Dear ladies...

pisi jacky

Member
Oct 21, 2020
31
150
Hope mko poa...

Niwaibie siri mwenye maskio na asikie. Jamani siku hizi kuna kamsemo, "mwanaume akimwaga mboga we mwaga ugali ikiwezekana mwaga hadi maji ya kunawa".

Jaman mwanamke asiposimama imara dunia yote inayumba, kamwe kwenye maisha yako usimlipe mwanaume ubaya kwa ubaya anaokutendea!!

Nitawaambia kwanini...

Mungu alivotuumba ametuumba in search an amazing way. Mioyo yetu na akili zetu zinasemehe na kusahau kwa haraka sana.

Kwa mlioingia leba kwa yale maumivu ya leba sidhani kama kuna mtu angekua anaruhusu mwanaume ampatie tena mimba nyingine lakini huwa tunasahau, na unakuta mwingine mwaka mimba, mwaka mtoto. Tumeumbwa hivyo kuumia, kusamehe, kusahau na kuendelea mbele.

Kuna nguvu kubwa sana kumvumilia mwanaume anayekuumiza bila kumlipa ubaya.

NB: SIZUNGUMZII MA BOYFRIEND WALA WANAUME WANAOPIGA WAKE ZAO NA WALE WANAOWAINGILIA WAKE ZAO KINYUME NA MAUMBILE AISEE KAMA ANA SIFA IZI KIMBIA VIBAYA MNO. PIA NAMUONGELEA MUME WAKO WA NDOA.

Unapovumilia na kumlilia Mungu juu ya matatizo yako kuhusu mumeo Mungu anashughulika mwenyewe katika kumrekebisha, lakini unaposema akichepuka na mi nachepuka unampa shetani nafasi ya kuitawala ndoa yako

Jamani uvumilivu unauma, uvumilivu unagharama lakini atakayevumilia mpaka mwisho ataokoka

Mwanaume wa kumwombea Mungu akiamua kumrejesha anamrejesha kwa machozi na kamasi na magoti juu.

Dear ladies muombee usichoke, achana na wanaosema akimwaga mboga mwaga ugali. Mimi leo nakwambia akimwaga mboga nenda jikoni kapike zingine na umuite kula. Kuna nguvu katika upendo inayoweza kuhamisha milima.

Usishindane na huyo baba, mlilie Mungu aliyekupa atamnyoosha, trust me! Zipo shuhuda kibao mwanaume anahama hadi nyumba lakini mwanamke badala ya kutaka kukomoa na yeye ajioneshe ni mzuri alikaa alilia na Mungu Hadi Mungu akamrejesha.

Ni wakati wa wanawake wa Mungu kusimama, wanawake wanaovumilia, wanaoheshimu mahali wanapodharaulika, wanaosamehe bila kuhesabu.

Simamia nyumba yako, irejeshe amani iliyopotea, omba bila kukoma.
 

Quetzal

JF-Expert Member
Dec 9, 2018
5,258
2,000
Usishindane na mwanaume...Hiyo Vita kushinda inawezekana but at what cost?

Sijawai Amini katika Mungu katika maisha yangu..Kama navyomuanini Sasa...Anatenda pale ambapo unaona kabisa haiwezekani Mungu haishiwi mbinu..

Japo tunabezwa kwa kujifanya wacha Mungu...But Mimi SITAKI KURUDI nyuma katika Imani yangu ..
Nawasihi wadada wenzangu Mmche Mungu kwa kumaanisha.

Wallahi naapa...Amtagemea Mungu ..Mungu humfanyia njia pale ambapo Katika macho ya Mwanadamu ..hakuna njia.

Hakika kwa Mungu mambo Ni mepesi Sana ..Ni kusema TU kun faya Kun.

Athiest Sitaki mabishano
 

Quetzal

JF-Expert Member
Dec 9, 2018
5,258
2,000
Dada pisi Kali...Nakubaliana kabisa na Wewe...yaaani umeongea ukweli kabisa..

Put your trust in Allah....He will provide for you in ways you didn't anticipate.

Na usikate tamaa...Ukasema mbona Mungu anachelewa kujibu....Mungu ndie Alie kuumba anajua unaihitaji Nini na kwa wakati gani...

He is all knowing, He is the wise.. He is the best of planners, The provider of Rizk etc

Na Mimi naamini Mungu ndo anaamrisha flani mpende Fulani..

NAAMINI KATIKA MUNGU WANGU BILA SHAKA......yaaani Naweza andika sana
 

MLEVi Mmoja

JF-Expert Member
Jun 29, 2019
7,032
2,000
Ila uvumilivu ni kitu muhimu sana yule mzee wa miaka 80 aliefia gesti alishindwa kujizuia kabisa alishindwa kuwa na uvumilivu anajikuta

Anakojoa mpka roho
 

Quetzal

JF-Expert Member
Dec 9, 2018
5,258
2,000
Kuna wanawake wanasema... mwanaume Sio lazima eti kuwa nae..
Doooh....
. WAACHENI wakeshe kwa Mwamposa na Madhabauni..
kumpata mwanaume sahihi katika maisha yako... Ni Jambo la kushukuru Sana.

Mwanaume na AHESHIMIWE.... Man are important to us we value them...
 

Eli79

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
28,341
2,000
Usishindane na mwanaume...Hiyo Vita kushinda inawezekana but at what cost?

Sijawai Amini katika Mungu katika maisha yangu..Kama navyomuanini Sasa...Anatenda pale ambapo unaona kabisa haiwezekani Mungu haishiwi mbinu..

Japo tunabezwa kwa kujifanya wacha Mungu...But Mimi SITAKI KURUDI nyuma katika Imani yangu ..
Nawasihi wadada wenzangu Mmche Mungu kwa kumaanisha.

Wallahi naapa...Amtagemea Mungu ..Mungu humfanyia njia pale ambapo Katika macho ya Mwanadamu ..hakuna njia.

Hakika kwa Mungu mambo Ni mepesi Sana ..Ni kusema TU kun faya Kun.

Athiest Sitaki mabishano
Mungu yupi huyo? Sema nature!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom