DC Mrisho Gambo apandishwa kizimbani

DC Mrisho Gambo apandishwa kizimbani

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wilaya ya Korogwe leo (jana) imemkataa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kumwakilisha Mkuu wa wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo katika kesi ya madai ya sh.Milioni 96 dhidi yake.

Katika kesi hiyo Na. 7/ 2012 mlalamikaji ni Mwanasheria wa halmashauri ya Mji Korogwe, Najum Tekka anayedai kukashifiwa na Gambo wakati wa kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya kwamba stashahada ya Sheria aliyopata mtumishi huyo niya chupi.

Awali ilidaiwa kwamba mkuu huyo alimwalika mlalamikaji kutoa ushauri wa kisheria kuhusu namna ya kumaliza mgogoro baina ya halmashauri ya mji na wafanyabiashara na kwamba baada ya kufanya hivyo mlalamikiwa alipinga ushauri uliotolewa na kIsha kutoa kauli hiyo kwamba shahada yake ni ya chupi.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Hamis Salum mlalamikaji huyo aliiomba mahakama imwondoe mwanasheria mkuu wa serikali ambaye aliwakilishwa mahakamani hapo na Wakili wa Serikali, Rebecca Msalangi kwakuwa hana mamlaka katika madai hayo na kamwe ofisi yake haikuwahi kupeleka ombi maalum la kutaka kumwakilisha Gambo kwenye shauri hilo.

Kwa upande wake Hakimu Mkazi akisoma uamuzi mdogo wa mahakama kuhusiana na mabishano hayo alikiri kwamba utaratibu haukufutwa na kamwe hapakuwa na ombi la mwanasheria mkuu wa serikali kutaka kumwakilisha Gambo kwenye madai hayo.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 14 mwaka


Source: Wavuti





 
Ndo matatizo ya kuwapa madaraka vijana ambao hata hawajamaliza balehe, kisa unataka kumkomoa Laigwanan. Ona sasa aibu yake mkuu wa wilaya ndio aibu ya aliyemteua na ndio aibu ya swahiba wa mteuliwa bw Riziwan
 
Laigwanan anatisha, hvi unajua sasa hivi ukisema Laigwanan = CCM.
 
sasa ndio tutaona kati Mrisho Gambo na Na NajjumTekka nani mwenye degree ya :ballchain:chupi😛hoto:
 
Aligombea UBUNGE wa EA akakwanguliwa na Wabunge wa CCM alipata kura MMm kwa kifupi chache zaidi ya William John Malecela... Na bado akabeba CHEO CHA UKUU WA WILAYA; Tangu lini mtu aliyesomea Masomo ya Computer Science awe na Uwezo na HEKIMA ya kuendesha WILAYA bila MATUSI ??? Kubebana wanajua kuna ULAJI sehemu fulani, lazima waungane waubebe wale hizo pesa
KIONGOZI MKUU THE PRINCE...
 
Gambo kafanya shambulio la aibu, bora awajibishwe!
 
Siku zote nimekuwa nasema haya ni matatizo ya JK na CCM kukurupuka kuwapatia vyeo vya utawala vijana bila maandalizi yoyote na kuangalia sifa za mteule husika. Ingekua wakati wa utawala wa Mwl. Nyerere huyo dogo angekwisha vuliwa madaraka zamani. Ni maneno ya hovyo ambayo yanaweza tamkwa na wahuni ktk vijiwe siyo na mtumishi wa umma.
 
Aligombea UBUNGE wa EA akakwanguliwa na Wabunge wa CCM alipata kura MMm kwa kifupi chache zaidi ya William John Malecela... Na bado akabeba CHEO CHA UKUU WA WILAYA; Tangu lini mtu aliyesomea Masomo ya Computer Science awe na Uwezo na HEKIMA ya kuendesha WILAYA bila MATUSI ??? Kubebana wanajua kuna ULAJI sehemu fulani, lazima waungane waubebe wale hizo pesa
KIONGOZI MKUU THE PRINCE...

Tafadhali ndugu hapo kwenye bold tutake radhi. Elimu haitengenezi au kuondoa busara. Bila hao computer scientists hii JF ungeisikia kwenye bomba.

Anyway back to the topic, kila mtu abebe mzigo wake. Kumwambia mwanamke kwamba "Degree yake ni ya chupi", sio tusi tu kwake bali ni udhalishaji wa kijinsia. Cha ajabu watu wako kimya, na bado anatamba ofisini.
 
Natamani sana huyo mama ashinde kesi yake! Ni upuuzi sana kwa dc kumdhalilisha hadharani halafu anataka kutetewa na serikali!
 
Natamani sana huyo mama ashinde kesi yake! Ni upuuzi sana kwa dc kumdhalilisha hadharani halafu anataka kutetewa na serikali!

ndugu yangu mwisho wa kesi, Mrisho Gamba atahukumiwa kwenda jela miezi 6 au kulipa faini ya Tsh 250000.
 
Kwanini awakilishwe na mwanasheria wa serekali in the first place? Kwani hili suala linahusu nini serekali, yeye si alitamka kama Gumbo au ni mawazo ya serekali kuwa dada wa watu ana degree ya Chupi? Nadhani ni mawazo yake binafsi na asimame yeye kama yeye kutokana na matamshi yake.

Napingana na mchangiaji aliesema wenye degree ya IT hawana busara ya kuongoza.
 
ndugu yangu mwisho wa kesi, Mrisho Gamba atahukumiwa kwenda jela miezi 6 au kulipa faini ya Tsh 250000.
hakuna kifungo wala iyo faini hii si kesi ya jinai ni kesi ya madai ..madai yenyewe ni milioni 96 mahakama ikimtia hatiani aidha iongeze au ipunguze lakini haiwezi kapunguza kufikia laki kadhaaaa
 
Itabidi pia aithibitishie mahakama kuwa degree yake si ya chupi. Na Dc itabidi athibitishie mahakama kuwa degree ya mtuhumiwa wake ni ya chupi.
 
Back
Top Bottom