Serikali ilikuwa haipo ? leo ni siku ya tano toka kufanyika kwa tendo hili ,je serikali ilikuwa inanisubiir mpaka pale nilipowazungumza kwamba si kweli Raisi,PM na waziri wake hawana habari ndio wamekurupuka aidha walikuwa wanasubiri mshindo wa WaTanzania, kwa kweli ni aibu kwa serikali hii ambayo inajisifu kuwa imejikita kila pembe ya Tanzania,naamini kabisa hao niliowataja hapo walisikia once kitendo kilipofanyika maana ni kitendo kisichostahili kufanyiwa wafanyakazi wa serekalini na hata wale wasekta binafsi, kwani kuchelewa kazini kunafuatiwa na onyo la barua rasmi na ikiwa onyo hilo halikufua dafu ni kufukuzwa kazi vilevile kwa barua rasmi ,DC aliziona taratibu hizo zote hazifai na ni kucheleweshana.
Viongozi hao wakuu kuanzia Mkuu wa Mkoa ichunguzwe nae alichukua hatua gani ,je alitaarifu uongozi wa juu pale aliposikia kioja hicho ? Au alikaa nae kusikiliza mshimndo ? Tunaweza kusema Raisi alisikia kutoka kwa mashushu lakini akangoja ushahidi kamili wa Mkuu wa Mkoa ,aidha Mkuu wa Mkoa sina uhakika kama anaweza kumsimamisha kazi ,lakini kwa upande fulani ikiwa amehakikisha tendo hilo limefanywa angeweza kabisa kumsimamisha kazi na japo sio kumfukuza bila ya shaka aliona atamvunjia heshima mwenziwe kwa kumsimamisha kazi ,anaogopa ,atakuwa hana adabu ,ndio maana yake viongozi waliopewa madaraka wanashindwa kukemea wanashindwa kuwawajibisha wababe anangojewa Raisi ndipo pale niliposema kuwa hawa wote wameoza na kunahitajiwa Chama cha uongozi chengine CCM hawafai kwani wanaogopana ,mi nakuaminia kabisa Mkuu wa mkoa anamwogopa hata balozi wa nyumba kumi kumi ,sasa hapa unafikiri kuna utawala wa kufuata sheria ni mazonge tu ,Kikwete nae amakerupuka baada ya siku kibao kupita ameona joto linaanza kupanda kwa kasi ,kwani Kikwete anaielewa vizuri maana ya kasi ,sasa afahamu tu anaposikia udhalilishaji kama huu basi ampigie simu muhusika moja kwa moja na kumuuliza ,eti jamani kama huyo DC baada ya kufanya mauzauza hayo ,na Mheshimiwa Raisi kusikia basi Mheshimiwa angeweza kumhoji direct na baada ya kupata uhakika kuwa jamaa amekiri ,hapohapo angekata simu na kutangaza kumsimaisha kazi na sheria ya kunyanyasa au kudhalilisha ichukue mkondo wake aidha na walimu walipwe fidia na mwajiri aliewadhalilisha mambo ya kufukuzana kazi halafu jamaa akawa anapeta uraiani hayatoshi tunataka kusikia kuwa amekwenda jela mwaka mmoja na kila asubuhi anachapwa kiboko kimoja tu, ubabe tu ,ndio maana yake.