DC Godwin Gondwe awaomba radhi waandishi wa habari kufuatia DED wa Temeke kumkemea Richard wa ITV

Mkuu wa wilaya ya Temeke mh Godwin Gondwe amesimamisha ujenzi wa shule ya Lumo hadi pale kesi iliyopo mahakamani itakapotolewa maamuzi.
Kiwanja cha shule hiyo kina mgogoro kati ya wananchi wa eneo hilo na manispaa ya Temeke.

Kadhalika mh Godwin Gondwe amewaomba radhi waandishi wa habari kote nchini kufuatia kitendo cha mkurugenzi wa manispaa ya Temeke kumkashifu mwandishi wa habari chipukizi wa ITV Richard Stephen kwamba hana hadhi ya kuongea naye na kwamba yeye hadhi yake ni mkurugenzi wa ITV Joyce Mhaville.

Source ITV.

cc: Erythrocyte, Gentamycine

Maendeleo hayana vyama!
Huyo DED Mwakibibi amekuwa mtoto mpaka aombewe radhi...hii si radhi..
Kama kweli anamaanisha aombe yeye mwenyewe .
....kwa kifupi waandishi mnadharaulika sana poleni.
 
Kongole kwake mh.Gondwe....

Wewe tunaufahamu UZALENDO HEKIMA BUSARA NA HESHIMA ZAKO....

Hakika huo ndio USTAARABU kwani taifa letu hili haliwezi kurudi nyuma kwa baadhi ya watu KUTOLEWA LUGHA ZA KASHFA NA ZILIZOKOSA UTU NA HESHIMA....

CCM imelijenga taifa hili ndani ya imani kuu 3:
1.Binadamu wote ni sawa
2.Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.
3.Ujamaa na kujitegemea ndio njia sahihi ya KUJENGA JAMII iliyo sawa na huru.

Kudos mh.Double G

MAENDELEO HAYANA VYAMA
 
Serikali SIKIVU ya AWAMU ya 5 ina wenye weledi wa uongozi Kama akina DC GONDWE wengi tu....

Serikali ya CCM inaziishi imani kuu hizi;

1.Binadamu wote ni sawa.
2.Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa UTU WAKE...

Kudos
 
Back
Top Bottom