Dawa ya Kuvuta Wateja kwenye Biashara Mpya

Dawa ya Kuvuta Wateja kwenye Biashara Mpya

I conquer with you! Ni kweli mama ntilie wengi utasikia wanatumia dawa, but miaka nenda rudi utamkuta palepale kwenye kakibanda chake with less capital growth or expansion...au ndo masharti yenyewe
tumia mgahawa kama daraja la kupush miradi mingine mkuu, faida inayopatikana ipeleke katika kilimo, kodi shamba nunua mbegu mbolea lima. mazao yatakayotoka huko yafanye kama mtaji wa kuanzisha mradi mwingine. Usikalili biashara ndugu. Naomba ujipange kiangazi hiki masika ikifika lima,utakapovuna na kuuza mazao yako uje urejee uzi huu na unikumbushe kuhusu komenti yangu hii. Mgahawa utumie kama daraja. Kila la kheri.
 
Asante kwa ushauri mkuu, kilimo nacho ni biashara ndugu maana kinahusisha mtaji na mauzo (mavuno) ili kupata faida.
 
chukua ushauri wote ila nakuapia pia ukiacha kwenda kwa waganga na wataalamu utashtuka tu biashara imedoda. Mjini ndipo kuna uchawi zaidi kuliko popote,unaweza ukawa na mwendelezo,sijui customer care,usafi,huduma nzuri lakini wateja wakakuhama na unakuwa unapata hasara kila siku,ndugu kama unataka ufanikiwe katika biashara yako tembelea kwa wataalamu,kama unahtaji tu mtaji wa kujishikiza na showoff kwamba na wewe una mgahawa basi usichoke kupiga maombi. MAFANIKIO HAYAJI KWA KUKATA TAMAA.
Hilo la wataalamu nataka kulifanyia kazi, shida inakuja nathibitishaje huyu ni mtaalamu wa kweli na sio kanjanja?
 
Asante kwa ushauri mkuu, kilimo nacho ni biashara ndugu maana kinahusisha mtaji na mauzo (mavuno) ili kupata faida.
mtaji ni mgahawa wako mkuu faida unaipeleka kwenye kilimo unafeli wapi?.
 
Habari wakuu. Nimekuja leo nikiwa na maswali mawili kuhusu biashara yangu mpya ya restaurant/mkahawa.


Swali la kwanza linahusu biashara yenyewe. Nimefungua restaurant wiki mbili zilizopita baada ya kuwahi kufanya biashara kama hii miaka kadhaa nyuma lakini sikufanikiwa sana. Safari hii nimerudi nikiwa na mtaji mkubwa, plan nzuri, usafi, na nidhamu ya biashara. Eneo nililopo lipo barabarani na kuna movement ya watu hasa asubuhi, mchana na usiku lakini bado faida na mauzo sio mazuri kama nilivyotarajia. Kwa sasa naisimamia mwenyewe muda wote kabla ya kuja kuweka meneja na pia nina mpango wa kufunga CCTV jikoni na maeneo ya mbele ili kudhibiti wizi, matumizi mabaya ya bidhaa, na kuongeza usimamizi wa kazi. Changamoto kubwa ninayoiona ni upande wa chipsi. Naomba msaada kwa wenye uzoefu, kilo 1 ya viazi inatakiwa kutoa sahani ngapi za chips kwa portion ya kawaida ya mjini? Nahisi huenda portion zangu ni kubwa sana ndio maana faida inakuwa ndogo. Ushauri wowote wa kuongeza faida na kuimarisha restaurant unakaribishwa.


Swali la pili linahusu kuvuta wateja. Naomba kujua ni vitu gani hasa vinafanya restaurant mpya kuvuta na kuhifadhi wateja wengi. Ukiachana na location, huduma, usafi, bei, matangazo, ubora wa chakula, maombi ya kuombea biashara, kwa maana haya yote nayafanya kwa asilimia 90-95%, au kuna mambo mengine muhimu zaidi? Pia kama kuna watu wanaoamini katika “dawa ya biashara” kuvuta wateja, naomba mnishauri kwa hekima na uzoefu wenu. Niko tayari kujifunza na kuboresha biashara yangu.
Acha kutusanifu hapa wewe. Nimeamini na naendelea kuamini kuwa watanzania wengi wana akili fupi sana na za kipumbavu kama zako. Karne ya 21 unafikiria dawa.....Kweli una wazimu wewe.
 
Humu kila mtu anasema usiende kwa mganga wakati wao biashara zao wanaroga kama kafara unaziweza nenda!

Humu kila mtu anasema usiende kwa mganga wakati wao biashara zao wanaroga kama kafara unaziweza nenda!
Kweli mkuu humu kila mtu anasema usiende kwa mganga!😂 Nipo tayari kwenda lakini mambo ya kafara sitayaweza ila kama ni dawa tu za kuvuta wateja bila kuathiri watu nipo tayari.
 
Acha kutusanifu hapa wewe. Nimeamini na naendelea kuamini kuwa watanzania wengi wana akili fupi sana na za kipumbavu kama zako. Karne ya 21 unafikiria dawa.....Kweli una wazimu wewe.
Mbona unatumia nguvu nyingi kuandika ndugu?
 
Kweli mkuu humu kila mtu anasema usiende kwa mganga!😂 Nipo tayari kwenda lakini mambo ya kafara sitayaweza ila kama ni dawa tu za kuvuta wateja bila kuathiri watu nipo tayari.
Kama kafara huwezi tulia! Mwanzoni utaambiwa leta vitu vidogo ukinogewa jiandae.
 
Back
Top Bottom