Dear ladies...

Reward ya huyo mjane wake Ni nini hasa Kwa kuvumilia ushenzi wa mume wake aliefia kwenye kifua cha mwanamke mwenye umri sawa na mjukuu wake?

Wanawake wanapata nini kuvumilia mabaya ya waume zao Zaidi ya presha, msongo wa mawazo na aibu?
Utaitwa feminist na single maza, haha unaijua JF wewe? Nawapenda binadamu wanaosimamia mitazamo yao bila kujali wangapi watapenda wangapi hawatapenda, Hongera.
 
Ukielewa hii principle hlf ukapata mwanaume sahihi


Watu watasema umemloga na kweli ni haki yao kusema hivyo maana utafanyiwa makubwa sana...
 
Utaitwa feminist na single maza, haha unaijua JF wewe? Nawapenda binadamu wanaosimamia mitazamo yao bila kujali wangapi watapenda wangapi hawatapenda, Hongera.
Hahah hata nikiitwa, sioni tusi liko wapi. Wakiweza kunijibu tunanufaika na nini kusamehe upuuzi huu then i can reconsider my opinion lakini kwa sasa naona huu uzi unapotosha sana.

Ntatoa mawazo yangu sababu najua mabinti wengi wanapitia humu kimya kimya wanasoma kinachoandikwa na asilimia nyingi nyuzi kama hizi zinapotosha. Lazima hivi vitu vitamkwe wazi ili wajue it doesn't have to be this way.
 
Usishindane na mwanaume...Hiyo Vita kushinda inawezekana but at what cost?

Sijawai Amini katika Mungu katika maisha yangu..Kama navyomuanini Sasa...Anatenda pale ambapo unaona kabisa haiwezekani Mungu haishiwi mbinu..

Japo tunabezwa kwa kujifanya wacha Mungu...But Mimi SITAKI KURUDI nyuma katika Imani yangu ..
Nawasihi wadada wenzangu Mmche Mungu kwa kumaanisha.

Wallahi naapa...Amtagemea Mungu ..Mungu humfanyia njia pale ambapo Katika macho ya Mwanadamu ..hakuna njia.

Hakika kwa Mungu mambo Ni mepesi Sana ..Ni kusema TU kun faya Kun.

Athiest Sitaki mabishano
Kuna silaha kubwa sana MUNGU amewapatia all Ladies out there ila niwenye busara tu ndio hufunuliwa neema hiyo, mwanaume ni kiumbe strong lakini pia ni kiumbe dhaifu kama mwanamke akiongea nae maneno mazuri sana no matter what affair yao iko vibaya either kwa mambo ya michepuko etc na bado mwanamke akavumilia na kuongea na mpenzi wake kwa lugha laini na yastaha amini usiamini Mume lazima atapata guilty conciseness na moyo wake utalainika kama biscuit na kumrudia mke wake na maisha yakaendelea
 
Hope mko poa...

Niwaibie siri mwenye maskio na asikie. Jamani siku hizi kuna kamsemo, "mwanaume akimwaga mboga we mwaga ugali ikiwezekana mwaga hadi maji ya kunawa".

Jaman mwanamke asiposimama imara dunia yote inayumba, kamwe kwenye maisha yako usimlipe mwanaume ubaya kwa ubaya anaokutendea!!

Nitawaambia kwanini...

Mungu alivotuumba ametuumba in search an amazing way. Mioyo yetu na akili zetu zinasemehe na kusahau kwa haraka sana.

Kwa mlioingia leba kwa yale maumivu ya leba sidhani kama kuna mtu angekua anaruhusu mwanaume ampatie tena mimba nyingine lakini huwa tunasahau, na unakuta mwingine mwaka mimba, mwaka mtoto. Tumeumbwa hivyo kuumia, kusamehe, kusahau na kuendelea mbele.

Kuna nguvu kubwa sana kumvumilia mwanaume anayekuumiza bila kumlipa ubaya.

NB: SIZUNGUMZII MA BOYFRIEND WALA WANAUME WANAOPIGA WAKE ZAO NA WALE WANAOWAINGILIA WAKE ZAO KINYUME NA MAUMBILE AISEE KAMA ANA SIFA IZI KIMBIA VIBAYA MNO. PIA NAMUONGELEA MUME WAKO WA NDOA.

Unapovumilia na kumlilia Mungu juu ya matatizo yako kuhusu mumeo Mungu anashughulika mwenyewe katika kumrekebisha, lakini unaposema akichepuka na mi nachepuka unampa shetani nafasi ya kuitawala ndoa yako

Jamani uvumilivu unauma, uvumilivu unagharama lakini atakayevumilia mpaka mwisho ataokoka

Mwanaume wa kumwombea Mungu akiamua kumrejesha anamrejesha kwa machozi na kamasi na magoti juu.

Dear ladies muombee usichoke, achana na wanaosema akimwaga mboga mwaga ugali. Mimi leo nakwambia akimwaga mboga nenda jikoni kapike zingine na umuite kula. Kuna nguvu katika upendo inayoweza kuhamisha milima.

Usishindane na huyo baba, mlilie Mungu aliyekupa atamnyoosha, trust me! Zipo shuhuda kibao mwanaume anahama hadi nyumba lakini mwanamke badala ya kutaka kukomoa na yeye ajioneshe ni mzuri alikaa alilia na Mungu Hadi Mungu akamrejesha.

Ni wakati wa wanawake wa Mungu kusimama, wanawake wanaovumilia, wanaoheshimu mahali wanapodharaulika, wanaosamehe bila kuhesabu.

Simamia nyumba yako, irejeshe amani iliyopotea, omba bila kukoma.
hakika ww ni mwanamke..
 
Mwisho wa siku hakuna taji, za kuambiwa changanya na zako.

I can’t live half of my life unhappy because of someone else
Badala nijiombee mwenyewe na wanangu malengo yangu etc nichakae kuhusu mume aisee hii si kumkomoa ila ni kuendelea na maisha yangu mengine mwanaume ni part tu ya maisha
 
Back
Top Bottom