DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Kwanza napenda kuwapongeza sana DAWASCO kwa utaratibu huu mzuri sasa hebu tuelezen barabara ya Goba ya mbezi mnaleta maji lini?
Kule mtasubiri sana chimbeni visima vyenu milima utafikiri tupo nchi ya Rwanda bwana
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu yaliyo Jijini Dar es salaam , miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani pwani. DAWASCO inapokea maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Ndugu wana jukwaa, DAWASCO inajipambanua kwa kusimamia maadili ,kutoa huduma iliyotukuka pamoja na kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa kila mwananchi.

Kama kutatokea kuharibika kwa bomba, wizi wa Maji, umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: DAWASCO - Welcome to new site
2. Kupitia mitandao yetu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter|DawascoOfficial..Facebook|DawascoOfficial ...Instagram|DawascoOfficial
3. Kwa mwananchiposta ; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASCO
P. O. Box 5340
Sokoine Drive
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu huduma kwa wateja dawasco
0800110064 /022 2164800 ( Kupiga namba hizi ni Bure)
Salimia Mh Luhemeja kwa kazi nzuri ...
Mwambie amshauri Mkurugenzi wa Maji Moshi (Mama Msiru) kunaka muhaya pale kanaitwa 'Rujomba' katamuaribia kazi badala ya kufanya kazi amekuwa mtu wa Del del... !!! Amuweke kando mapema kabla hajamuaribia kazi..
 
Attention DAWASCO

Meneja wa DAWASCO Tabata namshauri atembelee eneo lake la kazi angalau mara 1 kwa miezi mitatu. Kule Tabata Kimanga, kuanzia Maji Chumvi, Kisukulu, Bonde la Mchicha (Kwa Mr Blue), hadi Tabata Reli mabomba yamechimbiwa juu juu yanapasuka kila uchao:
1. Kama unakaa Bonde la Mchicha na unapita Maji Chumvi, kuosha gari ni kujisumbua. Madimbwi makubwa ya maji kiasi cha kumeza gari hadi usawa wa radaitor.
2. Maji yanayotoka mabombani ni machafu. Kwa kuwa maji yanatoka kwa mgao, kila yanapokatika maji machafu ya madimbwini huingia kwenye mabomba na maji yanapokuja kutoka wananchi wanapata maji taka kabla ya maji safi hayajaanza kutoka...kwa hili mtatuletea maradhi.
3. Matope yaliyokithiri yasiyo na msimu ni kero kwa watembea kwa miguu. Watoto wa shule wanajichafua na hiyo mimaji michafu ya madimbwi.
4. Huu upotevu mkubwa wa maji ni zaidi ya hayo mnayoibiwa. Bomba kubwa linalovuja karibu na shule ya msingi Kisukulu ndio chanzo pekee kinachosupply mto wa jirani.

Ninayo hakika Dawasco Tabata wanaijua hali hii sababu mara kwa mara tunawaona mtaani na Kibajaj, wanafungafunga leo kesho hali ni ile ile. Kwa kifupi hii ni KERO KUBWA kufungua bomba yanakuja maji machafu yenye udongo na kuchafuliwa magari yetu. Haya mabomba yana mitaro mifupi sana.

Nimeliweka hili hadharani kwa kuwa ninalo kusudio la kulifikisha jambo hili kwa DC kama sitaona mabadiliko ninapofungua bomba kuchota maji na madimbwi yanayotuchafulia magari yetu.

Tafadhali ondoa kero hii kwa wakati.
 
Bili za maji mnaboa katika kudai, yan unakuta mwisho wa mwez bado, watenda kaz wanatumwa, wakifika ata kama mweeny nyumba hayupo mnataka kukata maji, house girl anapata wap pesa ya kulipia hayo maji
Kibaya zaid unakuta ni elfu kumi, na mwez haujaisha mnaboaga sana , hasa uku tabata kisiwani, yan mnaboa mnooo,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na Mimi naomba majibu kidogo lini mtareta maji maeneo ya Chamanzi Mbande na maeneo Jiran kwani idadi ya watu inaongezeka uko na lini mtawaletea maji wakazi hawa ili waondokane na kuuziwa maji na watu binafsi ambao wamechimba visima na hawajui usalama wa hayo maji? Au kipindu pindu kikiwa kinashamili ndo mtakuja?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Napenda kutangazia umma kuwa dawasco mnatuntanyasa naish ktk jengo lenye apartment kumi as mmoja wetu hajalipa bill zake yenye malimbikizo.sasa dawasco wameziba chemba ambayo inaathir jengo zima sasa kuna faida gan kulipa kwa wakat .dawasco mko humu tunaomba mrejesho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bili za maji mnaboa katika kudai, yan unakuta mwisho wa mwez bado, watenda kaz wanatumwa, wakifika ata kama mweeny nyumba hayupo mnataka kukata maji, house girl anapata wap pesa ya kulipia hayo maji
Kibaya zaid unakuta ni elfu kumi, na mwez haujaisha mnaboaga sana , hasa uku tabata kisiwani, yan mnaboa mnooo,

Sent using Jamii Forums mobile app
bili yako unaletewa kutokana na usomaji mita wa eneo lako. sio lazima usomewe mwisho wa mwezi inategemea na routine ya Msoma mita katika eneo Hilo. kwahiyo unavyosomewa mita na kutumiwa bili yako ndani ya siku 7 uwe umeshalipa huduma
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu yaliyo Jijini Dar es salaam , miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani pwani. DAWASCO inapokea maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Ndugu wana jukwaa, DAWASCO inajipambanua kwa kusimamia maadili ,kutoa huduma iliyotukuka pamoja na kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa kila mwananchi.

Kama kutatokea kuharibika kwa bomba, wizi wa Maji, umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: DAWASCO - Welcome to new site
2. Kupitia mitandao yetu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter|DawascoOfficial..Facebook|DawascoOfficial ...Instagram|DawascoOfficial
3. Kwa mwananchiposta ; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASCO
P. O. Box 5340
Sokoine Drive
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu huduma kwa wateja dawasco
0800110064 /022 2164800 ( Kupiga namba hizi ni Bure)
Tunaomba mlete mradi was maji ya mabomba Goba mpakani

Don't tress urself with knowing all answers to every question. Don't worry nobody will be clever enough to ask you
 
Nimelipa kuunganishiwa maji tokea tarehe 29/05/17 Kwa ajili ya kuunganishiwa maji. Lakini mpaka leo sijaunganishiwa, nimeenda DAWASCO Boko nimeambiwa hawana mipira ikiwa tayari watanipigia.
Kama mnajua kuwa mipira haitoshi kwanini mnawaambia wateja walipe??
tafadhali wasiliana nasi kupitia inbox kwa kutupa taarifa zako nasi tutazifanyia kazi
 
Kwanza napenda kuwapongeza sana DAWASCO kwa utaratibu huu mzuri sasa hebu tuelezen barabara ya Goba ya mbezi mnaleta maji lini?
watu wa DAWASCO walioweka hii threand nashindwa kuwaelewa manake naona kama wanachagua maswali ya kujibu hilo swali langu nililouliza hapo juu miezi kibao imepita halijajibiwa
 
Hongera,
Natuma pongez kwa meneja uhusiano dawasco baada ya kupata kero kutoka dawasco niliwasiliana nae kupitia humuhumu jamii forums na alinitatulia tatizo langu Siku hiyohiyo. hongera meneja uhusiano!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
bili yako unaletewa kutokana na usomaji mita wa eneo lako. sio lazima usomewe mwisho wa mwezi inategemea na routine ya Msoma mita katika eneo Hilo. kwahiyo unavyosomewa mita na kutumiwa bili yako ndani ya siku 7 uwe umeshalipa huduma

Sasa mteja anapokupa mrejesho kuwa huo utaratibu wenu unaleta usumbufu kwa nini msilichukue Hilo Na kwenda kulifanyia kazi ili Mje na convenient way ambayo itakuwa rafiki Kwa mteja? Hivi nyie mnafanya hizi kazi kwa weledi ? Can you execise respect and due care? Customernization, are after Customers? Modern mgt hufanya continues improvements, Vipi kuhusu nini? Je mnavyo viwango vya utoaji huduma na kupimwa na Watu huru kisha kutunukiwa Cheti?
 
Kule mtasubiri sana chimbeni visima vyenu milima utafikiri tupo nchi ya Rwanda bwana
Milima sio ishu. Mwanza kuna milima mikubwa lakini maji mpaka juu kilimani na yanatoka kila siku na cha kushangaza Mwanza uwezi kukuta Mabomba yamepasuka pasuka kama Dar es salaam tatizo menejimenti ya Dawasco imekaa kirushwa Rushwa tuu ndio maana Mh. Raisi alisema yule Mtalemwa wa Dawasco ajistaafishe mwenyewe pasipo serikali kumlazimisha kustaafu. Lakini nashangaaa kimiya mpaka Leo inamaana kaleta ukaidi kwa Mh. Raisi.

Aliaambiwa ajistaafishe mwenyewe amefanya kazi tokea Magufuli yupo Sekondari mpaka Leo hiii mzee hataki kuachia ofisi
 
Back
Top Bottom