Dawa ya Kuvuta Wateja kwenye Biashara Mpya

Dawa ya Kuvuta Wateja kwenye Biashara Mpya

Kwq sababu umerudi mara ya pili unatakiwa uwe umefanya research ya kutosha.
Kwanza angalia wanaokuzunguka wanachaji bei gani hata kama mama ntilie kisha wewe weka bei ambayo mtu ataona kuliko kulia chakula kwenye benchi bora aje mgahawqni ale kwa heshima.
Ajili wapisho bora wanaojua kupila ikiwekana mmoja awe ametoka chuon8 kabisa, ukipika vizuri wateja ndio watakutangaza.
Customer care sio mteja anaingia anakaa muda mrefu hajasikilizwa pia wateja ni sawa, kuna wengine kutokana na nature ya kazi zao wako rough sasa watumishi wako wakianza kuhudumia wateja kwa mwonwko wao utapoteza pakubwa.
Ofa ya vitu vidogo nunua maji madogo yale ya mia tatu wape bure wateja au matunda ukifanya hivyo baadae faida utapata kubwa wakitaka ya kunujia uza kuanzia lita moja.
 
  • Hakikisha jikoni harufu ya nyama choma inashawishi wapita njia, kila bada ya dakika 20 dumbukiza futa lenye viungo kwenye moto ili utoke moshi wenye ladha kuwaita wateja waliopo mbali watakaonusa huo moshi.​
  • Lugha nzuri kwa wateja, mteja ni mfalme​
  • Anzisha posheni za kufunga, nyama choma ndizi.​
  • Wahudumu wawe wanavutia, na wawe wanatabasamu.​
 
Asante mkuu, hii nikikuwa naitafuta!
Kanuni ni mbili tu au nyingine moja ya 3

ya kwanza heshimu wateja wako wote yaan wote wape heshima kuanzia mtoto mdogo wa mwaka mmoja mpaka mzee wa miaka 100, nilishangaa sehemu fulani jamaa anauzia chips mpaka watoto wa shule yaan tule tuchips twa kuonja 200 200 anawapa na anacheka nao tu vizuri safi kabisa eeh ni customer service tu yaan na heshima kwa wateja haijalishi wana umri gani na huyo jamaa anauza magunia ya viazi kwa magunia kwenye ofisi yake ni magunia manne mpaka matano yanapaki naa yanaisha kwa siku sababu ya huduma nzuri na heshima kwa wateja

ya pili usifukuze wateja lugha mbaya dharau matusi kejeli kusema vibaya na kuwateta wateja usithubutu ukiwa ofisini kazi iwe ni kazi usiongee sana onyesha ubora wa huduma yako kwa vitendo zaidi sio maneno vitendo ndio iwe lugha yako, funga mdomo wako

ya tatu jali wateja wako uwe na contact safi package za delivery faster wenzio wana mpaka bodaboda walioendelea na kutanua biashara hua wanafanya delivery za mbali inapigwa simu tu inafungwa package safi anapewa bodaboda anapeleka mzigo na hio bodaboda inalipiwa kupeleka chakula, umeona bana
 
I conquer with you! Ni kweli mama ntilie wengi utasikia wanatumia dawa, but miaka nenda rudi utamkuta palepale kwenye kakibanda chake with less capital growth or expansion...au ndo masharti yenyewe 😁😎
Na bado ana tarehe zake za kurudi kwa mganga kwenda eti kuongeza dozi. Ndyo chain ya utumwa hiyo.
 
Kama yote hayo umefanikiwa kuyafanya basi dawa kubwa ambayo umebakiza hapo ni nyama ya ulimi...🤗
 
Weka mhudumu mwenye tako na uzuri wa sura na anayefahamu kuchangamsha wateja.
Hii sio bar mkuu sija-target wateja wa kiume pekee, hizo attributes zinaweza kunifanya nikose wateja wa kike maana watamuona kama threat....na hii biashara wateja wake wengi ni wa kike!
 
Weka mhudumu mwenye tako na uzuri wa sura na anayefahamu kuchangamsha wateja.
Hii sio bar mkuu sija-target wateja wa kiume pekee, hizo attributes zinaweza kunifanya nikose wateja wa kike maana watamuona kama threat....na hii biashara wateja wake wengi ni wa kike
Kama yote hayo umefanikiwa kuyafanya basi dawa kubwa ambayo umebakiza hapo ni nyama ya ulimi...🤗
Sawa kaka, hili nalo neno
 
sio kijana bali mdada tena mzuri
Kaka biashara ya chakula ni ya wateja wa jinsia zote, na kwa upande wa chips wanakula wote japo watoto wa kike ndo hula zaidi, kisaikolojia mwanamke akimzidi mwenzake uzuri yule mwingine huwa anam-treat kama threat, kwa lugha nyingine wanaweza kumkwepa especially wakiwa na mabwana wao hivyo nikakosa wateja bure.....so nafikiri hapo ni stick tu kwenye kijana mtanashati mwenye kauli nzuri na kuvutia wateja..... I stand to be corrected
 
Biashara ina mda gani? Mkuu

Endelea kuandaa chakula kizuri mkuu, mambo mazuri na faida zaidi inakuja

Inabidi usipate hasara ila kama unapata faida kidogo upo nafasi nzuri sana

Unanunua mahitaji yote na unalipa wafanyakazi na wewe unapata kidogo, endelea na biashara

Usafi,chakula kuzuri, huduma nzuri kwa wateja.. endelea mkuu

Endelea na maombi biashara zinahitaji sana maombi zaid, acha mambo ya waganga na kutafuta dawa za kuvuta wateja, mwambie M/Mungu akuletee wateja

Fanya na vitangazo vya hapa na palee

Kila la kheri mkuu
 

Chakula Ni Dawa Tosha,,Uvumilivu Tu Ndio Unahitajika Kwa Kuwa Biashara Ndio Inachomoza,,,Tengeneza Dawa Bora Yenye Ubora,,Kwenye Mazingira Bora Yenye Ubora,,Kutoka Kwa Watu Bora,,,Ili Uendelee Kutoa Dozi Bora,,Kwa Wateja Bora Pia.....
 
Habari wakuu. Nimekuja leo nikiwa na maswali mawili kuhusu biashara yangu mpya ya restaurant/mkahawa.


Swali la kwanza linahusu biashara yenyewe. Nimefungua restaurant wiki mbili zilizopita baada ya kuwahi kufanya biashara kama hii miaka kadhaa nyuma lakini sikufanikiwa sana. Safari hii nimerudi nikiwa na mtaji mkubwa, plan nzuri, usafi, na nidhamu ya biashara. Eneo nililopo lipo barabarani na kuna movement ya watu hasa asubuhi, mchana na usiku lakini bado faida na mauzo sio mazuri kama nilivyotarajia. Kwa sasa naisimamia mwenyewe muda wote kabla ya kuja kuweka meneja na pia nina mpango wa kufunga CCTV jikoni na maeneo ya mbele ili kudhibiti wizi, matumizi mabaya ya bidhaa, na kuongeza usimamizi wa kazi. Changamoto kubwa ninayoiona ni upande wa chipsi. Naomba msaada kwa wenye uzoefu, kilo 1 ya viazi inatakiwa kutoa sahani ngapi za chips kwa portion ya kawaida ya mjini? Nahisi huenda portion zangu ni kubwa sana ndio maana faida inakuwa ndogo. Ushauri wowote wa kuongeza faida na kuimarisha restaurant unakaribishwa.


Swali la pili linahusu kuvuta wateja. Naomba kujua ni vitu gani hasa vinafanya restaurant mpya kuvuta na kuhifadhi wateja wengi. Ukiachana na location, huduma, usafi, bei, matangazo, ubora wa chakula, maombi ya kuombea biashara, kwa maana haya yote nayafanya kwa asilimia 90-95%, au kuna mambo mengine muhimu zaidi? Pia kama kuna watu wanaoamini katika “dawa ya biashara” kuvuta wateja, naomba mnishauri kwa hekima na uzoefu wenu. Niko tayari kujifunza na kuboresha biashara yangu.
Usisubiri wateja waje wafuate maofisini na madukani kwao, mida ikikaribia tuma mtu akachukue order au chukua namba zao za simu pigia kila mmoja, hii inaweza kudouble biashara muda mfupi
 
Back
Top Bottom