DC JOKATE MWEGELO: TAA ZA KISASA KUWEKWA ENEO LA NJE MKABALA NA UWANJA WA BENJAMIN MKAPA TEMEKE.
MKUU wa Wilaya ya Temeke, Mhe Jokate Mwegelo ametanabaisha dhamira yake ya kubadilisha taswira ya muonekano wa eneo la mbele ya Ofisi DC iliyopo maeneo ya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wanahabari mara baada ya kukutana na Maafisa wa TARURA, wa Manispaa wakiongozwa na mkurugenzi wa Manispaa Mh. Jokate alisema eneo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya linatazamana na uwanja wa Benjamin Mkapa na kwamba hukutanisha maelfu ya Watanzania na watu wa mataifa mbalimbali, hivyo ni vyema taswira yake ikaendana na hadhi hiyo.
"Eneo hili lina taswira ya Kitaifa na Kimataifa kwa kuwa hutumika katika michezo na dhifa mbalimbali za kiinchi, hivyo ni lazima linafanane na hadhi hiyo", alisema.
Alisema ana taarifa za uhalifu nyakati za usiku ambapo eneo hilo kwa kukosa taa huwa na kiza kinene, kinachopelekea wepesi wa vitendo viovu kufanyika.
"Mimi ni mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa wilaya ya Temeke haitaleta afya hata kidogo uhalifu kufanyika eneo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya na kwa Temeke usalama ni moja ya kipaumbele chetu" Alisema Mhe. Mwegelo.
Meneja wa TARURA ambaye pia ni mratibu wa uendelezaji Jiji la Dar es Salaam, amesema kuwa zoezi la ukarabati na uwekaji wa taa 32 katika eneo hilo la barabara lenye urefu wa kilometa 1.3 litagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 102 na litakamilika baada ya majuma mawili mara baada ya taratibu nyingine kukamilika.
Naye Diwani wa kata ya Miburani, Mhe.Juma Mkenga amemshukuru Mkuu wa wilaya Jokate kwa kutambua umuhimu wa eneo hilo na kwamba uwekaji wa taa hizo kwa kiasi kikubwa utapunguza matukio ya uhalifu na kulipa heshma eneo la uwanja wa Taifa.
Kwa kipindi kirefu wananchi wamekuwa wakilalamikia eneo hilo hasa kwa kukithiri kwa vitendo vya kiuhalifu kama uporaji hasa nyakati za usiku. Lakini mheshimiwa Jokate amedhamiria kukomesha uovu huo na kuwa historia.