DC Ally Hapi: Uwanja wa Fisi kubadilishwa na kujengwa shopping malls

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,950
29,532
Nimemuona DC Hapi katika maadhimisho ya asasi ya Patrice Lumumba.

Kuna maelezo aliyoyatoa kuhusu maisha ya watu wanaoishi maeneo ya uwanja wa fisi.

Amesisitiza kuwa yeye hataamuru polisi kupita nyumba kwa nyumba ili kuwakamata wanaoishi huko ambao wanajihusisha na uchangudoa kwenye madanguro.

Ameenda mbali na kusema kuwa anafikiria kulibadilisha eneo hili na kulifanya eneo la uwekezaji kwa kujenga shopping malls na vitu vya namna hiyo.

Ingawa hakugusia ni wapi wakazi hao watapelekwa lakini aliahidi kuwafidia.

Source ni channel ten jioni hii

My take:

Ana wazo zuri sana la kitaka kulibadili eneo hili la uwanja wa fisi lakini nina wasiwasi na kauli yake hii na dhamira yake kama sio ya kutaka kumnanga mkuu wa mkoa hasa hasa katika kipindi hiki tunachoshuhidia mvutano wa ndani ya mtandao.

Naamini haya aliyoyasema ni jibu kwa ile thread iliyoliliwa kumpa ban Lizaboni
 
Hawa vijana wa CCM Magufuli awaangali sana, hawapo kwa maslai ya nchi zaidi ya matumbo yao.!

Ni utovu wa nidhamu DC kupinga agizo la RC hata kama linamakosa....ana namna nyingi za kuwasiliana Na boss wake....DC akumbuke alikula kiapo kwa RC.





Mkubwa naona unajilazimisha kusahau,huo ndiyo mfumo wa uendeshaji wa serikali ya awamu ya 5,katika awamu hii hakuna kiongozi hata mmoja anayejipa muda wa kutafakari kabla ya kuitoa kauli yake mbele ya Umma,wote ni wakurupukaji tu.Unajuwa kuwa hata wale waliotumbuliwa kwa mbwembwe mbele ya makamera wengi wao wamerudishwa katika utumishi wao kimya kimya?

Pamoja na nia njema ya serikali hii,lakini imejidhihirisha kuwa na nakisi kubwa sana ya hekima na busara,ikiirekebisha kasoro hiyo inaweza kuwa serikali nzuri sana,lakini ikiendelea na mwenendo huu wa "kutekwa na hadhira", inaweza kujikuta inalaumiwa kila kona.
 
Back
Top Bottom