Mwanakili90
JF-Expert Member
- Nov 24, 2010
- 1,568
- 246
Hii ni kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari mchana wa leo. Katika maelezo yake, DCI anasema kwamba:
"Kutokana na uchunguzi wa kipolisi ulioshirikisha Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, hakuna ushahidi juu ya hilo".
Alipoulizwa na waandishi wa habari:
Je, Dr. Mwakyembe anasumbuliwa na maradhi gani?
DCI alijibu kwamba:
"Kazi ya Jeshi la Polisi sio kuchunguza maradhi bali kuchunguza tuhuma, na baada ya uchunguzi wake kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Jeshi la Polisi limebaini kwamba tuhuma kwamba Dr. Mwakyembe amelishwa sumu hazina ukweli."
!.Mkuu Pasco,
Mtu akiwekewa sumu hawezi kujua kabla hajaambiwa na wataalam wa tiba. Unaweza kuwekewa sumu na usijue kwamba umewekewa sumu ila utaona unaanza kuugua na vipimo vya hospitali ndio ambavyo vinaweza kuthibitisha kwamba huyu mtu aliwekewa sumu na wanaweza ku-identify hata aina ya sumu aliyowekewa kama wana utaalam wa kutosha na vifaa vinavyoweza kugundua.
Litvinenko-aliwekewa Polonium-210, hakujua mpaka alipoenda hospitali na baadaye kuanza ku-trace alipita wapi na wapi na watu gani aliokutana nao. Kama unakumbuka vyema kwenye hilo sakata sehemu zote ambazo alipita siku hiyo ziliwekwa under investigation na kuzuwia watu wasiende. Sasa Mwakyembe ange-ripoti vipi bila kuwa na uhakika wa kulishwa/kuwekewa sumu?
Zama za Mkapa, Mh. John Pombe Magufuli aliwahi kuwekewa sumu na hakujua sumu hiyo aliipata wapi, alipelekwa haraka sana Ujerumani kwenda kutibiwa na baada ya hapo Mh. Pombe alipewa ulinzi na Jeshi la Polisi, walimpa bila kuomba. Maelezo ya Polisi yalikuwa kwamba mtu akishakumbwa na msukosuko kama huo huwezi kujua mtu aliyemfanyia hayo alikuwa na nia gani. Sikumbuki ulinzi huo ulidumu kwa muda gani.
Kwa kufuatilia mtiririko wa matukio ambayo Mwakyembe aliya-report, la kuhusu ajali kule Iringa na kutaka kuuawa Morogoro, kama jeshi la polisi linafanya kazi inavyotakiwa basi lingeweza kuanza kufuatilia nyendo zake hata bila kutangaza na hiyo ingewapatia jibu.
Tatizo la Jeshi la Polisi, linafanya kazi kwa maslahi ya kundi fulani la watu. Kibaya zaidi ni kwamba kwenye tuhuma za Mwakyembe, polisi na gari la polisi walikuwa ni wahusika/watuhumiwa. Sasa unapokuta kwamba Jeshi la Polisi linatuhumiwa, polisi inapoteza sifa ya kufanya uchunguzi ambao unaweza kutoa majibu sahihi. "Dili" kama hizo za kutumia magari ya polisi na polisi wenyewe kufanya jinai, mara nyingi huwa zina baraka za wakubwa wa Jeshi hilo, refer, case ya Zombe na askari wake.
Kwa hiyo Mwakyembe asingeweza kujua kabla hajaenda India kutibiwa. Muhimu ni kile ulichokisema kwamba as long as Manumba amesema Mwakyembe hajalishwa sumu, basi Mwakyembe akirejea kutoka India aje aseme kwamba report ya madaktari inasema nini.
. Ndugu yangu Gwalihenzi, asante kwa koreksheni, mimi ni product ya UPE!Pasco, sasa hicho ndio kiingereza gani? Ingependeza kama ungeweka hivi 'the disclosure rights lie with the patient'
Hii ni kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari mchana wa leo. Katika maelezo yake, DCI anasema kwamba:
"Kutokana na uchunguzi wa kipolisi ulioshirikisha Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, hakuna ushahidi juu ya hilo".
Alipoulizwa na waandishi wa habari:
Je, Dr. Mwakyembe anasumbuliwa na maradhi gani?
DCI alijibu kwamba:
"Kazi ya Jeshi la Polisi sio kuchunguza maradhi bali kuchunguza tuhuma, na baada ya uchunguzi wake kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Jeshi la Polisi limebaini kwamba tuhuma kwamba Dr. Mwakyembe amelishwa sumu hazina ukweli."
dci au dice?
Hahaha, huyu mwalimu wa Pasco ni mnafiki sana:-
1. Alipika report na kujifanya kuwa ameisoma nusu bungeni na nusu ni siri ya kamati, kumbe kamba tupu
2. Alidai kuwa once akirudi kutoka India ataweka mambo hadharani lakini kaja kakaa kimya, huyu ni mnafiki hatari...
`sasa nadhani watanzania wote tuko kwenye page moja, safi sana Manumba na Wizara ya Afya....hahahhaha....
Serikali makini itamshughulikia Sitta haraka iwezekanavyo, scrap him his ninisterial positions na kumpandisha kizimbani kwa kosa la "uchochezi"!.
Mkuu Nguruvi3 kwenye hili la sumu, mwisho wa uwezo wa serikali kusema sio sumu ndio hapo. Serikali haipaswi kusema ilichunguza nini na ni kwa vigezo gani waliend up kuhitimisha sio sumu, japo pia nina doubt na uwezo wa kiteknolojia kufanya uchunguzi wa sumu kama polonium!.
Ile hoja kuwa alishalalamika huko nyuma bali polisi hawakufanya chochote its still valid, polisi walipaswa wauambie umma wa Watanzania why ili wengi wenu msio mwelewe vizuri Mwakyembe what he is really is!.
Tuhuma za Mwakiyembe kutishiwa kuuwawa,sasa hizi tuhuma za sumu si angalau wamejibu!, si wangeweza kukaa kimya na wasiulizwe chochote kama kawaida yao!.
Mkuu Pasco, kwa kusema serikali itamshughulikia Sitta huoni hapo tayari umeshakua upande! (Quote 1). Na kwanini imshughulikie Sitta kwa uchochezi na si Dr Mwakyembe kwa madai 'fake'(Quote yako 2). Halafu unasema waandishi wa Tanzania si wachokonozi, sasa mkuu kwa jinsi ulivyofikia conclusion ya uchochezi wa Sitta na 'fake' ya mauaji ya Mwakyembe huoni una ji-limit kuchokonoa kama waandishi wa Tanzania?Kuusema ukweli sisi waandishi wa Tanzania ni wavivu na sio wachokonozi!. Waandishi wanaoripoti issues za polisi, kazi yao ni kumeza tuu kila wanacholishwakwenye zile daily press co. zao badala kuuliza serious issues.
Pasco, sasa hicho ndio kiingereza gani? Ingependeza kama ungeweka hivi 'the disclosure rights lie with the patient'
Pasco, nadhani huko serious. Unafanya mzaha nadhani, unadhani ingekuwa rahisi hivyo hata yeye mwenyewe angesema sema ovyo? Tafadhali Mkuu ila tuombeane uzima tu. Bahari imechafuka, tsunami iko njiani.Haya Bwana naona unajitahidi kweli.