Demokrasia inavyodumaza Maendeleo Afrika

Michewen

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
24,551
32,175
Fikiria nchi imepata uhuru miaka 50 iliyopita leo hii bado ni tegemezi kwa zaidi ya 50% ya bajeti yake na bado watu wake wanataka demokrasia, ipi? Napendekeza yafuatayo;

1. Kufuta Uchaguzi ili kutumia pesa zinazotengwa uchaguzi kujenga miundo mbinu, vituo vya afya na mashule.

2. Futa vyama pinzani maana hivyo ndivyo vinapummbaza watu (miluzi mingi....)

Afrika bado kufikia mambo ya demokrasia, wananchi wetu ni maskini sana hivyo kwa sasa wanahitaji maji, elimu, afya, barabara na si eti inayoitwa DEMOKRASIA, hivi mtu wa huko Lindi vijijini demokrasia yeye ya nn?

** USA imepata uhuru 4 july 1776 na bado demokrasia ya kweli (true democracy) hawajaifikia, wewe na SACCOS yako unadai eti unataka Demokrasia. Piga chini.

NB: Pia hizi imani zinaleta umaskini zaidi, watu wanadanganywa kuwa kuna muujiza katika kufanikiwa (maendeleo) wakati wengine wanakamuliwa pesa wanakosa mpaka ada ya kuwalipia watoto wao Chuo kikuu (ukihoji eti uhuru wa kuabudu).
 

Attachments

  • VID-20200723-WA0000.mp4
    2.5 MB
Una uhakika pesa zitakazo okolewa katika gharama za demokrasi zitaelekezwa kwenye masuala ya maendeleo ya watu? Nani atakayefanya uamuzi huo, atapatikana aje ili apewe dhamana hiyo? Atawajibika/wajibishwa na nani katika utendaji wake?
 
Nakubaliana kabisa na wewe mtoa mada!

Tatizo ni moja, kwa kuwa tulikubali kama taifa kufuata demokrasia, basi inabidi tuiishi, na siyo kudanganyana.

Alternatively, bwana mkubwa atangaze kwamba Tanzana sasa siyo nchi ya kidemokrasia. It is that SIMPLE.

Lakini akiendelea kujificha chini ya stuli ya demokrasia, huku akiwa autocratic, basi nasi tutaendelea kumsema mpaka ukichaa wake ufikie level ya kupelekwa Mirembe. Na tena asivyoweza kujizuia kusoma posts zetu, ni raha mtupu.
 
Brother why don't you shut up and sleep kama una stress zako usijaribu kutupa nasisi.... The first thing is kwanza umejidharau kuona rangi yako haifai na unajaribu kuembrace udikteta, democracy is what made America where it is today, the only thing ambayo unaita demokrasia kwetu haipo na wala haijakuwepo.

Ukiona chama pinzani kinashinda uchaguzi (mfano Zanzibar) the next day una unull matokeo demokrasia hakuna, ukiona mwenyekiti wa tume anachaguliwa na kiongozi anaetawala definitely hakuna demokrasia.

Wapinzani Africa hajitambui kwakuwa wanatumiwa na vyama tawala kujificha nyuma ya mgongo wa demokrasia ili nchi iendelee kupata misaada but na ushenzi wote wanafanya watawala hawawezi kuvifuta coz wanavihitaji zaidi kuonekana huko magharibi wanademokrasia.
 
Waafrika maana ya demokrasia kwao ni;
1. Kuzaa bila mpangilio;
2. Kulalamika bila kutimiza wajibu (Vyama pinzani)
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
 
Hao wanaotoa misaada wameendelea kwa sababu ya demokrasia. Nitajie hata nchi moja iliyo first world ambayo haina demokrasia.
 
Hao wanaotoa misaada wameendelea kwa sababu ya demokrasia. Nitajie hata nchi moja iliyo first world ambayo haina demokrasia.
1. United Kingdom, nielezee demokrasia yao ilipo. Ningeweka na Uchi-na lakini haipo First world (so naiondoa) twende na UK kwanza.
 
UK waliopiga kura ya brexit juzi unasema hawana democracy?

Unajua PM wao ni mpaka athibitishwe na nani? Na ni lazima awe MKRISTO tena ANGLICAN. Hapo kuna demokrasia? Ficha upumbavu wako ndg. usije kukuta umesoma ile shule pale karibu na Shaurimoyo pamoja na ndugu yako Maulida Khanga ambae anamzuia askari kutimiza wajibu wake. Asirudie tena maana yule askari alikuwa mstaarabu sana. Vinginevyo Maulida alipaswa kuwa sehemu salama kwa sasa kama mgeni maalum akirekebishwa tabia.

**Hizi dini zinawafanyaje aisee mbona ubongo mzito hivyooo
 
Narudia tena, Watanzania ni wavivu mno, lazima kufundishwa namna ya kufanya kazi kwa bidii na nidhamu. Umbea hautusaidii
 
Kitu ambacho hukijui ni kwamba maendeleo ya USA unayotaona yameanza kuja baada ya kuanza kwa Demokrasia na yamekuwa kwa kasi baada ya kuimarika kwa demokrasia. Ndio maana kwao hawana hicho unachoita wewe "upinzani" wala "chama tawala". Haya ni maneno ya kikoloni na ya kipuuzi ambayo msingi wake ni kubagua watu wa nchi moja katika makundi tofauti kwa itikadi za kichama.

Nadhani hoja yako ingekuwa na mashiko kama ungelihoji iweje serikali za kiafrika zijiibie zenyewe? Yaani zinaandaa uchaguzi kwa gharama huku hawakubaliani na matokeo ya uchaguzi huo. Huu ndio udhaifu wa kiafrika ambapo kila aliyeko madarakani anajiona yeye ndio alpha na omega.

Ukweli ni kwamba Denokrasia ya kweli ndiyo njia sahihi ya kuleta maendeleo kwa haraka kwasababu human nature ni kutopenda kuwa defeated. Lakini pia binadamu kiasili ili kuwajibika ni lazima pawepo mtu au kitu ambacho atakuwa anawajibika kwayo.

Mfumo wa demokrasia iliyo komaa, namna pekee ya watu kuendelea kukupa ushindi ni kukidhi matakwa ya watu, au kuwajibika na matatizo ya wapiga kura. Nje ya Demokrasia, kiongozi hawajibiki popote hivyo hana sababu ya kuwajibika na hivyo hana sababu ya kutimiza matakwa ya kijamii. Na matokeo yake umaskini. Hii ndio sababu ya umaskini wa Afrika. Viongozi kutoamini mamlaka za kuwajibika na hivyo hawana sababu ya kutekeleza matakwa ya nchi. Hujachelewa rudi tena shule.
 
Una uhakika pesa zitakazo okolewa katika gharama za demokrasi zitaelekezwa kwenye masuala ya maendeleo ya watu? Nani atakayefanya uamuzi huo, atapatikana aje ili apewe dhamana hiyo? Atawajibika/wajibishwa na nani katika utendaji wake?
hizo fedha za demokrasia badala yake zitaenda kununua silaha
 
Back
Top Bottom