DC Bukoba aamuru walimu wachapwe mboko!

Mwiba, tusipende kila wakati kulaumu tu, hata pale tunapoona kuna ukweli. Hutakiwi unaposikia jambo mara moja unamchukulia mtu hatua, kwanza ni vizuri kupata ukweli. Yaweza kweli kuwa siku zimepita tangu tukio litokee, lakini nadhani kuna mambo yalikuwa yanafuatiliwa kwanza.

Unaposema Mkuu wa Mkoa alichukua hatua gani,kwa mujibu wa magazeti alishapeleka taarifa kwa Waziri Mkuu, soma hapa HabariLeo: Gwiji la habari Tanzania | DC aliyechapa walimu ashitakiwa kwa Pinda.

Mimi nadhani kufukuzwa tu haitoshi, hawa waalimu wanahitaji ushauri, manake mmoja niliyemsikia akihojiwa na BBC yaonesha kuna kudhalilika kukubwa mbele ya wanafunzi wao. Pia wanaweza kwenda mahakamani.

Kukimbia tatizo sio kutatua tatizo hilo, je walimu hao wahamishwe au? Wapelekwe mikoa mingine maana watakapo kuwa wanaingia darasani wanafunzi wanaweza kuwadharau. Inawezekana hata watakapohamishiwa wanafunzi wanaweza kuwadharau ila rate ya kuzalauliwa inaweza kuwa ndogo. Sijui mnasemaje?
 
"Hilo ni tukio la aina yake na lakusikitisha sana kwa sababu binadamu hawezi kuongozwa njia kwa kuswagwa kama ng'ombe... ni lazima serkali ichukue hatua kali dhidi ya wahusika".

Huyu ndo anastahili kuwa Waziri mkuu wangu badala ya anayelia mbele ya watu. Viboko vya makalioni vitawatoa akili ya kifisadi Mawaziri woote! Hata hao wabaoitwa Mawaziri vijana wataamuka kulinda Albino usiku wa manane.
 
Kwa taarifa zisizokuwa rasmi kutoka BBC (Leo Afrika) saa tatu kasa robo jioni (ya tarehe 13 Feb 2009) mtangazaji amesema kuwa mheshimiwa huyu 'amefukuzwa kazi'.
wenye habari zaidi tupeni.
 
Taarifa latest ni kuwa Mkuu huyo wa Wilaya tayari amefukuzwa kazi. Hata hivyo naona adhabu hiyo haitoshi kwani Mkuu huyo ametenda kosa la jinai kwa kuumiza mwili na kukiuka upeo wa madaraka yake. Chombo kinachoweza kutoa adhabu ya namna hiyo ni mahakama pekee.

Juu ya kufukuzwa kazi inabidi ashitakiwe mahakamani na ikibidi naye aonjeshwe mboko. Pia washirika wake kama vile Polisi aliyepiga viboko na Walimu Wakuu wa shule husika nao wachukuliwe hatua kwa kutii na kuruhusu utekelzwaji wa amri batili.
 
Kwa taarifa zisizokuwa rasmi kutoka BBC (Leo Afrika) saa tatu kasa robo jioni (ya tarehe 13 Feb 2009) mtangazaji amesema kuwa mheshimiwa huyu 'amefukuzwa kazi'.
wenye habari zaidi tupeni.

Kweli kabisa amefukuzwa kazi na rais.
Lakini amejigamba pia amelekebisha tabia za walimu hao kwani walikuwa wanachelewa kufika kazini kuanzia saa 3.30 - 4.30 sasa watajirekebisha.
 
Kweli kabisa amefukuzwa kazi na rais.
Lakini amejigamba pia amelekebisha tabia za walimu hao kwani walikuwa wanachelewa kufika kazini kuanzia saa 3.30 - 4.30 sasa watajirekebisha.

Huyu apimwe akili kwa sababu anaonekana kuwa ni sociopath kama Blagojevich! Hahaaaa
 
Amekiri kuwa aliwachapa viboko, sasa utaona atakapopelekwa mahakamani, atakana mashtaka na kusema kuwa hakuwachapa! Asiyeamini asubiri siku chache zijazo
 
poleni sana walimu wote mliyopata mboko sasa kama wanafunzi wenyewe walikuwa hawaelewi yaani vichwa vizito!! mkuu usilaumu upande mmoja
 
JK amtimua kazi DC aliyechapa walimu

2009-02-14 10:39:02
Na Waandishi Wetu, Dar na mikoani

Rais Jakaya Kikwete, amemvua madaraka na kumfukuza kazi Mkuu wa Wilaya ya Bukoba (DC), mkoani Kagera, Albert Mnali, kutokana na kitendo cha kuwacharaza bakora walimu wa shule za msingi wa wilaya hiyo.

Habari zilizopatikana jana usiku kutoka ofisi ya Waziri Mkuu zilisema kwamba Rais alichukua hatua hiyo kutokana na mkuu wa wilaya hiyo kufanya kitendo ambacho hakikubaliki, kinadhalilisha na kuwaua moyo waalimu kufanya kazi.

Akiongea na Nipashe kwa njia ya simu, Mwandishi katika ofisi ya Waziri Mkuu, Irene Bwire, alisema kwamba madaraka ya DC huyo yalitenguliwa rasmi kuanzia jana.

Mnali anadaiwa kuwaamrisha polisi kuwacharaza viboko walimu hao kutokana na kusababisha wanafunzi kufeli mitihani pamoja na kuchelewa kazini.

Katika taarifa ya kumfukuza kazi DC huyo, Rais alisema kulingana na taratibu, kamati za nidhamu za wilaya na mikoa ndizo zenye majukumu ya kutoa adhabu kwa wafanyakazi wa umma kama ikionekana inafaa na kwamba kitendo alichofanya mkuu huyo wa wilaya kimekiuka kanuni hiyo.

``Amevunja kanuni na ameidhalilisha ofisi na mamlaka ya ukuu wa wilaya,`` sehemu ya taarifa hiyo ilisema kama ilivyosomwa na Bwire.

Mapema jana, Waalimu karibu nchi nzima walilaani vikali kitendo kilichofanywa na Mkuu huyo Wilaya wakisema kimewadhalilisha na ni ukiukwaji wa haki za binadamu.

Baadhi ya walimu mkoani Ruvuma, walitoa malalamiko yao kwa masharti ya kutotajwa majina, wakisema kitendo hicho alichokifanya DC huyo ni kinyume cha sheria na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Walisema kuwa kitendo hicho kimewadhalilisha sana walimu, si wa watanzania tu bali wa dunia nzima na kwamba haijawahi kutokea walimu kucharazwa bakora na kuongeza kuwa Mnali ameonyesha wazi kuwa amejichukulia madaraka mikononi kwa kutumia cheo chake.

Baadhi ya wakuu wa shule za sekondari mkoani Ruvuma ambao walikuwa kwenye mkutano wa kuboresha elimu ya sekondari mjini hapa, walisema kuwa ipo haja sasa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuchukua hatua za haraka za kumuajibisha Mnali ambapo walitishia kutotamuunga mkono endapo atachelewesha kulitolea maamuzi jambo hilo, ambalo limewakatisha tamaa walimu nchini.

Walimu hao walisema kuwa Mkuu huyo wa Wilaya kabla ya kujichukulia sheria mkononi, alipaswa kutafuta kiini cha tatizo lililosababisha wanafunzi kufeli na kwamba wilaya yake inawataalam waliobobea, wakiwemo maafisa elimu na Katibu waTume ya Utumishi ya Walimu (TSD) ambao wangeweza kumpa ushauri wa kitaalamu na kujua ni kwa nini wanafunzi wamefeli na adhabu ya kuwapa walimu na si vinginevyo.

Naye Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Ruvuma, Luya Ngonyani, alisema kuwa kitendo alichofanya Mnali, kimewasononesha na kuwadhalilisha walimu wenzao na kwamba wanaamini taratibu zingine za kisheria zitafuatwa ili kurejesha utu na heshima ya walimu pamoja na utumishi wao.

Alisema wameunga mkono taarifa ya Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwamtumu Mahiza, ya kumtaka DC huyo akapimwe akili kabla ya taratibu zingine kufuatwa.

Nyanda za Juu wamuomba JK kumfuta kazi DC
Nacho chama cha waalimu (CWT) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, kimemuomba Rais Jakaya Kikwete kutengua wadhifa wa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Albert Mnali, na kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa askari polisi aliyetekeleza amri isiyo halali.

Akizungumza na waaandishi wa habari ofisini kwake jana, Katibu wa CWT Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Tweedsmuir Zambi, alisema chama chao kinalaani kitendo cha Mkuu wa Wilaya hiyo kuamuru walimu wachapwe viboko.

Alisema wanamwomba Rais Kikwete amfute kazi Mnali na pia Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema, amchukulie hatua za kinidhamu polisi aliyetekeleza amri isiyo halali, ya kuwachapa viboko walimu.

Aidha, alisema chama hicho kinamwomba mwajiri wa walimu hao waliochapwa viboko agharimie uhamisho ili kulinda hadhi ya walimu hao kwa kuwa wameathirika kisaikolojia.

Moshi wataka DC ashughulikiwe
Kwa upande wake CWT mkoani Kilimanjaro kimeiomba serikali kumchukulia hatua za kisheria Mnali kutokana na kuwadhalilisha walimu kwa kuwacharaza viboko kwa madai ya kushusha kiwango cha elimu wilayani mwake.

Kaimu Katibu wa CWT, Dauson Temu, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa na kuongeza kuwa kitendo hicho kimewadhalilisha walimu na kuwashushia heshima mbele ya wanafunzi na jamii kwa ujumla.

Alisema CWT kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa hizo na kinalaani vikali kitendo hicho kwani si cha kiungwana wala taratibu za ajira na utawala bora na kuwa kimewaathiri walimu kisaikolojia.

Temu alisema wanaiomba serikali kukemea tabia hiyo na kumwadhibu Mkuu huyo wa wilaya na isitokee kwa kiongozi mwingine wa serikali kutumia vibaya madaraka yake na kuwa walimu watapanga kufanya maandamano ya kupinga kitendo hicho.

``Serikali imchukulie hatua kwani taswira ya sasa inaonekana hadhi ya walimu itashuka hata mbele ya wanafunzi wanaowafundisha na tabia hii isipoangaliwa mapema hata watendaji wa vijiji watawachapa walimu makonde na viboko kwa tuhuma kama hizo,`` alisema Temu.

Alisema Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro imewahi kushika mkia mara sita mfululizo mkoani hapa katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba kuanzia mwaka 1994 hadi mwaka 2000 lakini wadau mbali mbali walikutana na kuondoa kasoro zilizopo na sasa wilaya ya Hai inapeta katika matokeo hayo kila mwaka.

Alisema Mkuu wa Wilaya ya Bukoba hanabudi kutembelea Mkoa wa Kilimanjaro na kujifunza namna mbalimbali za uboreshaji wa elimu katika wilaya yake na si kuwaadhibu walimu pekee, tena kwa adhabu ya aibu ya viboko.

Kaimu huyo alisema toka nchi imepata uhuru wake, hajawahi kusikia kokote duniani mwalimu kuchapwa viboko kwa sababu ya wanafunzi kufeli na kwamba tukio hilo limeweka historia nchini na duniani.

Zaidi ya walimu 32 wa wilayani Bukoba wameripotiwa na vyombo vya habari wakidai kucharazwa viboko na Mnali.

Tume ya Haki za Binadamu yalaani Wakati huo huo, TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, imelaani kitendo cha Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Albert Mnali cha kuwachapa viboko walimu wa shule tatu za msingi, wilayani humo, ikisema kuwa kitendo hicho ni ukiukwaji wa haki za binadamu na kimedhalilisha utu na kuwavunjia heshima kwa wanafunzi, familia zao na jamii kwa jumla.

Walimu walioripotiwa kuchapwa viboko na Mkuu huyo wa Wilaya, ni wa Shule za Msingi za Katerero, Kanazi na Kasenene mkoani Kagera.

Tamko hilo lilisomwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mahfoudha Alley Hamid, kwa niaba ya Mwenyekiti wake, Jaji Mstaafu Amiri Manento, alipozungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Tume hiyo, jijini Dar es Salaam jana.

Jaji Mahfoudha alisema Tume imeshitushwa na kusikitishwa na taarifa kuhusu kitendo kilichofanywa na Mkuu huyo wa Wilaya dhidi ya walimu hao.

``Kitendo hicho ni cha ukiukwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa mujibu wa sheria za nchi hususan Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na mikataba ya kimataifa inayolinda haki za binadamu na misingi ya utawala bora ambayo Tanzania imeridhia,`` alisema Mahfoudha.

Alisema Ibara ya 13 (6) (e) ya Katiba inatamka kuhusu adhabu kwa kusema: ``Ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha.``

Kutokana na hali hiyo, alisema Tume, ambayo ina mamlaka ya Kikatiba, inalaani vikali kitendo kilichofanywa na Mkuu huyo wa Wilaya, ambaye moja ya majukumu yake ni kulinda hazi za binadamu na misingi ya utawala bora.

Alisema uvunjaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora uliofanywa na Mkuu huyo wa Wilaya ni pamoja na kutoa adhabu isiyostahili kwani adhabu ya viboko hutolewa na mahakama peke yake tena kwa kosa la jinai lililoainishwa kisheria.

Pia kutoa adhabu ya kutweza au kudhalilisha utu, ikiwamo walimu wa kike kucharazwa bakora, kuwapa adhabu walimu bila kufuata taratibu za kinidhamu, ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha maafisa elimu wa wilaya na Idara ya Utumishi wa Walimu na kutumia vibaya madaraka aliyokasimiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na akala kiapo.

Alisema kitendo hicho alichokiita cha aina yake na cha aibu nchini, kimeleta athari kubwa kwa walimu, ikiwamo kuwavunjia heshima kwa wanafunzi, familia zao na jamii kwa jumla na pia kimewavunja moyo katika kazi zao za kila siku.

Hata hivyo, aliwataka walimu kuzingatia maadili yao ya kazi ili nao wawatendee haki watoto ya kupata elimu bora, badala ya kuwa watoro, wazembe na walevi kama walivyotuhumiwa.

Imeandikwa na Gideon Mwakanosya, Ruvuma Jackson Kimambo, Moshi Pendo Fundisha, Mbeya na Muhibu Said, Dar

SOURCE: Nipashe
 
Lakini hao walimu walikuwa wanatii amri alali ya mkuu. Na amri ya mkuu haipingwi.

Wewe ndiye Mtanzania halisi. Amri isiyojikita katika sheria za nchi inakuwaje halali? Je Mkuu akituma vijana wake wampelekee mkeo atese naye leo kwenye Valentine unatii mara moja na kuchekelea? Kweli kazi ipo:confused:
 
=Ngongo;375582]JK amtimua kazi DC aliyechapa walimu

Baadhi ya wakuu wa shule za sekondari mkoani Ruvuma ambao walikuwa kwenye mkutano wa kuboresha elimu ya sekondari mjini hapa, walisema kuwa ipo haja sasa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuchukua hatua za haraka za kumuajibisha Mnali ambapo walitishia kutotamuunga mkono endapo atachelewesha kulitolea maamuzi jambo hilo, ambalo limewakatisha tamaa walimu nchini.

Kwa hiyo sasa watamuunga mkono kama kawaida kwa sababu huyo DC ameshafukuzwa kazi??? Kwa hiyo Serikali saaafi!!!!???:confused:

``Serikali imchukulie hatua kwani taswira ya sasa inaonekana hadhi ya walimu itashuka hata mbele ya wanafunzi wanaowafundisha na tabia hii isipoangaliwa mapema hata watendaji wa vijiji watawachapa walimu makonde na viboko kwa tuhuma kama hizo,`` alisema Temu.
Ila pia sina hakika kama walimu wenyewe wanajua hadhi yao kwani kama wangeijua basi wangekuwa tayari kwa lolote na si kulala kupokea chai (zamani bakora tuliambiwa ni chai!!!). Tena mbaya zaidi walimu wakike wanakubali kuchapwa matakoni?? Kama wangekuwa kwenye hali mbaya nani angewasaidia kuokota hizo ped? Bado tatizo ni kubwa na walimu wanatakiwa kuchukua hii kama mahali pa kuanzia!!
 
Baadhi ya walimu mkoani Ruvuma, walitoa malalamiko yao kwa masharti ya kutotajwa majina, wakisema kitendo hicho alichokifanya DC huyo ni kinyume cha sheria na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Walisema kuwa kitendo hicho kimewadhalilisha sana walimu, si wa watanzania tu bali wa dunia nzima na kwamba haijawahi kutokea walimu kucharazwa bakora na kuongeza kuwa Mnali ameonyesha wazi kuwa amejichukulia madaraka mikononi kwa kutumia cheo chake.

Baadhi ya wakuu wa shule za sekondari mkoani Ruvuma ambao walikuwa kwenye mkutano wa kuboresha elimu ya sekondari mjini hapa, walisema kuwa ipo haja sasa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuchukua hatua za haraka za kumuajibisha Mnali ambapo walitishia kutotamuunga mkono endapo atachelewesha kulitolea maamuzi jambo hilo, ambalo limewakatisha tamaa walimu nchini.

Walimu hao walisema kuwa Mkuu huyo wa Wilaya kabla ya kujichukulia sheria mkononi, alipaswa kutafuta kiini cha tatizo lililosababisha wanafunzi kufeli na kwamba wilaya yake inawataalam waliobobea, wakiwemo maafisa elimu na Katibu waTume ya Utumishi ya Walimu (TSD) ambao wangeweza kumpa ushauri wa kitaalamu na kujua ni kwa nini wanafunzi wamefeli na adhabu ya kuwapa walimu na si vinginevyo.

Kwa habari kamili angalia hapa:JK amtimua kazi DC aliyechapa walimu

Haya sasa hao walimu wa sekondari wanaogopa nini kutajwa majina yao? Ni uoga kama huu ndio unaowafanya watu wengine waone kuwa ni ruksa kuwachapa bakora na kuwadhalilisha wapendavyo!
 
Baada ya kupokea habari DC aliondoka katika nyumba ya serikali siku hiyo hiyo kurudi kijijini kwao ambako inasemekana alitayarishiwa mapokezi ya kishujaa, kabla ya kuondoka DC huyo aliwahabarisha wakuu wa kijijini kwake ambao walipita nyumba kwa nyumba ili kutayarisha mapokezi na muda si mwingi kijiji na vijiji vya karibu vilipokezana habari na kuandaa tafrija ya aina yake.
 
Huyu ndo anastahili kuwa Waziri mkuu wangu badala ya anayelia mbele ya watu. Viboko vya makalioni vitawatoa akili ya kifisadi Mawaziri woote! Hata hao wabaoitwa Mawaziri vijana wataamuka kulinda Albino usiku wa manane.

Kitendo cha kumfukuza kazi mkuu huyu wa wilaya ni kitendo cha uonevu. Mkuu huyu aliamua kuwatandika viboko kwa nia njema kabisa ya kuwatisha walimu ili wasirudie tena tabia ya kuchelewa na kutowapa huduma muhimu sana ya elimu bora watoto ambao wamekuwa wakiikosa kwa muda mrefu kutokana na tabia hii mbaya ya walimu.

Ni uonevu kwa kuwa yeye alifikia hatua hiyo akiwa na nia thabiti kabisa moyoni mwake ya watoto wa Bukoba kupata Elimu bora kwa manufaa ya Taifa katika siku zijazo. Huenda kama angepewa muda wa kujitetea basi tungeingiwa na huruma jinsi ambavyo angejitetea na hata chozi kumtiririka kwa uchungu aliyo nao juu ya watoto kutofundishwa na walimu hawa watoro na wazembe, tena usijekuta wengine wamesha sahau hata kusoma kwa uzembe wao. Hapa Rais hajatenda haki kwa mtazamo wangu, kwani hakufanya kwa kujifurahisha bali kwa manufaa ya Watoto - Rejea ya Pinda na wauaji wa Albino ndiyo utakubaliana na mimi kuwa huyu kaonewa
 
Mkuu heshima mbele;

Hata kama walimu walikuwa na makosa makubwa kiasi gani, viboko haikuwa adhabu ya kutolewa na DC kivile. Kama walikosea kuna taratibu zake, kuna kamati za nidhamu za Wilaya na mkoa ambazo ndo vyombo sahihi vya kutoa adhabu kwa walimu hao......!

Kama umesikiliza taarifa mbalimbali utagundua walimu wale wana matatizo mengi sana ikiwa moja wapo ya kuto lipya mshahara kwa zaidi ya miezi sita na pia wanatoka umbali mrefu sana kwenda kny vituo vyao vya kazi...so DC alipashwa kufanya uchunguzi kwanza kabla ya kuamua tu kuwatandika ki vile.....! ndugu yangu chukulia moja ya walimu waliopigwa ni mama yako mzazi....ungefeel vipi? ule ni udhalilishaji wa hali ya juu wa utu!

So binafsi naunga mkono kufukuzwa kazi kwakwe na pia nafikiri anatakiwa apelekwe mahakamani kwa makosa ya jinai!
 
Kitendo cha kumfukuza kazi mkuu huyu wa wilaya ni kitendo cha uonevu. Mkuu huyu aliamua kuwatandika viboko kwa nia njema kabisa ya kuwatisha walimu ili wasirudie tena tabia ya kuchelewa na kutowapa huduma muhimu sana ya elimu bora watoto ambao wamekuwa wakiikosa kwa muda mrefu kutokana na tabia hii mbaya ya walimu.

Ni uonevu kwa kuwa yeye alifikia hatua hiyo akiwa na nia thabiti kabisa moyoni mwake ya watoto wa Bukoba kupata Elimu bora kwa manufaa ya Taifa katika siku zijazo. Huenda kama angepewa muda wa kujitetea basi tungeingiwa na huruma jinsi ambavyo angejitetea na hata chozi kumtiririka kwa uchungu aliyo nao juu ya watoto kutofundishwa na walimu hawa watoro na wazembe, tena usijekuta wengine wamesha sahau hata kusoma kwa uzembe wao. Hapa Rais hajatenda haki kwa mtazamo wangu, kwani hakufanya kwa kujifurahisha bali kwa manufaa ya Watoto - Rejea ya Pinda na wauaji wa Albino ndiyo utakubaliana na mimi kuwa huyu kaonewa

....siku zote TATIZO LETU KUBWA WATANZANIA ni..........tunapofeli tunatafuta mchawi.......wakati mchawi ni sisi wenyewe wana Bukoba (Mkuu wa Wilaya inclusive)..........Kufeli kwa wanafunzi kunachangiwa na mambo mengi............Mkuu wa Wilaya alitakiwa kuweka mikakati ili haya matokeo yasijirudie tena........
 
Kitendo cha kumfukuza kazi mkuu huyu wa wilaya ni kitendo cha uonevu. Mkuu huyu aliamua kuwatandika viboko kwa nia njema kabisa ya kuwatisha walimu ili wasirudie tena tabia ya kuchelewa na kutowapa huduma muhimu sana ya elimu bora watoto ambao wamekuwa wakiikosa kwa muda mrefu kutokana na tabia hii mbaya ya walimu.

Ni uonevu kwa kuwa yeye alifikia hatua hiyo akiwa na nia thabiti kabisa moyoni mwake ya watoto wa Bukoba kupata Elimu bora kwa manufaa ya Taifa katika siku zijazo. Huenda kama angepewa muda wa kujitetea basi tungeingiwa na huruma jinsi ambavyo angejitetea na hata chozi kumtiririka kwa uchungu aliyo nao juu ya watoto kutofundishwa na walimu hawa watoro na wazembe, tena usijekuta wengine wamesha sahau hata kusoma kwa uzembe wao. Hapa Rais hajatenda haki kwa mtazamo wangu, kwani hakufanya kwa kujifurahisha bali kwa manufaa ya Watoto - Rejea ya Pinda na wauaji wa Albino ndiyo utakubaliana na mimi kuwa huyu kaonewa

namshukuru sana rais wa awamu ya hii, kwa hili ametenda kwa wakati na kufuata utawala bora na utawala wa sheria bila kujali nafaisi uwezo wa mtu.

Maan New Employement and labour relation act No 6 of 2004 imebainisha wazi kabisa hata kwa mtu ambye si mtaalmu wa sheria za kazi kwamba nini kifanyika mtumishi wa umma akikosa maadili ya kazi , na hakuna sehemu hata moja inayosema akikosa achapwa bakora.

huku ni kuwazalilisha waalimu na taaluma ya waalimu, yeye kama mkuu wa wilaya hajawi kuchelewa kazi au kufanya kukosa lolote?!

Waalimu kama taaluma lazima watoe tamko kulaini kitendi hiki kwani baadala ya kuendeleza elimu kinashusha elimu yetu kwa kweliu.

Hongera rais wetu kwa kuwa makini kwa hili.
 
Back
Top Bottom