DC Polepole aenda Supermarket na Kundi la Polisi

DC Polepole aenda Supermarket na Kundi la Polisi

Waungwana,
Niko hapa Musoma, nilishangazwa sana na kitendo cha Mkuu wa Wilaya ya Musoma Ndg. Humphrey Polepole kwenda kufanya manunuzi katika duka la Alpha Choice akiwa na kundi kubwa la maafisa wa polisi.

Ndugu DC tunakukaribisha Musoma na kukutaarifu kuwa Mkoa wa Mara una amani, hakuna ulazima wa wewe kutembea na mapolisi hata unapoenda sehemu kama hizo...

Ondokana na ile old fashioned paranoia ya kutembea na mapolisi wakati wananchi wanawahitaji hao mapolisi wawalinde mtaani...

Muunge Mkono Rais kwa kubana matumizi kwani kuwa na misafara kwenda shoping ni gharama kubwa kwetu walipa kodi...

Itetendee haki spirit uliyokuwa nayo wakati wa mchakato wa katiba...
Polepole ni Limbukeni mkubwa anataka waandishi waandike andike juu yake lakini kasahau kuwa aliyemteua anataka kubana matumizi si kumaliza mafuta na misafara isiyo na Tija .
 
Kumbe tayari kesharepoti Musoma? Njaa mbaya sana nilidhani bado anatafakari na kujipima kwanza!
 
Pole pole masifa tu, mfano mkuu wa mkoa wa mwanZa kila siku namuona pale U turn supermarket ni yeye na dereva wake tu basi hakuna cha polisi wala nini!
 
Mwambieni mkurya haogopi polisi, mwanamama tu alimnyang'anya jambazi bunduki. Kijana analipangua kombora kwa rungu.

Hata hivyo kuamini habari zako tuwekee picha inaweza kuwa rongo yako.

Mkuu inawezekana hapakuwa na mazingira ya kupiga picha ,Ila tunajua hawa watu wanao ulinzi na kazi zao unazifahamu ....
 
Kama taarifa hii inaweza kuwa na chembe ya ukweli basi ukweli huo ni kwamba ni kweli Polepole ndiye Mkuu wa hiyo wilaya na labda ni kweli alienda kufanya shopping supermarket.
Sidhani kama kuna ukweli wowote kuhusiana na hilo lundo la askari katika shughuli yake hiyo.
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Kama taarifa hii inaweza kuwa na chembe ya ukweli basi ukweli huo ni kwamba ni kweli Polepole ndiye Mkuu wa hiyo wilaya na labda ni kweli alienda kufanya shopping supermarket.
Sidhani kama kuna ukweli wowote kuhusiana na hilo lundo la askari katika shughuli yake hiyo.
Polepole ni Limbukeni sishangai kusikia kufanya chochote .
 
Aliutafuta ufalme kwa nguvu kubwa ikiwa ni pamoja na kukosa nidhamu kwa kukashifu binadamu wenzake kwenye vyombo vya habari, kafanikiwa kawa mfalme anataka kuonja ladha ya ubwanyenye.
 
Back
Top Bottom