DC Muro Matatani kwa kushusha Bendera za CHADEMA Arumeru

DC Muro Matatani kwa kushusha Bendera za CHADEMA Arumeru

Falme zilikuja zikapita, watu maarufu pia wamepita, kila Jambo unalofanya, sukumwa na hisia za ndani sio kumpendeza mtu kikundi Cha watu. Let's respect each other. Bwana ibariki Tanzania
 
hawa wakuu Wa wilaya vijana wanatuangusha sisi vijana wenzao sana. kwa kufanya kazi ni kwa kuvunja sheria tu. inasikitisha sana...
 
Hiyo ni dalili kwamba kaletwa hapo kupambana na cdm na sio kutumikia wananchi. Huyo ndio kwenye uchaguzi atakuwa anaagiza zoezi la kura liendeshweje. Halafu CDF atakaa kimya kwa hilo.

Wakuu zangu, kama habari hiyo ni ya kweli...

Hapana, sipendi kuamini kuwa tumefika huko..., lakini kama ni kweli na kuna watu wanashangilia ...!

Kila nikiijaribu kuliwaza tendo kama hilo, katika nchi yetu hii nzuri...! Hivi kweli inawezekana? Hivi kweli ndio tumefika huko?

Naona nazungukazunguka tu kwa kukosa maneno ya kujieleza nilivyostushwa na habari hii! Huenda ni mimi ndio sijaelewa vizuri yaliyoelezwa na mleta mada, maana naona mjadala unajiendea tu kama ni jambo la kawaida tu lisilokuwa na maana yoyote.

Mkuu wa Wilaya... anakuja hadi nyumbani kwa mtu ambaye hajavunja sheria yoyote na kuamuru? Yule Mhehe Mwamwindi sikupenda aliyofanya wakati ule... Inaumiza sana.

Nitaendelea kusoma tu yanayojadiliwa.
 
Huyu naye naona anahitaji afungiwe speed gavana. Ameanza kuvuta bangi.

Siku zote watu wamekuwa wakipeperusha bendera za vyama vyao. Akiendelea hivi atakuja na YOYOTE ANAYEBEBA CARD ZA CHAMA CHA UPINZANI HATAPATA HUDUMA ARUMERU.

Tupinge tabia hii sote kama watanzania bila ya kujali itikadi zetu.

Uhuru wa kuwa mwanachama wa chama chochote ni haki ya kila mtanzania bila kuingiliwa na kulazimishwa.
 
hivi anadhani magufuli atatawala milele? kuna watu baada ya magufuli kuondoka kuna watu watapata tabu sana kama si kusaga meno
 
hivi anadhani magufuli atatawala milele? kuna watu baada ya magufuli kuondoka kuna watu watapata tabu sana kama si kusaga meno

Huwa nawasikitikia sana watalia kilio cha mbwa koko,wengi wao ni Vijana ni lzm wataijibu historia japo sasa wamenyimwa ufahamu.
 
Hizi ni zile teuzi zilizopatikana kama fadhila baada ya kutukana upinzani ulitegemea nn hao wapo kwa maslai ya anaewalipa na si wananchi
 
Huyo chama kimburuze mahakamani hawana semina elekezi hao hawajui hata mipaka yao.
 
Yule Msajili yuko wapi aandike barua kama alivyoiandikia ACT?,huyu mshamba(kwa sauti ya Zitto) anafanya haya yote hajui hii ni nchi ya vyama vingi?hajui Chattle nzima ni Oposition na wenye mji wao wanapata usingizi?
 
Bado hajawajua wameru vzr. Akawaulize wachungaji wa kilutheri kuhusu mgogoro ule wa makanisa ulisababishwa na nn. Nchi ya vyama vingi lazima kiongozi uheshimu itikadi za watu
 
Wakuu zangu, kama habari hiyo ni ya kweli...Hapana, sipendi kuamini kuwa tumefika huko...,
Mkuu Kalamu1, habari hii ni ya kweli...Hapana, sipendi kuamini kwamba hatujafika huko...

lakini kama ni kweli na kuna watu wanashangilia ...!
Ni kweli na kuna watu wanashangilia...!

Kila nikiijaribu kuliwaza tendo kama hilo, katika nchi yetu hii nzuri...! Hivi kweli inawezekana?
Naam, usiwaze sana tendo kama hilo, katika nchi yetu hii ya leo...inawezekana sana tu.

Hivi kweli ndio tumefika huko?...
Si tu tumefika huko, tumevuka huko na tunazidi kusonga mbele.

Mkuu Kalamu1, kuna Mbunge, mwakilishi aliyepigiwa kura na wananchi, aliwahi kumiminiwa risasi risasi zaidi ya 30 na kati ya hizo 16 zikatua mwilini. Kitendo hicho kilifanyika mchana kweupe akitoka bungeni an akiwa anarejea nyumbani kwake sehemu yenye ulinzi na ambapo wanakaa watumishi wakuu wa serikali. Wakati Wasamaria wema wakimsaidia asikate roho, si Bunge wala Serikali ilikuwa tayari kugharamia matibabu yake lakini kwa neema ya Mwenyezi Mungu, aliweza kunusurika na kifo na hadi leo hii yuko mzima akiendelea na matibabu kwa msaada wa ndugu, marafiki na Wasamaria wema.

Naam, katika hii nchi yetu unayoiita nzuri, tendo la ukatili kama huo liliwezekana na washangiliaji walikuwepo na wanaendelea kuwepo. Nashangaa tu kwamba umeshtushwa na kushushwa kwa bendera, sijui ulizungumziaje hili! Sijui unaongeleaje kupotea kwa wananchi na miili yao kuokotwa kando ya bahari. Sijui unaongeleaje kuhusu kutekwa, kuteswa na wakati mwingine kuuliwa kwa Watanzania kwa sababu tu ya kuwa na msimamo tofauti kiitikadi. Najua wapo wanaoshangilia! Naam, tumefikia huko...na bado! Yapo makubwa zaidi yanatusubiri huko mbele ya safari...kumbuka aliyeonja nyama ya binadamu haachi!
 
Back
Top Bottom