Yaliyojiri wakati Rais Magufuli alipokutana na Mabalozi wa Tanzania wanaoiwakilisha taifa nchi za nje

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ambayo inajengwa kwa fedha za Watanzania.

Mabalozi hao 43 ambao wapo hapa nchini tangu tarehe 13 Agosti, 2019 wametoa pongezi hizo leo tarehe 22 Agosti, 2019 walipokutana na kuzungumza na Rais Magufuli Ikulu Jijini DSM.

Wametoa pongezi hizo baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa bwawa la Nyerere katika Mto Rufiji, mradi wa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (standard gauge railway), jengo la 3 la abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, mradi wa ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya barabara ya Morogoro na Sam Nujoma (Ubungo Interchange), mradi wa upanuzi wa bandari ya DSM, mradi wa usambazaji wa gesi (Taifa Gas), mradi wa udhibiti wa mawasiliano Tanzania na mradi wa ujenzi wa daraja la Tanzanite (New Selander Bridge) katika bahari ya Hindi.

Kwa upande wa Zanzibar wametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la biashara na makazi (shopping mall) eneo la Michenzani, mradi wa ujenzi wa jengo la 3 la abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sheikh Abeid Amani Karume, mradi wa ujenzi wa nyumba za kisasa wa Fumba Wilaya ya Magharibi, mradi wa ujenzi wa barabara ya Kaskazini – Bububu – Mkokotoni na mradi wa ujenzi wa bandari ya mafuta na gesi katika eneo la Manga Pwani.

Mabalozi hao wameeleza kuwa utekelezaji wa miradi hiyo pamoja na juhudi nyingine kubwa zinazofanywa na Serikali katika nyanja mbalimbali za huduma za jamii zimeleta heshima kwa nchi na machoni mwa Jumuiya ya Kimataifa, na kwamba zimedhihirisha kufikiwa kwa malengo ya Tanzania kuingia katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Pia wamempongeza kwa kuwa Mwenyekiti SADC kwa kipindi cha mwaka mmoja na wameahidi kuongoza vyema katika mikutano ya Mabalozi wa SADC katika nchi wanazowakilisha kwa kuzingatia mwelekeo ambao Mhe. Rais Magufuli ameutoa katika Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC uliofanyika tarehe 17-18 Agosti, 2019 Jijini DSM.

Akizungumza baada ya kuwasilikiza Mabalozi hao, Rais Magufuli amewapongeza kwa kazi wanazozifanya katika nchi wanazoiwakilisha Tanzania na amewataka waendelee kutekeleza majukumu yao kizalendo na kwa kutanguliza maslahi ya Tanzania.

Pamoja na kueleza kuhusu hali ya uchumi wa nchi, juhudi za kuwapelekea
maendeleo Watanzania na juhudi za kujenga uwezo wa kujitegemea, Rais Magufuli amewataka Mabalozi hao kutafuta wawekezaji watakaowekeza katika miradi yenye manufaa hapa nchini.

“Nataka Mabalozi mtuletee miradi ya maendeleo, ifike mahali Balozi ujiulize kwa kuwa kwangu Balozi nimepeleka nini nyumbani? Nimewezesha kujengwa kiwanda? Kujengwa barabara? Kujenga daraja au jengo fulani?” Rais Magufuli.

Rais Magufuli amewasisitiza Mabalozi hao kuhakikisha wanasimamia na kufuatilia kwa karibu masuala wanayoamini yana manufaa kwa nchi ikiwemo uwekezaji na kwamba wasikubali kukwamishwa na viongozi ama wizara yoyote.

“Nataka muwe very aggressive, na ukiona mtu anakukwamisha mimi nipo niandikieni uone kama hatakwama yeye, mimi nataka kuona vitu sio maneno maneno” amesisitiza Rais Magufuli.


1(6).jpeg
IMG_20190822_190128.jpeg
IMG_20190822_190131.jpeg
 
No!
Mkutano huu ni muhimu sana, Tanzania tunatekeleza diplomasia ya kiuchumi, ila ubalozini tuna waambata wa kijeshi tuu, hatuna waambata wa uchumi!. To be able to move forward, things must change.
P
Ni waambata wa kisiasa kaka maana tangu wameteuliwa kuwa mabalozi siyo Mara ya kwanza Mh Raisi anawaasa habari ya kuleta wawekezaji nyumbani, naisi bado awajakwiva kiuchumi!
 
Sekta binafsi bado ambapo ndiyo walipo walipa kodi wakubwa. Mfano mradi wa nyumba za kisasa, Fumba wilaya ya Magharibi tu ndiyo wa Sekta binafsi. Vipi kuvutia uwekezaji ktk viwanda vya kubangua korosho kuongeza thamani na viwanda vya kusindika mazao / soko la uhakika kwa mazao yote ya kilimo, mifugo na uvuvi. Au mabalozi hawatakiwi kuunga mkono juhudi binafsi za wakulima wengi wanyonge na wavuja jasho wa sekta binafsi?

Naona mkazo ni madaraja, reli na barabara . Mikutano ya mabalozi wetu na mwanadiplomasia namba moja (Mh. Rais) na namba 2 (Waziri Mambo ya Nje) inabidi wasikilize maoni yetu pia ili kutanua wigo wa majukumu msingi ya mabalozi wetu nje ya nchi.

Source : Channel ten
 
August 2019
Dar es Salaam, Tanzania
MANENO YA HUSSEIN BASHE KWENYE KUFUNGA MKUTANO WA SADC Naibu waziri wa kilimo Hussein Bashe amesema kuwa serikali haina mashamba na " serikali haina sera ya kilimo hivyo tunaipitia upya sera ya kilimo na kuifanya kuwa ya kisasa"..

Source : Global TV online

N.B
Mawazo nje ya miundo mbinu ya barabara na reli ndiyo yatachochea kilimo na viwanda vinavyoendana na mazingira ya nchi yetu.
 
Awamu hii kipaunbele ni miradi ya maendeleo tu maswala mengine yamefumbiwa macho kabisaaaa mf:- demokrasia,katiba mpya,kampeni ya haki sawa sijui kama pengine usawa ulishapatikana,haki ya kumkwamua mwanamke kielimu pale atakapo pata ujauzito akiwa shuleni,uzazi wa mpango n.k
 
Sijaona nchi yoyote kubwa kiuchumi au inayotaka kujinasua kiuchumi, ikijisifia kwa miundo-mbinu bali huona ikijisiifia kwa kutengeneza au kuweka mazingira ya kuongeza ajira, ujenzi wa viwanda kimkakati kutegemea na maliasili ilizonazo au ufundi na tekenelojia iliyo nayo kuzidi nchi zingine n.k
Ultimately, nations succeed in particular industries because their home environment is the most forward-looking, dynamic, and challenging. Source: https://hbr.org/1990/03/the-competitive-advantage-of-nations
 
Diplomasia ipi ya kiuchumi? 😳 ya kuwawekea vikwazo vya kiuchumi wafanyakazi kwa kuwanyima nyongeza kwa miaka minne sasa na kuwadhulumu mabilioni ya pesa wakulima wa korosho pia kupunguza kiwango cha mzunguko wa pesa nchini!? 😳

Mkutano huu ni muhimu sana, Tanzania tunatekeleza diplomasia ya kiuchumi, ila ubalozini tuna waambata wa kijeshi tuu, hatuna waambata wa uchumi!. To be able to move forward, things must change.
P
 
Hakuna balozi yeyote Kati yao aliyedukuliwa kweli? Kama yupo na clip ipo mikononi mwake, ole wake!
 
No!
Ni waambata wa kisiasa kaka maana tangu wameteuliwa kuwa mabalozi siyo Mara ya kwanza Mh Raisi anawaasa habari ya kuleta wawekezaji nyumbani, naisi bado awajakwiva kiuchumi!
Set up ya balozi zetu waambata ni wa kijeshi tuu, labda sasa ndio tuanzishe waambata wa uchumi. Mambo mengine yote ya ubalozini, yanashughulikiwa na Minister Plenipotentiary .P
 
Sijaelewa kitu hapa. Yaani balozi alete ujenzi wa barabara, kiwanda, daraja nk. Ninaona kama mabalozi hawa wametumwa kwenda kuwa ombaomba kwa niaba ya nchi. Ni hao hao tunaowaita mabeberu siku nyingine na kwamba wasitupangie mambo yetu??? Mbona tunasema vitu hivo tunajenga kwa fedha zetu za ndani??

Imefika wakati tukiri sisi sio nchi tajiri wala hatuwezi kuwa dona kantri - kama balozi anahitajika kuleta miradi ya barabara na madaraja kutoka nchi wanazotuwakilisha.

Tukubali kuwa sisi ni tegemezi na wanafiki!! Inasikitisha!
 
No!
Ni waambata wa kisiasa kaka maana tangu wameteuliwa kuwa mabalozi siyo Mara ya kwanza Mh Raisi anawaasa habari ya kuleta wawekezaji nyumbani, naisi bado awajakwiva kiuchumi!
kuleta wawekezaji..., ni lini tutaanza kupeleka wawekezaji.., naomba niulize hao wawekezaji wanakuja ili tupate ajira then what ?..., tunashindwa kupata teknolojia ya kujilisha wenyewe na kujivisha wenyeywe na tukiungua tukatumia miti shamba yetu..., Issue ya wawekezaji ndio waje ila wakija mara zote ni makombo na masalia ndio yanabaki na hayo makombo kamwe hayafiki kwa makabwela....
 
Back
Top Bottom