Mwana wa Mungu
JF-Expert Member
- Aug 14, 2008
- 1,003
- 83
tatizo, hili jambo halikuwa kwa watu wote ninyi, lilikuwa kwa watz wachache ambao ni walokole, hata halikuwa linawahusu. Tumewahusisha mmeanza kutuchefua? Tutarudisha liwe kwa walokole tu. Sisi kama walokole tunaridhika, na maadam tumesha vuna kwa mara nyingi tukapata faida, hatuna shida. Hata ikiisha leo hatuna hasara. Pilipili usoila inawawashia nini? Wanaotumia wamenyamaza kimya, ninyi ambao hamjatumia mnaongea. Mnaweza mkamkomvisi vipi mtu ambaye ameshavuna pesa mara kibao, aliweka laki mbili amesha vuna mle takribani million nne tayari, sasa. Tunapata faida, na hatutaiacha, na hata kama watu watasema sana, mnachelewa bure, mtasema matokeo yake mtakuja kuujua ukweli wake muda wakati umeisha na ninyi nafasi ya kufaidika imefungwa. Kalaga baho.
c. Sasa Benki haiwezi kutoa fedha tu za faida bila yenyewe kutengeneza faida vile vile. Hivyo kwenye hii DECI maswali yanayokuja ni kwamba hao jamaa wao wanapata faida gani?
TATIZO:
Kwa kadiri ya kwamba mtindo huo unategemea wateja wapya na unaendelea kuahidi mavuno makubwa, basi hatima yake ni kuanguka au kuporomoka kwani baada ya watu wote kujiunga na mtandao huo wale wanaoingia mwisho watajikuta hakuna wa kuwalipa wakati wale walioingia mwanzoni watakuwa wameshakuwa matajiri wa haraka haraka!
QUOTE]
HAPO TU MIMI PAMETOSHA KABISA KUNIFUNGUA MACHO!haswa haswa.KWENYE TATIZO.
sasa wanajamii wenzangu tuwasaidie wenzetu wasio na access ya mtandao!walau kutoa ANGALIZO KWA WATU WAWILI TU,ili taarifa zisambae
Unajaribu kutuaminisha kuwa walokole ni malaika? Kama umekiri kuwa sasa walokole wako kwenye madhehebu mengi, na kama unakumbuka kuwa kuna baadhi ya wachungaji walokole ambao wako jela au kesi zao bado zinaendelea kwa makosa ya wizi, una ushahidi gani wa kutueleza kuwa hawa ni tofauti? Ningefurahi sana kama ungejibu hoja za watu wenye wasi wasi na DECI badala ya kutuletea hadithi za walokole katika mambo ambayo yanaonekana ni wizi mtupu!!
nina mashaka na ulokole wako. Yesu hakuwa mfanyibiashara, asilani. Na hakutumia dini wala sinagogi kufanyia biashara. Bali nyumba ya baba yake itaitwa nyumba ya sala, yaonekana mmegeuza kuwa pango la wachuuza fedha!
It is unclear, but it was used in a study by America's Federal Reserve bank as far back as 1967.tunaweza kuassume kuwa hawa DECI ni kama wale watumishi waliopewa Talanta na bwana wao. Mmoja talanta 5000, mwingine 1000 na mwingine 100. Yule bwana aliporudi kutoka safari ya mbali aliwaita wote na kuwauliza "mlifanyia nini talanta zile, leteni mahesabu yenu".
yule wa Talanta 5000 akasema "bwana mimi nilianzisha kituo cha mafuta, duka la viyoyozi na pia nimejenga shule ya chekechekea". Akaendelea "kutoka zile talanta 5000, nimepata faida ya talanta 10,000 so hizi hapa hela zako.
Akamwita yule wa pili, naye akasema "mimi nilianzisha ujasiriamali wa shamba la vitunguu kwenye mabonde ya Tukuyu, na pia nimelima viazi na kutoka zile zile talanta 1000 nimekuwa nikiagiza matunda toka kwa Mkapa huko Lushoto. Kutokana na kiasi kile nimepata faida ya talanta 5000!, hizi hapa fedha zako".
Yule bwana akamuita yule aliyepewa talanta 100 naye atoe hesabu zake. Yeye akaja na kusema "bwana mimi nilijua wewe ni mtu katili, unakula usivyopika, na unavuna usivyopanda. Kwa kukugwaya wewe niliamua kuzifukia ardhini hadi utakaporudi".
Yule bwana akamuuliza "haya nipe kilicho changu". Jamaa akasema "twende mnisaidie kufukua."
Walipoenda na kufukua wakakuta talanta 100 zimeongezeka na kuwa talanta 100,000!
Yule bwana akamuuliza "umewezaje hili?"
Yule mtumishi akasema "nilianzisha mchezo wa Deci!"
Bwana akashikwa na mshangao akamuambia "hakika na wewe ni fisadi!"
Swala la DECI mie nadhani uwaachie wahusika kwa sababu najua kwamba mpaka mtu afikie hatua ya kutoa fedha zake na kujiunga atakuw ana akili timamu.
Kwenda DECI hulazimishwi sasa ambacho chakutia wasiwasi ni nini? Ninchokushauri wewe ni kufanya uchunguzi then ndo uje umwage data zako.
"No Research, No Right to speak"
Mugerezi,
Wewe ulipanda shilingi ngapi na mpaka sasa umeshavuna bei gani kama faida ...July 08 to date?
hahaha, we ni kaduguda kweli. kwasababu ulichoandika hakina hata mantiki. kwa taarifa yako, Yesu anataka watu wawe matajiri, alileta uhuru tutoke kwenye umasikini twende kwenye utajiri. alikuja kutukomboa na utumikishwaji wa shetani anayependa watu waamini kuwa shetani na uchawi ndio huleta utajiri. Yesu anataka watu waone na kuamini kuwa mtu anaweza kutajirika bila kutumia kiungo cha albino wala kusoma kuran ili kuita majini ya kuiba nyota za watu. ndio maana hata sasa, watu wengi wanatajirika bila hata kutumia uchawi wala nini. wanafanya biashara na wanafanikiwa sana, na Yesu anawasaidia kufanya izo biashara. watu wapinga kristo kama wewe ndio vibaraka wa shetani, hutumiwa na mwovu kupinga mambo ya Mungu. pata hiyo?