DC Mrisho Gambo apandishwa kizimbani

Huyo Mrisho Gambo sifa zitamponza kama Nape.Hiyo jeuri ya kuwa mtandao mmoja na Riz1 na wenzake unakuwa na dharau,ulipe sasa gharama ya dharau zako,kesi usimame mwenyewe hakuna cha wakili wa serikali maana umeshitakiwa wewe kama wewe.naona utapata adabu na heshima kwa wafanyakazi weledi.
 
Nina imani kabisa wapo wenye uwezo mzuri kabisa walioachwa na hatimae kichukuliwa watu wasio na uwezo kwa ajili tuu ya urafiki.Dc ni mwakilishi wa rais hivyo amemdhalilisha rais, kimsingi angetakiwa kujiuzulu.
 
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wilaya ya Korogwe leo (jana) imemkataa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kumwakilisha Mkuu wa wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo katika kesi ya madai ya sh.Milioni 96 dhidi yake.

Katika kesi hiyo Na. 7/ 2012 mlalamikaji ni Mwanasheria wa halmashauri ya Mji Korogwe, Najum Tekka anayedai kukashifiwa na Gambo wakati wa kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya kwamba stashahada ya Sheria aliyopata mtumishi huyo niya chupi.

Awali ilidaiwa kwamba mkuu huyo alimwalika mlalamikaji kutoa ushauri wa kisheria kuhusu namna ya kumaliza mgogoro baina ya halmashauri ya mji na wafanyabiashara na kwamba baada ya kufanya hivyo mlalamikiwa alipinga ushauri uliotolewa na kIsha kutoa kauli hiyo kwamba shahada yake ni ya chupi.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Hamis Salum mlalamikaji huyo aliiomba mahakama imwondoe mwanasheria mkuu wa serikali ambaye aliwakilishwa mahakamani hapo na Wakili wa Serikali, Rebecca Msalangi kwakuwa hana mamlaka katika madai hayo na kamwe ofisi yake haikuwahi kupeleka ombi maalum la kutaka kumwakilisha Gambo kwenye shauri hilo.

Kwa upande wake Hakimu Mkazi akisoma uamuzi mdogo wa mahakama kuhusiana na mabishano hayo alikiri kwamba utaratibu haukufutwa na kamwe hapakuwa na ombi la mwanasheria mkuu wa serikali kutaka kumwakilisha Gambo kwenye madai hayo. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 14 mwaka

Source: Wavuti
Huyu kumbe tangu mwaka 2012 alikuwa mkuu wa wilaya enzi za JK halafu akapandishwa cheo kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha naonesha kejeli kwa JPM?

Hana maadili ya kiuongozi kwa kitendo tu cha kufikishwa mahakamani akishitakiwa kumkashifu afisa mwingine wa serikali.

HAFAI Arusha mmesikia hiyo? Msirudie makosa mrejesheni Lema haraka kwa sasa mna msaka tonge mdomoni hakuna mwakilishi wa ukweli hapo
 
Huyu kumbe tangu mwaka 2012 alikuwa mkuu wa wilaya enzi za JK halafu akapandishwa cheo kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha naonesha kejeli kwa JPM?

Hana maadili ya kiuongozi kwa kitendo tu cha kufikishwa mahakamani akishitakiwa kumkashifu afisa mwingine wa serikali.

HAFAI Arusha mmesikia hiyo? Msirudie makosa mrejesheni Lema haraka kwa sasa mna msaka tonge mdomoni hakuna mwakilishi wa ukweli hapo

Sasa kwenye kile kipengele cha mgombea asiwe na historia ya uhalifu au kuwahi shtakiwa kwa jinai mahakamani. Yeye alikwepaje?
 
Back
Top Bottom