Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 17,305
- 26,815
Fursa ya wastaafu wenye mafao wasiojua la kufanya kufungua maduka ya kuuza dawa ya kuacha pombe pembezoni mwa Baa kubwa.
Pia kwenye vituo vya daladala kama Bifara ambapo wanauza pombe zote na bange, morroco na sehemu nyingine hizi awa ziwepo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Grace Magembe, ameiagiza Bohari ya Dawa (MSD) kuharakisha mchakato wa upatikanaji wa dawa ya Naltrexone inayotibu uraibu wa pombe na kuhakikisha inasambazwa nchini kabla ya mwisho wa mwezi Septemba 2026.
Akizungumza jijini Dodoma katika mafunzo ya siku tatu ya matumizi sahihi ya dawa hiyo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Afya ya Akili Tanzania (TMHI), Dkt. Magembe amesisitiza kuwa unywaji wa pombe kupindukia unachangia kwa kiasi kikubwa matatizo ya afya ya akili, ukatili, migogoro ya familia na ajali za barabarani.
Akitolea ufafanuzi agizo hilo, Msimamizi wa Dawati la Wateja Wakubwa wa MSD, Mfamasia Michael Bajile, amethibitisha kuwa mchakato wa zabuni ya ununuzi wa Naltrexone umeshakamilika.
Amehakikisha kuwa dawa hiyo itaingia nchini ndani ya mwezi huu wa Septemba na kusambazwa mara moja TMHI kulingana na mahitaji, ili kuwezesha huduma hiyo kuanza kutolewa bila kukwama.
Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo na uelewa wa kisayansi wataalamu wa afya na wadau wa TMHI juu ya matumizi sahihi na salama ya Naltrexone.
Hatua hii inalenga kuimarisha huduma za matibabu kwa watu wanaokabiliwa na changamoto ya uraibu wa pombe (Alcohol Use Disorder) na kurejesha ustawi wa jamii.