Sawa bro , sasa kipi kimekufanya useme ya kuwa wachangiaji humu JF na magazeti yalikuwa biased, umeona na kuisoma hukumu na mwenendo wa kesi?Au you referring to what stand point to conclude hao watu walikuwa biased?
Sawa, comrade, umekuwa very king'ang'anizi (nadhani kwa nia njema) kwa suala hili ili kufahamu kwa nini nasema walikuwa biased. Nakujibu in short: Namna walivyokuwa wakiripoti walikuwa biased kwa kuwa walikuwa wanachukua habari au angle ya stori inayoonekana kumpendelea mtu mmoja tu...hata headlines zilikuwa zinamtaja huyo tu, na wengine ndani ya JF walifikia hata kuaminishwa kuwa huyo mtu angeshinda na wakawa wanasema kweli atashinda...Uandishi wa aina hiyo ni mbaya na haufai...mimi niliwaonya humu katika baadhi ya comments zangu kuwa wasiandike hivyo kwani wanaingilia uhuru wa mahakama, baadhi wakanishambulia kwa maneno ya matusi na kejeli....