micro_almunia
Senior Member
- Jan 16, 2011
- 134
- 37
Ndugu wana JamiiForums,
Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu yaliyo Jijini Dar es salaam , miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani pwani. DAWASCO inapokea maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.
Ndugu wana jukwaa, DAWASCO inajipambanua kwa kusimamia maadili ,kutoa huduma iliyotukuka pamoja na kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa kila mwananchi.
Kama kutatokea kuharibika kwa bomba, wizi wa Maji, umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:
1. Kupitia tovuti: DAWASCO - Welcome to new site
2. Kupitia mitandao yetu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter|DawascoOfficial..Facebook|DawascoOfficial ...Instagram|DawascoOfficial
3. Kwa mwananchiposta ; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:
Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASCO
P. O. Box 5340
Sokoine Drive
Dar es Salaam, Tanzania.
4. Au kwa kupiga simu huduma kwa wateja dawasco
0800110064 /022 2164800 ( Kupiga namba hizi ni Bure)
THREAD IMELALA SANA DAWASCO. Ni bora muifunge kama hamkujipanga kuitumia kuwafikia wateja. Kama kuna pesa munailipia, basi ni matumizi yasiyo na tija.