Danny Jully
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 4,416
- 3,860
Hakuna ugumu wowote. Rais ni taasisi siyo mtu mmoja.Na ni vigumu sana kwa Rais kuwajua 'vizuri' watu anaowateua..
Hakuna ugumu wowote. Rais ni taasisi siyo mtu mmoja.Na ni vigumu sana kwa Rais kuwajua 'vizuri' watu anaowateua..
Yaani ndani ya saa24 amesha misbehave? Kabla hata ya kuapishwa?Mbona hii ni kawaida na ilikuwa inatokea sana enzi ya Nyerere. Mtu unapata taarifa kuwa umeteuliwa cheo fulani, unaitisha party ya kusheherekea na kuropoka maneno ya ajabu ajabu. Mara eti 'Oh nimeukata, umasikini sasa bye bye, mademu sasa watanikoma nk'. TISS huanza kufuatilia mwendo na tabia ya mteuliwa kwa karibi sana mara tu baada ya uteuzi na uki misbehave wanatoa taarifa mteuaji ambaye atatengua mara moja.
Nadhani hiki ndicho alichokipata mteuliwa huyu.
Mungu mkubwa....kaamuà kumfundisha kwamba binadamu si kamili asilimia mia,Mkubwa hakosei....
Akikosea ujue kateleza tu kwa bahati mbaya.
..uzi wangu naona umefutwa.
..ngoja nimtonye bosi labda atawatumbua hawa moderators.
BAK, Mag3, Richard, Maxence Melo
Usishangae JokaKuu, hata mimi nimekuwa nikianzisha thread Jukwaa la Siasa lakini hazitokei na sasa nimeamua kuchangia tu za watu wengine. JF nadhani imeingiliwa na kwa sasa michango iliyojaa utadhani imeandikwa na watoto wa Chekechea na hasa ile inayomsifu Magufuli na serikali yake. JF si tena forum where we dare, imekuwa kama jamvi la Lumumba sycophants!..uzi wangu naona umefutwa.
..ngoja nimtonye bosi labda atawatumbua hawa moderators.
BAK, Mag3, Richard, Maxence Melo
Labda ule mtambo wa kichina wa kutimiza ndoto ya mkulu umeanza kazi, si unakumbuka alisema anaomba malaika wa kufunga mitambo ashuke!! JF maudhi tu sasaUsishangae JokaKuu, hata mimi nimekuwa nikianzisha thread Jukwaa la Siasa lakini hazitokei na sasa nimeamua kuchangia tu za watu wengine. JF nadhani imeingiliwa na kwa sasa michango iliyojaa utadhani imeandikwa na watoto wa Chekechea na hasa ile inayomsifu Magufuli na serikali yake. JF si tena forum where we dare, imekuwa kama jamvi la Lumumba sycophants!
MmmhDC mpya wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida Mwl. Fikiri Avias Saidi uteuzi wake umetenguliwa leo, ameteuliwa ndugu Miraji Mtaturu ambae alikuwa katibu wa CCM mkoani Mwanza.
Ngoma inogile.
=========
Juni 26 mwaka huu Rais John Pombe Magufuli alitangaza kuteua Wakuu wa Wilaya zote nchini, na Wakuu wa Mkoa watatu. Kati ya Wakuu wa Wilaya 139 walioteuliwa, 39 wamebakishwa katika nafasi zao huku 100 wakiwa ni wapya.
Katika hali ya kushangaza siku moja baada ya orodha hiyo kutangazwa, Rais Magufuli ametengua uteuzi wa mkuu wa wilaya ya Ikungi iliyopo mkoani Singida. Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Bwana Fikiri Avias Said ndani ya masaa 24 tangu uteuzi wake.
Sababu kuu ya Rais kutengua Uteuzi huu ameisema leo hii wakati wa hafla ya kuwaapisha Wakuu wote walioteuliwa, ni kwamba jina lilikosewa, na kusema kwamba Mkuu wa Wilaya halali wa Ikungi ni Bwana Miraji Mtaturu ambaye ni Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mwanza,