DC wa Bariadi adaiwa kushinikiza wananchi kupiga kura ya siri kuwataja wachawi na wenye Fisi

Fanfa

JF-Expert Member
Sep 25, 2009
1,815
2,862
Nimepokea taarifa kutoka kwenye chanzo chenye uhakika zikidai kuwa DC wa Bariadi amewashinikiza wananchi wa mtaa wa Mangaka wilayani Bariadi kupiga kura ya siri kuwaandika majina wachawi na wenye Fisi.

Takribani wiki tatu (3) zilizopita tulisikia habari za fisi kujeruhi na kuua watu kadhaa katika Mtaa wa Mangaka wilayani Bariadi. Katika kulishughulikia tatizo la fisi kujeruhi na kuua wananchi wa mtaa huo, Mkuu wa wilaya hiyo aliitisha kikao katika mtaa ule na kuwaeleza wananchi kuwa Fisi hao ni wa wachawi na kuwataka Wakina mama wawadhibiti fisi wao la sivyo atawachukulia hatua kali wahusika.

Viongozi (Mtendaji na mwenyekiti wa Mtaa) na wananchi wa eneo hilo hawakufurahishwa na kauli hiyo ya mkuu wa wilaya ya kuhusisha hao Fisi na mambo ya kichawi/Kishirikina. Badala ya kuwasaidia wananchi ili Fisi hao waondoshwe na mamlaka ya maliasili, badala yake mkuu huyo wa Wilaya amechukua hatua zifuatazo.

Tarehe 22/04/2022 katika mtaa wa Mangaka aliitisha kikao kwa njia ya Mwano (kupiga yowe ili wananchi wakusanyike) na kuwatuhumu wananchi kuwa baadhi yao ni wachawi na kwamba fisi wao wanajeruhi na kuua watu katika mtaa huo. Alieleza kuwa anataka kuwakamata wachawi wote na kuwashughulikia kwa kuwa wanawatuma fisi wao kwenda kuua na kula watu. Baada ya maelezo hayo aliwaamuru kwa nguvu kila mwananchi aandike majina ya wachawi anaowafahamu katika mtaa huo kwa njia ya siri. Wananchi waliosema hawajui mchawi waliwekwa pembeni. Wananchi waliokubali kupiga kura ya siri kuwataja wachawi waliruhusiwa kuondoka. Wale waliosema hawawajui wachawi walibakizwa na kuanza kupewa vitisho kuwa wasipowataja wachawi na wenye fisi basi wao ndo wachawi na kwamba angeondoka nao wasipofanya hivyo. Wananchi hao walioendelea kuwa na msimamo wa kutowatambua wachawi na wenye fisi, baadae aliwaandika majina na kuwaachia na kuwaeleza kuwa atawachukulia hatua.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa, kabla ya zoezi hilo la upigaji kura kufanyika, mnamo tarehe 20/04/2022 Mkuu wa Wilaya alimwagiza mwenyekiti wa mtaa wa Mangaka Bw. Mdeli Masanja aitishe kikao cha wananchi wote wa mtaa huo ili tarehe 21/04/2022 saa 1 asubuhi akutane nao kwa ajili la swala hilo la kutambua wachawi. Mwenyekiti wa mtaa Bw. Mdeli Masanja hakufanya kama alivyoagizwa na mkuu huyo wa wilaya. Ilipofika tarehe 21/04/2022 asubuhi ya saa moja na nusu, Mkuu wa wilaya alifika eneo la mkutano akiwa ameambatana na Polisi, lakini hakukuta mtu. Akampigia mwenyekiti aende kwenye eneo la makutano. Mwenyekiti wa mtaa alitii na kwenda eneo husika na alipofika alikamatwa kwa madai kuwa hakuwajulisha wananchi na yeye mwenyewe hakufika muda waliokubaliana. Mwenyekiti aliwekwa ndani tangu tarehe 21/04/2022 na mpaka jana jioni ya tarehe 22/04/2022 majira ya saa 2 usiku alikuwa bado yuko lockup. Kikao cha jana (22/04/2022) cha mkuu wa wilaya na wananchi wa mtaa huo kilifanyika huku mwenyekiti wa mtaa akiwa lockup polisi.

Matendo haya ya hovyo yanayofanywa na DC wa Bariadi yanaichafua Serikali na hata mamlaka yake ya uteuzi. Kwamba serikali inaamini Fisi ni mali ya wachawi na kwamba fisi wanatumwa na wachawi kwenda kujeruhi au kuua watu. Kama mtu level ya mkuu wa Wilaya na mwakilishi wa Mhe. Rais anaamini haya na kuanza kupiga ramli chonganishi kwa wananchi, je, wananchi wa kawaida itakuwaje?.

Tunapswa kujiuliza maswali haya;

  • Kosa alilofanya mwenyekiti wa mtaa Bw. Mdeli Masanja na kupelekea kuwekwa ndani na mkuu wa wilaya ni lipi?
  • Je, DC wa Bariadi anataka kutuambia kuwa serikali inaamini Fisi wanaojeruhi watu wanatumwa na wachawi na kwamba serikali inaamini katika uchawi?
  • Kama DC wa Bariadi anawajua wachawi na wenye Fisi kwa nini asiwakamate badala ya kulazimisha wananchi wawataje?
  • Je, Serikali imeshatoa mwongozo wa namna ya kuwatambua wananchi wachawi na wamiliki wa fisi.
  • Je, kuna sheria zinazoshughulikia makosa ya kichawi na matumizi ya fisi kwenye uchawi.
  • Mkuu wa wilaya ni mlizi wa amani ndani ya wilaya yake, inakuwaje awe chanjo cha ramli chonganishi?
Tabia hii ya DC wa Bariadi inabidi ikemewe kwa nguvu zote na ikomeshwe kabisa, maana itasababisha madhara makubwa sana kwa wananchi. Madhara hayo ni kama yafutavyo;

  • Tutegemee matukio ya akinamama wazee na wenye macho mekundu kukatwa mapanga na mashoka kwa tuhuma za uchawi yataibuka tena kwa kasi ya ajabu kwa kuwa wananchi sasa wameaminishwa na serikali kuwa kuna wachawi wanatuma fisi kuua watu.
  • Imani potofu kwa watu kuamini kuwa mtu akiumwa na fisi basi katumwa na mchawi
  • Baadhi ya wananchi watatumia visasi na chuki walizonazo dhidi ya wengine kuwatangaza na kuwachafua wenzao mbele ya jamii kuwa ni wachawi kwa lengo la kukomoana.
Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa pamoja na mamlaka za uteuzi wa DC wa Bariadi kwa heshima na taathima naomba mfuatilie swala hili. Mambo anayofanya mkuu wa wilaya yanaichafua serikali ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wananchi wanaamini kuwa anachofanya DC wa Bariadi ni maagizo ya serikali. Serikali ilifuatilie jambo hili kwa haraka na kuchukua hatua stahiki dhidi ya DC wa Bariadi. Likiachwa hilo jambo bila mhusika kuchukuliwa hatua kali, wananchi watajenga chuki dhidi ya serikali yao.

Tuwasaidie wananchi wa Bariadi kupiga kelele ili mamlaka husika zisikie na zifuatlie swala hili.
 
Mtaa-Nyangaka (mjini bariadi) hata mimi nilishangaa Sana, badala ya kusisitiza wananchi waondoe vichaka na kupuluni miti na kukwangua barabara, anaongea Mambo chonganishi, Sasa watu wakianza kukatwa mapanga kwa sababu ya uchawi sijui tena atasemaje?
 
Kwanini mwenyekiti wa kijiji ammepuuza agizo la DC
Kwa sababu aliona ni jambo la kijinga na la kipuuzi kwa DC kuwakusanya wananchi ili wapige kura ya kuwatambua wachawi na wenye Fisi. Kwani huyo DC ana kipimio cha kutambua wachawi na wamiliki wa fisi. Hongera kwa mwenyekiti kukataa ujinga huo wa karne.
 
Asante sana mkuu kwa masahihisho. Naomba moderator ubadilishe na isomeke "mtaa wa Nyangaka"
Moderator

Ni Mkuu wa wilaya wa ajabu sana. Kwa karne hii bado anaamini mambo ya ushirikina. Tunaamini mamlaka za uteuzi zitachukua hatua madhubuti kukomesha tabia hii
Haijalishi karne mkuu, uchawi bado upo..

Ila kwa nafasi ya DC alipaswa kuagiza askari wanyamapori kuweka kambi hapo na kutafuta hao fisi..

Pia angeagiza serikali ya mtaa kutenga siku moja ya weekend kusimamia wananchi kukata vichaka vyote..

Vilevile kutoruhusu watu kuzurula ovyo usiku haswa watoto na wanawake, na kama ni wanaume basi iwe kwa vikundi..
 
Mie nashindwa kuelewa kwamba inawezekana 2022 kuwa na Mkuu wa Wllaya kihiyo kiwango hiki!
 
Kuna watu wanafuga fisi huko
Wanasaidia kwenye kazi mbali mbali

images - 2022-04-24T001351.164.jpeg
 
Kwa sababu aliona ni jambo la kijinga na la kipuuzi kwa DC kuwakusanya wananchi ili wapige kura ya kuwatambua wachawi na wenye Fisi. Kwani huyo DC ana kipimio cha kutambua wachawi na wamiliki wa fisi. Hongera kwa mwenyekiti kukataa ujinga huo wa karne.
Mwenyekiti kakosa hekima ya uongozi. Kazi yake ilikuwa kuitisha kikao, wananchi ndio wangejenga hoja kumshawishi DC aachane na mpango huo!
 
Nimepokea taarifa kutoka kwenye chanzo chenye uhakika zikidai kuwa DC wa Bariadi amewashinikiza wananchi wa mtaa wa Mangaka wilayani Bariadi kupiga kura ya siri kuwaandika majina wachawi na wenye Fisi.

Takribani wiki tatu (3) zilizopita tulisikia habari za fisi kujeruhi na kuua watu kadhaa katika Mtaa wa Mangaka wilayani Bariadi. Katika kulishughulikia tatizo la fisi kujeruhi na kuua wananchi wa mtaa huo, Mkuu wa wilaya hiyo aliitisha kikao katika mtaa ule na kuwaeleza wananchi kuwa Fisi hao ni wa wachawi na kuwataka Wakina mama wawadhibiti fisi wao la sivyo atawachukulia hatua kali wahusika.

Viongozi (Mtendaji na mwenyekiti wa Mtaa) na wananchi wa eneo hilo hawakufurahishwa na kauli hiyo ya mkuu wa wilaya ya kuhusisha hao Fisi na mambo ya kichawi/Kishirikina. Badala ya kuwasaidia wananchi ili Fisi hao waondoshwe na mamlaka ya maliasili, badala yake mkuu huyo wa Wilaya amechukua hatua zifuatazo.

Tarehe 22/04/2022 katika mtaa wa Mangaka aliitisha kikao kwa njia ya Mwano (kupiga yowe ili wananchi wakusanyike) na kuwatuhumu wananchi kuwa baadhi yao ni wachawi na kwamba fisi wao wanajeruhi na kuua watu katika mtaa huo. Alieleza kuwa anataka kuwakamata wachawi wote na kuwashughulikia kwa kuwa wanawatuma fisi wao kwenda kuua na kula watu. Baada ya maelezo hayo aliwaamuru kwa nguvu kila mwananchi aandike majina ya wachawi anaowafahamu katika mtaa huo kwa njia ya siri. Wananchi waliosema hawajui mchawi waliwekwa pembeni. Wananchi waliokubali kupiga kura ya siri kuwataja wachawi waliruhusiwa kuondoka. Wale waliosema hawawajui wachawi walibakizwa na kuanza kupewa vitisho kuwa wasipowataja wachawi na wenye fisi basi wao ndo wachawi na kwamba angeondoka nao wasipofanya hivyo. Wananchi hao walioendelea kuwa na msimamo wa kutowatambua wachawi na wenye fisi, baadae aliwaandika majina na kuwaachia na kuwaeleza kuwa atawachukulia hatua.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa, kabla ya zoezi hilo la upigaji kura kufanyika, mnamo tarehe 20/04/2022 Mkuu wa Wilaya alimwagiza mwenyekiti wa mtaa wa Mangaka Bw. Mdeli Masanja aitishe kikao cha wananchi wote wa mtaa huo ili tarehe 21/04/2022 saa 1 asubuhi akutane nao kwa ajili la swala hilo la kutambua wachawi. Mwenyekiti wa mtaa Bw. Mdeli Masanja hakufanya kama alivyoagizwa na mkuu huyo wa wilaya. Ilipofika tarehe 21/04/2022 asubuhi ya saa moja na nusu, Mkuu wa wilaya alifika eneo la mkutano akiwa ameambatana na Polisi, lakini hakukuta mtu. Akampigia mwenyekiti aende kwenye eneo la makutano. Mwenyekiti wa mtaa alitii na kwenda eneo husika na alipofika alikamatwa kwa madai kuwa hakuwajulisha wananchi na yeye mwenyewe hakufika muda waliokubaliana. Mwenyekiti aliwekwa ndani tangu tarehe 21/04/2022 na mpaka jana jioni ya tarehe 22/04/2022 majira ya saa 2 usiku alikuwa bado yuko lockup. Kikao cha jana (22/04/2022) cha mkuu wa wilaya na wananchi wa mtaa huo kilifanyika huku mwenyekiti wa mtaa akiwa lockup polisi.

Matendo haya ya hovyo yanayofanywa na DC wa Bariadi yanaichafua Serikali na hata mamlaka yake ya uteuzi. Kwamba serikali inaamini Fisi ni mali ya wachawi na kwamba fisi wanatumwa na wachawi kwenda kujeruhi au kuua watu. Kama mtu level ya mkuu wa Wilaya na mwakilishi wa Mhe. Rais anaamini haya na kuanza kupiga ramli chonganishi kwa wananchi, je, wananchi wa kawaida itakuwaje?.

Tunapswa kujiuliza maswali haya;

  • Kosa alilofanya mwenyekiti wa mtaa Bw. Mdeli Masanja na kupelekea kuwekwa ndani na mkuu wa wilaya ni lipi?
  • Je, DC wa Bariadi anataka kutuambia kuwa serikali inaamini Fisi wanaojeruhi watu wanatumwa na wachawi na kwamba serikali inaamini katika uchawi?
  • Kama DC wa Bariadi anawajua wachawi na wenye Fisi kwa nini asiwakamate badala ya kulazimisha wananchi wawataje?
  • Je, Serikali imeshatoa mwongozo wa namna ya kuwatambua wananchi wachawi na wamiliki wa fisi.
  • Je, kuna sheria zinazoshughulikia makosa ya kichawi na matumizi ya fisi kwenye uchawi.
  • Mkuu wa wilaya ni mlizi wa amani ndani ya wilaya yake, inakuwaje awe chanjo cha ramli chonganishi?
Tabia hii ya DC wa Bariadi inabidi ikemewe kwa nguvu zote na ikomeshwe kabisa, maana itasababisha madhara makubwa sana kwa wananchi. Madhara hayo ni kama yafutavyo;

  • Tutegemee matukio ya akinamama wazee na wenye macho mekundu kukatwa mapanga na mashoka kwa tuhuma za uchawi yataibuka tena kwa kasi ya ajabu kwa kuwa wananchi sasa wameaminishwa na serikali kuwa kuna wachawi wanatuma fisi kuua watu.
  • Imani potofu kwa watu kuamini kuwa mtu akiumwa na fisi basi katumwa na mchawi
  • Baadhi ya wananchi watatumia visasi na chuki walizonazo dhidi ya wengine kuwatangaza na kuwachafua wenzao mbele ya jamii kuwa ni wachawi kwa lengo la kukomoana.
Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa pamoja na mamlaka za uteuzi wa DC wa Bariadi kwa heshima na taathima naomba mfuatilie swala hili. Mambo anayofanya mkuu wa wilaya yanaichafua serikali ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wananchi wanaamini kuwa anachofanya DC wa Bariadi ni maagizo ya serikali. Serikali ilifuatilie jambo hili kwa haraka na kuchukua hatua stahiki dhidi ya DC wa Bariadi. Likiachwa hilo jambo bila mhusika kuchukuliwa hatua kali, wananchi watajenga chuki dhidi ya serikali yao.

Tuwasaidie wananchi wa Bariadi kupiga kelele ili mamlaka husika zisikie na zifuatlie swala hili.
Ngumu sana maswala haya.Kamati ya ulinzi yake inaishia kwa majeshi tu wangekuwa wanawatu kadhaa wa uhakika kwa kamati ya asili.
 
Back
Top Bottom