances? Unafikiri watawala wakiachwa hivi hivi bila kelele kidogo watatenda kwa maslahi ya walio wengi?
 
Wazo zuri.....how about check and balance? Unafikiti watawala wakiachwa hivi hivi bila kelele kidogo watatenda kwa maslahi ya walio wengi?
Hakunaga kitu kinaitwa "checks and balance" kwenye uhalisia, (Kaimu) jaji mkuu (mkuu wa mahakama) anateuliwa na rais, Spika wa bunge, ni mwanachama wa chama tawala ambapo rais ndo Mwenyekiti. Tujikite kwenye kilmo tu. Mengine mbele kwa mbele.
 
Back
Top Bottom