Dawa kuacha pombe kuwasili Tanzania

Dawa kuacha pombe kuwasili Tanzania

Watu wengi ili waache walichokizoea ni hadi uwatenge na kitu hicho. Wasikione kabisa!
Kwangu ukinitenga na pombe siwezi kujua kama nimeacha au nimeishiwa tu.

Ndiyo maana nikiacha pombe lazima iwepo ndani nyumbani naiona kila siku.

Hapa nina Tequila, Scotch, Gin, wines, beers.

Nikiziona na kuzipita kila siku ndiyo najua nimeacha.

Nikiwa sina pombe ndani najiona kama nimeishiwa tu sijaacha mwenyewe.
 
Mh kula vizuri kaka ? Hapana ninachojua yeye ni rafiki yangu ,yeye ni mke wangu ,yeye ni mkaribu wangu no way naweza kusema bila kula vizuri atanisumbua ,yeye ni wangu na mimi ni wake .

Anyway uko wapi rafiki ? Sogea Strio hapa karibu na hospitali hii ,tupate vitu
Kaka itoshe kusema, yenyewe inapendana nawe, wewe unapendana nayo, yaani Mnapendana!
 
Kwangu ukinitenga na pombe siwezi kujua kama nimeacha au nimeishiwa tu.

Ndiyo maana nikiacha pombe lazima iwepo ndani nyumbani naiona kila siku.

Hapa nina Tequila, Scotch, Gin, wines, beers.

Nikiziona na kuzipita kila siku ndiyo najua nimeacha.

Nikiwa sina pombe ndani najiona kama nimeishiwa tu sijaacha mwenyewe.
Umenifundisha kitu kipya leo. Kwa hiyo ili ujiamini kabisa kuwa umekiacha kitu fulani unatakiwa uwe unakiona na unauwezo wa kukichukua, lakini hukichukui! 😂
 
Pombe unaacha tu.

Kama unavyomuacha mpenzi mbaya.

Kama unavyoacha social media yenye umbea.

Unatakiwa kuelewa kuwa wewe ndiye una control.

Dawa ya kuacha ipo kichwani mwako.

Usipoweza kutumia dawa hiyo, hizi nyingine zote zitashindwa tu.
Huu ndio ushaur mzurii na WA muda woteeeeeee naomba tufunge mjadala

Umemaliza Kila kitu.
 
Naam,

Ingawa naelewa pia wanaokataa kabisa kuwa nacho ili kujiondokea kishawishi.
Kuna jamaa mmoja pombe zime mletea shida ya ini na Figo ila alikua hatua za mwanzo mwanzo now kakaa miezi minne now naona karejea kwa kasii
 
Umenifundisha kitu kipya leo. Kwa hiyo ili ujiamini kabisa kuwa umekiacha kitu fulani unatakiwa uwe unakiona na unauwezo wa kukichukua, lakini hukichukui! 😂
Haaaha inaitaji Roho ngumu mtu mwingine hawezi ni kama kuona makebo waziwazi yamenona na kuyala kwa macho
 
Mimi ninahakika mtengenezaji mwakani hafiki atakuwa kabadilishwa jina marehemu
 
Mimi nakunywa Kila siku ila ni kwa kiasi Tu
Si kila mtu ana uwezo huo mkuu.

Kwa mfano, mimi ni mzuri sana katika kuacha kunywa kabisa.

Lakini nikiwa nakunywa, kunywa kwa kiasi ni vigumu. Halafu I have a high tolerance for alcohol kwa hiyo nakuwa nakunywa tu.

Yani kirahisi kabisa unaweza kunikuta on my third and fourth highland single malt double double.

Na kwa kujielewa hivyo, nikaamua kuacha kabisa. Kitu ninachoweza kufanya kwa urahisi kuliko kunywa kwa kiasi.
 
Pombe unaacha tu.

Kama unavyomuacha mpenzi mbaya.

Kama unavyoacha social media yenye umbea.

Unatakiwa kuelewa kuwa wewe ndiye una control.

Dawa ya kuacha ipo kichwani mwako.

Usipoweza kutumia dawa hiyo, hizi nyingine zote zitashindwa tu.
Ni kweli kabisa Mimi nilipumzika kunywa mwaka na miezi kadhaa.

Baada ya kupoteza begi lenye pesa nyingi tu ambazo hazikuwa zangu.

Kwanza kila nikiona bia nilikuwa nasisimkwa mwili Kwa hofu na uoga ,SITASAHAU

kwahiyo ukisema kuacha pombe hadi unywe dawa haiingii akilini
 
Pole sana mkuu. Sasa kesi ya kupoteza begi imeishaje?

Ila bora kupoteza pesa zinaweza kutafutwa tena, kuna watu wanapoteza uhai kwa sababu ya pombe.
 
Si kila mtu ana uwezo huo mkuu.

Kwa mfano, mimi ni mzuri sana katika kuacha kunywa kabisa.

Lakini nikiwa nakunywa, kunywa kwa kiasi ni vigumu. Halafu I have a high tolerance for alcohol kwa hiyo nakuwa nakunywa tu.

Yani kirahisi kabisa unaweza kunikuta on my third and fourth highland single malt double double.

Na kwa kujielewa hivyo, nikaamua kuacha kabisa. Kitu ninachoweza kufanya kwa urahisi kuliko kunywa kwa kiasi.
Bora umeacha huo unywaji ni mkubwa sanaa.

Mwingine anakunywa BIA yenye 2% alcohol anawehuka.. vichwa vinapishana
 
Pole sana mkuu. Sasa kesi ya kupoteza begi imeishaje?

Ila bora kupoteza pesa zinaweza kutafutwa tena, kuna watu wanapoteza uhai kwa sababu ya pombe.
Hakukuwa na namna zaidi ya kuomba muda na kulipa Kwa awamu 54 millions siyo rahisi,Kwanza sikusema nimepoteza ningeonekana mzembe na kupata aibu zaidi ,nilisingizia wife kaingiza Ile pesa kwenye biashara yetu.

Nilieleweka japo kuna watu muhimu niliwapoteza kwani waliamini mke wangu ananicontrol si unajua baadhi ya makabila hapa Nchini hawapendi mtu anayeongozwa na ke
 
Back
Top Bottom