Specification zake ni zile zile zinazoelezewa kwenye mtandao wa SONY. Na picha vile vile. Baadhi ni kwamba haiingii maji. Pia kamera yake ina ki button chake maalum pembeni huna haja ya kufungua simu kutafuta screen yenye app ya kupigia picha, by the time unapiga picha tukio lishatokea, picha huna. Pia ina megapixels 20.1Ebu nipe specification zake.. Na inavyoonekana ipige picha usiwe ya kichina.. ni PM
Kingine cha muhimu, kuliko vyote labda, kwa mazingira ya umeme mgogoro wa TANESCO, simu hii inakaa na charge kuliko simu zote duniani kwa sasa, kwa maelezo ya baadhi ya reviewers. Hukosi service eti chaji imeisha katikati ya siku.
Kuhusu uchina na ufeki nadhani tukiitumbukiza ndani ya maji itakuwa the best test. Kwa sababu sidhani kama Mchina atatengeneza simu feki ambayo haiingii maji . Kwa hiyo we njoo na chupa la Uhai, mi ntakua na kibeseni tutaiwashia kwenye maji tuipotezee kwa muda uliokuwa nao wewe kama itazima. Lakini kama una ma test yako mengine ya kimaufundi zaidi itakuwa bora pia. Kaa huna utaalam wowote hujui ya ukweli wala ya ufamba basi ukipenda chukua simu ukigundua feki rudi uchukue helaako.