Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 749
- 1,797
Mkuu wa wilaya ya Arumeru ,Jerry Muro huenda akaingia kwenye msuguano mkali na chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wilayani humo kwa hatua yake ya kushusha bendera zake pindi anapokuta zikipepea kwenye maeneo ya biashara zilizosimikwa na wapenzi wa chama hicho.
Mapema leo Muro wakati alitoka kuangalia majeruhi wa ajali katika hospital ya Selian ,Ngaramtoni,alifika katika Duka moja la mfanyabiashara wa Makochi na alipoiona Bendera ya Chadema ikipepea aliamuru Dereva wake asimame na kuifuata bendera hiyo.
Alipofika Muro alimwamuru mfanyabiashara huyo wa Makochi ambaye hakufahamika jina lake Mara moja, aamue moja kufanya biashara ama kuendeleza siasa ,Hata hivyo kabla ya kijana huyo kujibu alimtaka ashushe bendelea hiyo Mara moja.
"Arumeru hii si ile ya zamani msinijaribu lazima tuheshimiane chagua moja kazi ama siasa" Alisema Muro
Jambo hilo liliwashangaza wananchi mbalimbali waliokuwepo eneo hilo huku ikielezwa kuwa linaweza kuleta mtafaruku wa kisiasa kwa hatua yake ya kushusha bendera za Chadema huku za CCM zilizopo vijiweni kwenye biashara akiziacha ziendelee kupepea.