DC Iramba awazawadia walimu Shule ya Sekondari Lulumba safari ya kwenda mbuga wanayotaka nchini

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe. Suleiman Yusuph Mwenda ametoa zawadi kwa walimu wa shule ya Sekondari Lulumba kuchagua mbuga yoyote ya wanyama kwenda kupumzika kwa siku 3 baada ya shule hiyo kufanya vizuri sana kwenye matokeo ya kidato cha 6 na kuongoza Kiwilaya na Kimkoa na kushika nafasi ya 24 Kitaifa kati ya shule 610.

Mhe. Mwenda ameyasema hayo Julai 30, 2021 wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu na viongozi mbalimbali wa shule ya Sekondari Lulumba iliyoandaliwa na uongozi wa shule ya Sekondari Lulumba kwa lengo la kuwapongeza walimu waliofanya vizuri kwenye masomo yao na kuiwezesha Lulumba Sekondari kushika nafasi ya kwanza Kiwilaya na Kimkoa na nafasi ya 24 Kitaifa kwenye matokeo ya kidato cha sita mwaka huu. Akisoma historia fupi ya shule mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Mhe. Suleiman Yusuph Mwenda, Mkuu wa shule ya Sekondari Lulumba Mwalimu Kitiku amesema siri pekee ya mafanikio hayo ni kufanya kazi kwa ushirikiano.

Akitoa taarifa fupi ya historia ya shule Mkuu wa shule Mwalimu Kitiku amesema shule ya Lulumba ilianza Mwezi Machi 1990 chini ya usimamizi wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya wakati huo Kapteni John Chiligati. Kwa sasa shule ina wanafunzi 971 kidato cha kwanza hadi kidato cha sita, wasichana 370 na wavulana 601 kwa jumla ya mikondo 15. Pia shule ina walimu 35 kati ya hao walimu 3 wa muda, walimu wa kiume 21 na walimu wa kike 14, shule ina watumishi wasio walimu 9.

Kuhusu hali ya ufaulu, kidato cha nne kwa miaka mitatu mfululizo toka mwaka 2018 walifaulu wanafunzi 97 sawa na 95.9%, 2019 walifaulu wanafunzi 98 sawa na 100% na mwaka jana 2020 walifaulu wanafunzi 94 sawa na 98.9%.

Kwa upande wa kidato cha sita matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:
2018/2019 walifaulu wanafunzi 71 Sasa na 100%, 2019/20 walifaulu wanafunzi 151 sawa na asilimia 100%, 2020/21 walifaulu wanafunzi 130 sawa na asilimia 100% ambapo daraja la 1-96, daraja la 2-32, daraja la 3-3.

Kwa upande wa changamoto zinazoikabili shule, akitoa taarifa kwa mgeni rasmi, Mkuu wa shule Mwalimu Benjamin Kitiku alisema shule ina uhaba wa naji na maji wanaotumia kutoka idara ya maji yana mgao kwa wiki yanatoka mara 2 tu, uhaba wa vyumba vya madarasa, ukosefu wa gari la shule, uhaba wa nyumba za walimu na samani za ofisini.

Mkuu wa shule alimuhakikishia Mkuu wa Wilaya Mhe. Mwenda kuwa mikakati waliyo nayo ni kuhakikisha wanafanya maandalizi ya kutosha na wana uhakika matokeo yajayo ya kidato cha sita wataingia kwenye kumi bora kitaifa.

Mkuu wa Wilaya, Mhe. Mwenda aliwapongeza walimu kwa kujitoa na kufundisha kwa bidii huku akiwahakikishia walimu atahakikisha anakuwa mstari wa mbele kuhakikisha anasimamia suala la elimu na amewaambia walimu wote wilaya ya Iramba kwa mwenye shida au changamoto basi ofisi yake ipo wazi anawakaribisha na kama anatoka maeneo ya mbali anaweza kupiga simu na atatatua changamoto inayomkabili. "Mimi ni mwalimu na nawapenda walimu wenzangu kwani mara baada ya kumaliza masomo yangu ya elimu ya juu nimefanya kazi ya ualimu kwa kujitolea kufundisha" alisema Mhe. Mwenda

Kuhusu changamoto za shule Mhe. Mwenda alimuagiza Mkurugenzi kwa kusema "*angalia namna utakavyoweka kwenye mipango ya Halmashauri kuhakikisha unayatatua matatizo ya Lulumba sekondari".

#KaziinaendeleaIramba

2865946_IMG-20210801-WA0016.jpg
 
Mkuu wa wilaya amepata wapi fungu lakuwagharamia walimu kwa siku 3.

Walimu wana makazi mazuri yakuishi?

Mkuu wa wilaya ungewapeleka vyuoni kwa malipo yako ili waongeze weredi.
 
Na wanafunzi ambao kimsingi ndo wamefaulu vizuri na kuiweka shule nafasi hiyo nao wamezawadiwa nini?
 
MHE MWENDA AWAZAWADIA WALIMU SAFARI YA KWENDA MBUGA YOYOTE YA WANYAMA WANAYOTAKA NCHINI.

MKUU WA WILAYA YA IRAMBA, MHE.SULEIMAN YUSUPH MWENDA

Na Mwandishi wetu.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe. Suleiman Yusuph Mwenda ametoa zawadi kwa walimu wa shule ya Sekondari Lulumba kuchagua mbuga yoyote ya wanyama kwenda kupumzika kwa siku 3 baada ya shule hiyo kufanya vizuri sana kwenye matokeo ya kidato cha 6 na kuongoza Kiwilaya na Kimkoa na kushika nafasi ya 24 Kitaifa kati ya shule 610.

Mhe. Mwenda ameyasema hayo Julai 30, 2021 wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu na viongozi mbalimbali wa shule ya Sekondari Lulumba iliyoandaliwa na uongozi wa shule ya Sekondari Lulumba kwa lengo la kuwapongeza walimu waliofanya vizuri kwenye masomo yao na kuiwezesha Lulumba Sekondari kushika nafasi ya kwanza Kiwilaya na Kimkoa na nafasi ya 24 Kitaifa kwenye matokeo ya kidato cha sita mwaka huu. Akisoma historia fupi ya shule mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Mhe. Suleiman Yusuph Mwenda, Mkuu wa shule ya Sekondari Lulumba Mwalimu Kitiku amesema siri pekee ya mafanikio hayo ni kufanya kazi kwa ushirikiano.

Akitoa taarifa fupi ya historia ya shule Mkuu wa shule Mwalimu Kitiku amesema shule ya Lulumba ilianza Mwezi Machi 1990 chini ya usimamizi wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya wakati huo Kapteni John Chiligati. Kwa sasa shule ina wanafunzi 971 kidato cha kwanza hadi kidato cha sita, wasichana 370 na wavulana 601 kwa jumla ya mikondo 15. Pia shule ina walimu 35 kati ya hao walimu 3 wa muda, walimu wa kiume 21 na walimu wa kike 14, shule ina watumishi wasio walimu 9.

Kuhusu hali ya ufaulu, kidato cha nne kwa miaka mitatu mfululizo toka mwaka 2018 walifaulu wanafunzi 97 sawa na 95.9%, 2019 walifaulu wanafunzi 98 sawa na 100% na mwaka jana 2020 walifaulu wanafunzi 94 sawa na 98.9%.

Kwa upande wa kidato cha sita matokeo yalikuwa kama ifuatavyo
2018/2019 walifaulu wanafunzi 71 Sasa na 100%, 2019/20 walifaulu wanafunzi 151 sawa na asilimia 100%, 2020/21 walifaulu wanafunzi 130 sawa na asilimia 100% ambapo daraja la 1-96, daraja la 2-32, daraja la 3-3.

Kwa upande wa changamoto zinazoikabili shule, akitoa taarifa kwa mgeni rasmi, Mkuu wa shule Mwalimu Benjamin Kitiku alisema shule ina uhaba wa naji na maji wanaotumia kutoka idara ya maji yana mgao kwa wiki yanatoka mara 2 tu, uhaba wa vyumba vya madarasa, ukosefu wa gari la shule, uhaba wa nyumba za walimu na samani za ofisini.

Mkuu wa shule alimuhakikishia Mkuu wa Wilaya Mhe. Mwenda kuwa mikakati waliyo nayo ni kuhakikisha wanafanya maandalizi ya kutosha na wana uhakika matokeo yajayo ya kidato cha sita wataingia kwenye kumi bora kitaifa.

Mkuu wa Wilaya, Mhe. Mwenda aliwapongeza walimu kwa kujitoa na kufundisha kwa bidii huku akiwahakikishia walimu atahakikisha anakuwa mstari wa mbele kuhakikisha anasimamia suala la elimu na amewaambia walimu wote wilaya ya Iramba kwa mwenye shida au changamoto basi ofisi yake ipo wazi anawakaribisha na kama anatoka maeneo ya mbali anaweza kupiga simu na atatatua changamoto inayomkabili. "Mimi ni mwalimu na nawapenda walimu wenzangu kwani mara baada ya kumaliza masomo yangu ya elimu ya juu nimefanya kazi ya ualimu kwa kujitolea kufundisha" alisema Mhe. Mwenda

Kuhusu changamoto za shule Mhe. Mwenda alimuagiza Mkurugenzi kwa kusema "angalia namna utakavyoweka kwenye mipango ya Halmashauri kuhakikisha unayatatua matatizo ya Lulumba sekondari".

#KaziinaendeleaIramba

IMG-20210801-WA0011.jpg

IMG-20210801-WA0012.jpg

IMG-20210801-WA0013.jpg

IMG-20210801-WA0014.jpg

IMG-20210801-WA0016.jpg
 
Jambo jema, walimu hudharaulika hata kufedheheshwa sana, hii ni njia moja wapo ya kuwatia moyo na kutambua mchango wao. By the way DC asisahau kuboresha mazingira yao ya kazi, mazingira ya upatikanaji wa huduma za kijamii kama maji, umeme, afya nk ili kuwapunguzia frastration
 
Mkuu wa wilaya amepata wapi fungu lakuwagharamia walimu kwa siku 3.

Walimu wana makazi mazuri yakuishi?

Mkuu wa wilaya ungewapeleka vyuoni kwa malipo yako ili waongeze weredi.
Unampangia zawadi? Angewapeleka vyuo vile vile ungelalamika, alafu unajua mlolongo mzima na gharama za kusoma. Na wakisoma wote shule ibaki na nani?
 
Na wanafunzi ambao kimsingi ndo wamefaulu vizuri na kuiweka shule nafasi hiyo nao wamezawadiwa nini?
Wanabadilishiwa ratiba ya chakula, siku ya kula kende wanapikiwa wali maharage
 
Back
Top Bottom