DCs wapanguliwa na kustaafishwa

Kwa mtazamo wangu, tunahitaji kuwa na package nzima ya hatua zisizo za kawaida zitakazochukuliwa kukabiliana na tatizo hili lisilo la kawaida.

Na zipo nyingi tu zinazoweza kuchukuliwa. Kwa mfano; kwa nini Kikwete asilete mabadiliko katika serikali yake kwa kui-structure upya? Hivi katika anguko hili la uchumi wa dunia ambalo athari zake zitadumu kwa zaidi ya miaka mitano, bado tunaihitaji structure hii ya sasa ya uongozi yenye mawaziri, manaibu mawazi, makatibu wakuu, manaibu makatibu wakuu, wakurugenzi, manaibu wakurugenzi, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, ma-DED, ma-Ras nk?

Hayo yaliandikwa na Mwandishi bingwa nchini Johnson Mwambo Feb 4, mwaka huu, akizungumzia tatizo la anguko la uchumi na hatua madhubuti za kuchukua.

Inapotokea ?donor? wetu naye anakopa IMF?

Laiti viongozi wetu wangekuwa alau wanasikiliza!

NN.
 
Yetu macho watu ni walewale na tabia zao zilezile,tofauti ni majina na sehemu.
Tusilaumu matokeo tulaumu fomula inayopelekea hayo matokeo.
Kama mchakato una walakini tusitegemee matokeo tofauti.Ni vigumu hasa kama hakuna mchakato wa wazi wa kuwapata hawa mabwana na mabibi.Pengine ni wakati muafaka kwa kazi zote za kiutendaji kushindaniwa na hatimaye kufanyika uteuzi based on meritocrity.
 
Huyu Dc aliyestaafishwa wa Mbalari aliwahi kuwachapa vibao wafugaji mbele ya wajumbe wakati wa kampeni ya kuondoa mifugo Ihefu,je naye analindwa na katiba? Kimsingi inabidi awajibike kwa kitendo alichofanya cha udhalilishaji.
 
Huyu Dc aliyestaafishwa wa Mbalari aliwahi kuwachapa vibao wafugaji mbele ya wajumbe wakati wa kampeni ya kuondoa mifugo Ihefu,je naye analindwa na katiba? Kimsingi inabidi awajibike kwa kitendo alichofanya cha udhalilishaji.
Mkuu Malila,

Ndio wamemuadabisha hivyo. Tendo lile halikuleta munkari sana kwa jamii kama lile la DC wa Bukoba. Kwa Serikali hii, lile lilivumilika kidogo kuliko hili la Bukoba. Sijui kwa kigezo kipi?
 
Muungwana ni kilaza na mvivu. Imefika mahali sasa washauri wake wanaweza kumchagua yeyote kushika nafasi yeyote na wanajua jamaa hawezi hata kuuliza huyu amechaguliwaje.

Wakuu wa wilaya hawana kazi zaidi ya kupiga politics tuuu na kuandaa ground ya kufanyia wizi wakati wa uchaguzi

Kama tunataka maendeleo vijijini, maDED wanatosha sana kufanya kazi hii - kama wangekuwa wanateuliwa kufuata uwezo kiutendaji
 

Wakuu wa Wilaya ambao wamepangiwa kupewa kazi nyingine ni Bw. Patrick Tsere aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala (Dar es Salaam) na Bi. Doreen Kisamo aliyekuwa Uyui (Tabora).


Wamkataa DC mbele ya Mkuu wa mkoa!
Wakazi wa Kata ya Kipawa jana walimwambia mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Abass Kandoro kuwa hawamtaki mkuu wao wa wilaya, Patrick Tsere kwa madai kuwa ameshindwa kushughulikia madai yao na kutaka eneo hilo litangazwe kuwa "janga la kitaifa".

Wakazi hao, ambao jana waliandamana hadi ofisi za Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) zilizo Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, wanaishinikiza serikali kuwalipa fidia baada ya kuzuiwa kuendeleza makazi yao kwa takriban miaka 12 kwa sababu za upanuzi wa uwanja huo.

Wakazi hao walikuwa wamebeba mabango yenye ujumbe kama "rais na waziri mkuu ogopeni Mungu kwa kutuwekea alama za X, wajabika" na mwingine uliomtaka Waziri wa Miundo Mbinu, Shukuru Kawambwa kutimiza ahadi zake na pia kumtaka mkurugenzi wa TAA, Prosper Tesha kujiuzulu kutokana na kuwasababisha usumbufu.

Kandoro, ambaye alienda eneo hilo kwa lengo la kuongea nao baada ya kutaarifiwa kuwa wakazi hao wameandamana, alikuwa ameambatana na Tsere kuwasikiliza, lakini akakumbana na kauli kali kutoka kwa wananchi hao.

Akizungumza mbele ya Kandoro na Tsere, mwenyekiti wa wakazi wa Kipawa, Magnus Mulisa alisema Tsere amekuwa akitoa ahadi za uongo na kwamba ndiye aliyeshindwa kuwasaidia na kusababisha wahangaike.

"Tsere hajawahi kututembelea hata siku moja," alisema Mulisa bila ya kuonyesha woga huku Tsere akionekana kuwa na wasiwasi. "Ameonyesha kutudharau na anataka kutengeneza mbinu ya kutugawa kutokana na kuwakataa wahanga wenzetu wa Kigilagila na Kipunguni kuhudhuria mkutano wa kamati ya wakazi hao aliouitisha Ijumaa ofisini kwake.


"Alitudanganya kuwa angehudhuria mkutano wa wanachi uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Kipawa, lakini badala yake akamtuma mwakilishi."


Siku hiyo, mwakilishi huyo, Mathias Miyenjwa aliwekwa chini ya ulinzi na wananchi hao hadi alipookolewa na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).


Wakazi hao pia walimtaka Kandoro awaeleze ni lini watalipwa fidia zao ambazo wamekuwa wakisubiri kwa miaka 12 tangu serikali ilipowazuia kuendeleza makazi yao kwa maelezo kuwa ilikuwa inataka kupanua uwanja huo wa kimataifa wa ndege.


Hata hivyo, Kandoro alikataa kutoa majibu na badala yake akaeleza kuwa dhamira yake kwenda eneo hilo ilikuwa kuwasikiliza ili ajue kwa kina tatizo lao kabla hajachukua hatua.

"Nimesikia uchungu kuwaoneni hapa na ninaumia kwelikweli. Nayasema haya kutoka moyoni, lakini nachowaombeni ndugu zangu, mnipe muda wa kwenda kushughulikia tatizo hili kuanzia sasa ili tuweze kupata ufumbuzi.


"Siwezi kuwaambia mtalipwa fidia lini kwa sababu fedha zinapitia mikononi mwa watu wengi, hivyo ni lazima wakae na kupanga."

SASA HUYU MZEE TSERE WANAKWENDA KUMPA KAZI GANI TENA??? Nakumbuka aliwahi kushindwa kinyang'anyiro cha ubunge somewhere. Huyu hawezi kazi jamani!
 
Babati imepata bahati ya DC mwenye Dk kwa mara ya pili, baada ya Dr. Ramadhani ....... Je huyu Dk Ian J. Langiboli anayetoka Chamwino naye ni wa wa binadamu au ni wa fani gani?
 
Babati imepata bahati ya DC mwenye Dk kwa mara ya pili, baada ya Dr. Ibrahim Msengi. Je huyu Dk Ian J. Langiboli anayetoka Chamwino naye ni wa wa binadamu au ni wa fani gani?
 
wakuu JK naona anaendeleza libeneke lake kama kawaida... wale wasiowajibika ndio wanaendelea kutuzwa na kulindwa zaidi na wale wanaoonekana kusamamia haki ya wananchi wanastaafishwa..
tazama mfano Kanali Peter Madaha aliyekuwa wilaya ya nyamagana mwanza naona amestaafishwa baada ya kuwa imara katika kukemea maamuzi ya kifisadi mkoani mwanza... kumbukeni huyu ndio alisimama kupingana na mkuu wa mkoa pamoja na madiwani katika ule mpango wa kuuza uwanja wa nyamagana kwa kusingizia eti umechoka tunamuuzia mwekezaji ajenge hotel..
Alikuwa anakwaruzana mara kwa mara na mkuu wa mkoa kwa sababu ya kusimamia upande wa wananchi..
Inashangaza kuona kuwa nchini Tanzania kiongozi mzuri ni yule anayetetea mafisadi na sio anayetetea wananchi..

Kuna watu wameuliza ... Betty mkwasa kahamishiwa wilayani Bahi mkoani Dodoma.. hawezi kustaafishwa wakati ndio kwanza ameingia ofisini.
 
JK ni fisadi na ndiyo maana anaendelea kulea mafisadi. Francis Isaac alitimuliwa UVCCM kwa tuhuma za ufisadi, bado kambeba kama alivyo na kumpa Ukuu wa Wilaya, hivi kweli huyu Rais wetu yuko serious na vita ya mafisadi? Anapeleka msg gani kwa mafisadi wengine? Kwamba endelee kufanya ufisadi mkigundulika nitawahamishia sehemu nyingine! Kaazi kweli kweli.

Keil,
Kwani mpaka leo bado unatafuta uzuri wa Kikwete. Kubali kaka huyu ni da Gama basi.

Angalia hata historia yake ya nyuma ktk Wizara alizoshika. Ni wapi alifanya angalau Magufuli moja?

Lipi la kukumbukwa?
 
..................
tazama mfano Kanali Peter Madaha aliyekuwa wilaya ya nyamagana mwanza ..

Nikumbushe yule mkuu aliyetunisha misuri kwa Lowasa kule Mwanza, ni nani vile? kabakizwa kweli maana nahisi bado Lowasa ndiye anaye format HD ya mkuu wa Ikulu.
 
Hivi ni Vichekesho, Mkuu wa Wilaya(MwW) #1 anahamishiwa Wilaya #2, MwW#2 anahamia Wilaya #3, MwW#3 anahamia Wilaya#1 n.k.

Mabadiliko makubwa lakini hakuna sababu hata moja iliyotolewa kwa nini yamefanyika.
  1. Hivi kuhamisha Wakuu wa Wilaya 54 nia yake ni ipi hapa, kuwafundisha Jiographia?
  2. Ni nani anayelipa gharama za haya mabadiliko au gharama sio issue tena Tanzania?
  3. Hivi wapinzani hawana la kusema kabisa katika hili zaidi ya kukodoa tu mimacho, au kwa vile hakuna exchange ya cash (ufisadi)?
  4. Hivi hawa Wakuu wa Wilaya 54 wameboresha kitu gani hasa huko walikotoka kinachowaruhusu kuhamishiwa wilaya nyingine?
Kumuachia Kikwete kuendelea na maamuzi na utendaji mbovu bila kumuweka kiti moto, ni kukubaliana na afanyayo au kukosa vision all together.
 
Babati imepata bahati ya DC mwenye Dk kwa mara ya pili, baada ya Dr. Ibrahim Msengi. Je huyu Dk Ian J. Langiboli anayetoka Chamwino naye ni wa wa binadamu au ni wa fani gani?


Kaka Wambugani ni kweli Dr.Ian Justin Langiboli ni Daktari wa Binadamu kama ilivyo kwa Dr.Ibrahim Msengi,lakini katika mabadiliko haya Dr.Msengi hakuwa DC Babati,aliondolewa Babati kwenda Tanga Mjini July/2006....Aliyekuwa DC wa Babati wakati huu ni Mzee David Holela (amestaafishwa).Kwa pamoja Dr.Langiboli na Dr.Msengi ni wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).
 
Babati imepata bahati ya DC mwenye Dk kwa mara ya pili, baada ya Dr. Ibrahim Msengi. Je huyu Dk Ian J. Langiboli anayetoka Chamwino naye ni wa wa binadamu au ni wa fani gani?

Kaka Wambugani ni kweli Dr.Ian Justin Langiboli ni Daktari wa Binadamu kama ilivyo kwa Dr.Ibrahim Msengi,lakini katika mabadiliko haya Dr.Msengi hakuwa DC Babati,aliondolewa Babati kwenda Tanga Mjini July/2006....Aliyekuwa DC wa Babati wakati huu ni Mzee David Holela (amestaafishwa).Kwa pamoja Dr.Langiboli na Dr.Msengi ni wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).

Wandugu,
Nafikiri issue hapa iwe kuwa huyo mkuu aliisaidiaje wilaya kusonga mbele na isiwe majina na tittles wakati hakuna wanalofanya.

Ukuu wa Wilaya siku hizi imekuwa sehemu ya kupeleka wastaafu au watu wasio na uwezo wa madaraka ya kitaaluma serikalini. Kama akina Beti Mkwasa n.k.
 
Wandugu,
Nafikiri issue hapa iwe kuwa huyo mkuu aliisaidiaje wilaya kusonga mbele na isiwe majina na tittles wakati hakuna wanalofanya.

Ukuu wa Wilaya siku hizi imekuwa sehemu ya kupeleka wastaafu au watu wasio na uwezo wa madaraka ya kitaaluma serikalini. Kama akina Beti Mkwasa n.k.

Huyu Dr Msengi ni kama namfahamu vile. Nimekutana naye kwenye issue za ujenzi wa taifa Tanga mwaka 2007 na nimchapa kazi mzuri tu wandugu. Ila kwa kuwa yuko SISI M lazima awe na kakasoro.
 
Na mimi wakuu naungana tena na some members hapa including my friend FMES kuuliza ulazima wa kuwa na hawa wakuu wa wilaya! Hivi kweli kama si kwa sababu za kisiasa tu bado tunahitaji huu mfumo wa kikoloni?Nauliza tena hivi kweli bado tunahitaji hawa watu? Je kama tunawahitaji ni kwa kazi ipi? Propaganda? Je bado wadanganyika tunahitaki kuendelea kwa kupitia propaganda?
Kwa nini? Kwa nini pesa yetu ndogo tunayokusanya kutoka kwenye vyanzo hafifu ya kodi plus hii kidogo tunayopewa grant tunaichezea kwa vitu visivyoleta maendeleo wakati we are still far behind?
Hata hawa tunaodhani tunawahitaji kutuongoza yaani wakuu wa mikoa kwa nini wasiwe wa kuchaguliwa kama tunavyowachagua wabunge na madiwani? hapa si demokrasia yetu imetekwa nyara?
 
Hivi ni Vichekesho, Mkuu wa Wilaya(MwW) #1 anahamishiwa Wilaya #2, MwW#2 anahamia Wilaya #3, MwW#3 anahamia Wilaya#1 n.k.

Mabadiliko makubwa lakini hakuna sababu hata moja iliyotolewa kwa nini yamefanyika.
  1. Hivi kuhamisha Wakuu wa Wilaya 54 nia yake ni ipi hapa, kuwafundisha Jiographia?
  2. Ni nani anayelipa gharama za haya mabadiliko au gharama sio issue tena Tanzania?
  3. Hivi wapinzani hawana la kusema kabisa katika hili zaidi ya kukodoa tu mimacho, au kwa vile hakuna exchange ya cash (ufisadi)?
  4. Hivi hawa Wakuu wa Wilaya 54 wameboresha kitu gani hasa huko walikotoka kinachowaruhusu kuhamishiwa wilaya nyingine?
Kumuachia Kikwete kuendelea na maamuzi na utendaji mbovu bila kumuweka kiti moto, ni kukubaliana na afanyayo au kukosa vision all together.

Labda hapa ni kuwapa warning kwamba wameshindwa ku deliver hivyo wabadilike. historia inaonyesha kuwa kumhamisha mtu ni moja ya adhabu au shukrani wakati mwingine
mf. wakuu wa walaya za dar, naona wote wametolewa (adhabu) wameshindwa kabisa kuondoa kero mbalimbali za dar. Sasa kuna wengine wanakuja dar hapa (huenda wafanyaji kazi wazuri). kuna wanaostaafu na watakaopangiwa kazi nyingine, wanatakiwa kuwa replaced. let's be optimistic.
 
Wanabidii kama mnakumbuka vizuri mwaka 2007 Raisi wetu aliandaa mafunzo Fulani hivi kwa ajili ya MDC ambao wengine ndio wameachwa nyuma katika mabadiliko ya sasa pamoja na kuingiza sura mpya – hatujapata taarifa zinazoingia akilini ni nini haswa kinachoendelea mpaka hii kutokea ghafla hivi .

WAKUU wa Wilaya wote 113 walipata mafunzo ya siku tano ya maadili na ufanisi katika uongozi yaliyozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete kwenye hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam (Machi 4, 2007) mchana.

Ufunguzi wa mafunzo hayo ulihudhuriwa pia na Wakuu wa Mikoa wote 21 na baadhi ya mawaziri wa serikali ya Jamhuri ya Muungano shabaha ya mafunzo hayo ilikuwa ni kupata uelewa wa kanuni, ustadi na mwenendo unaosaidia kuleta uadilifu katika uongozi na ufanisi wa utendaji katika ngazi zote.

Mafunzo hayo yaliendeshwa na taasisi ya mfunzo iitwayo “Tanzania Global Development Centre” yangesaidia kujenga uwezo wa utendaji wa serikali ya Jamhuri ya Muungano ili kufanikisha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya mwaka 2025 .

Miongoni mwa madhumuni makuu ya mafunzo hayo ni kupata uelewa wa uadilifu katika uongozi na wa wajibu na majukumu yanayohusiana na uadilifu katika uongozi.

Mengine ni kujenga uwezo wa kujielewa na kuwaelewa wengine wakati wa kufanya maamuzi na kujifunza namna ya kufanya maamuzi katika mazingira ya kazi yako.

Madhumuni mengine ni kuhakikisha utoaji huduma wenye ufanisi wa hali ya juu katika utendaji na kutoa mfano wa uongozi kwa wengine ili waweze kuiga.

Miaka imepita sasa hatujapata Habari za jinsi mafunzo hayo yalivyowasaidia Hawa madc zaidi ya vituko vya Bwana Mnali na wengine wenye tabia za ajabu ajabu mitaani , kwanini kama Raisi anataka uwazi na uwajibikaji asingetoa ripoti ya mafanikio ya mafunzo hayo wakati ule mpaka sasa hivi ili aweze kusaidiwa na kushauriwa zaidi ?

Huu ni uwajibikaji kweli ??
 
Back
Top Bottom