Dawa ya Kuvuta Wateja kwenye Biashara Mpya

Dawa ya Kuvuta Wateja kwenye Biashara Mpya

Humu hakuna anayefanya/aliyefanya biashara kama hiyo ya mleta mada?
 
Nakusogeza kwenye mlango wa mkubwa wa ubaya mwenyewe,king Satan,angalia gereza kubwa maarufu,pale mlangoni,pachua kipande cha mbao ya mlango,kiweke kwenye lango lako la biashara,kingine weka kwenye droo,kwisha kazi,ulete ushuhuda hapa.🔥🔥🔥
-Ispofanyika kazi,tibu eneo lako.
 
ima yako itakuponya mkuu.

Lakufanya jifunze unversal laws.

sheria za ulimwengu ndo zinadeal na mambo hayo.

ila na dawa zipo unga vyote dawa na hizo sheria.
 
Habari wakuu. Nimekuja leo nikiwa na maswali mawili kuhusu biashara yangu mpya ya restaurant/mkahawa.


Swali la kwanza linahusu biashara yenyewe. Nimefungua restaurant wiki mbili zilizopita baada ya kuwahi kufanya biashara kama hii miaka kadhaa nyuma lakini sikufanikiwa sana. Safari hii nimerudi nikiwa na mtaji mkubwa, plan nzuri, usafi, na nidhamu ya biashara. Eneo nililopo lipo barabarani na kuna movement ya watu hasa asubuhi, mchana na usiku lakini bado faida na mauzo sio mazuri kama nilivyotarajia. Kwa sasa naisimamia mwenyewe muda wote kabla ya kuja kuweka meneja na pia nina mpango wa kufunga CCTV jikoni na maeneo ya mbele ili kudhibiti wizi, matumizi mabaya ya bidhaa, na kuongeza usimamizi wa kazi. Changamoto kubwa ninayoiona ni upande wa chipsi. Naomba msaada kwa wenye uzoefu, kilo 1 ya viazi inatakiwa kutoa sahani ngapi za chips kwa portion ya kawaida ya mjini? Nahisi huenda portion zangu ni kubwa sana ndio maana faida inakuwa ndogo. Ushauri wowote wa kuongeza faida na kuimarisha restaurant unakaribishwa.


Swali la pili linahusu kuvuta wateja. Naomba kujua ni vitu gani hasa vinafanya restaurant mpya kuvuta na kuhifadhi wateja wengi. Ukiachana na location, huduma, usafi, bei, matangazo, ubora wa chakula, maombi ya kuombea biashara, kwa maana haya yote nayafanya kwa asilimia 90-95%, au kuna mambo mengine muhimu zaidi? Pia kama kuna watu wanaoamini katika “dawa ya biashara” kuvuta wateja, naomba mnishauri kwa hekima na uzoefu wenu. Niko tayari kujifunza na kuboresha biashara yangu.
Njoo na fuvu la nyani aliy3kufa 9 Decemba 1961 na shillingi hiziii 5m. Nikufanyie kazi uone kazi.
 
Back
Top Bottom