DAWASA Mitaa ya Tabata Segerea kuna shida gani, Mbona hatupati Maji wiki ya tatu sasa?

Aug 31, 2022
54
99
Kuna mambo nchi hii yanachosha sana jamani, hebu fikiria Wiki tatu unakosa Maji ambayo unayalipia kila mwezi, ni utaratibu gani huu? Leo naomba kuwauliza Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) kuna shida gani katika jiji hili, mbona matatizo ya maji hayaishi? Mvua ziwepo zisiwepo shida ya maji haiishi huu mji sijui mnakwama wapi.

Hapa juzi kati mlisingizia Umeme kusumbua mkasema kutokuwepo kwa Umeme kumesababisha maeneo mengi kukosa Maji, kwasasa Umeme umetengemaa, haya tuambieni shida iko wapi tena?

Na cha ajabu tukienda ofisini pale Chama hakuna majibu ya kueleweka, mnaishia kusema tatizo linashughulikiwa, sasa tatizo gani linashughulikiwa wiki tatu? hao watumiaji Maji mnataka wawe katika hali gani? Hebu chukueni hatua zinazoeleweka na muwajibike muache kugombanisha Serikali na wananchi.


Soma DAWASA: Changamoto ya Umeme Mdogo imesababisha baadhi ya maeneo ya Dar kukosa Maji, maboresho yanaendelea
 
Sio Segerea tu, mitaa ya Bonyokwa Kisiwani hakuna maji miezi 2 sasa, na hakuna taarifa yoyote ya kibachoendelea. Wako busy tu kuja kusoma mita huku maji hakuna.
 
Huku Pugu mwezi wa pili huu hatuna maji, halafu kibaya zaidi, wanakaa kimya tu badala watuambie wateja wao tatizo nini na tuchukuwe hatua zapi. Wanatuona manyani tu!
 
Back
Top Bottom