Darasa la saba aukwaa u-DC

Darasa la saba aukwaa u-DC

Hatakuwa DC wa kwanza wa darasa la saba. JK aliishamteua mwingine anaitwa Hawa Ngulume. Alivurunda kila mahali alipopelekwa mwishowe akamtema.
 
ndugu wana jamii katika kile kinachoonekana kulipana fadhila ndani ya serikali hii, aliyekuwa mbunge wa chalinze 2005-2010 ramadhani a maneno, alishindwa vibaya kwenye kura za maoni mwaka 2010 baada ya kuwadanganya wapiga kura wake kwamba angejiendeleza kielimu,na hakufanya hivyo, mpaka anateuliwa mkuu wa wilaya ya kigoma elimu yake ni darasa la saba_____________tafakari.
darasa la mtu si hoja katika ngzi fulani za uongozi kama ma dc wa bongo wanakazi gani zaidi ya kutimiza yale aliyoagizwa,unahitaji gigrii kuwa dc wa serikali ya ccm? Kuna kazi awapo wilayani wakati mkurugenzi ndiye mtaalam wa mipangoi ya maendeleo ya ccm
 
inaweza ikawa ni kuwadhihirishia wale wanaosema kuwa DC sio kazi ya kuwagharimu walipa kodi. Na kizuri zaidi safari hii imeeleweka zaidi kuwa ni wawakilishi wa CCM na wala sio wananchi kwa ujumla wao.

Kibaya zaidi ni kuwa hii tume ya Katiba imeshaanza kuleta mashka mashaka na huenda katika mapendekezo yao wasikifute hiki cheo!


Lukindo ninakuunga mkono. Watanzania wapenda maendeleo ya kweli tuungane kwa nguvu zetu zote kutoa maoni yetu wakati wa mchakato wa katiba mpya - hiki cheo kifutwe kabisa. Ni upotezaji mkubwa wa pesa za walipakodi. Hawa jamaa ni makamisaa wa CCM. Hata chama kingine kikiingia madarakani mwendelezo utakuwa ni huo huo wa kuweka makamisaa wa chama tawala. Hakina maana yo yote, hakina faida yo yote. Ninawashangaa hata watu wenye taaluma zao nzuri kama Mhe Dr. Kadeghe au Dr. Mwenegoha kukubali kudhalilishwa kwa kupewa kazi ambayo hata darasa la saba anaweza kuifanya - ushahidi kuwa ni kazi ya porojo na kulinda maslahi ya watawala wakuu :frown::A S confused:
 
Mbona wabunge wengi darasa la saba? Kiona Lusinde, na yule wa Rorya nimemsahau jina!
 
Hakuna akifanyacho JK kikakosa usanii ndani yake!
 
Hivi hawa wasomi wetu tunaojitapa nao wamelisaidiaje Taifa letu?

Wametumiwa lini wakaacha kulisaidia taifa. Acheni kutoa mifano ya kina Balali, Chenge, Maige na wengine ilihali mkijiua hawakupewa kazi bali siasa ziliwapa nafasi. Embu kipeni chama makini nchi muone hao wasomi watakavyoonekana
 
Huyu jamaa alimaliza degree ya social works mwaka 2010 pale chuo cha ustawi. Tuandike vitu baada ya kufanya utafiti. Sio kila mtu aliyeteuliwa hana uwezo. Au ulitaka uteukiwe wewe.

siyo degree mkuu alimaliza diploma pale CBE hata magazeti yalipublish nnayo nakala hapa ya mwananchi!
 
Wakuu msimuonee huyu jamaa, sasa hivi RC mna DC hawana kazi kabisa, kwani kazi ya kubuni maendeleo na shughuli za maendeleo ziko chini ya halmashauri. Kingine haya hebu tutazame wasomi wamefanya nini cha ajabu? mifano mizuri Pro Kapuya, ni kipi amekifanya tangu amekuwa waziri ambacho unaweza kusema ni kumbukumbu katika uongozi uliotukuka? au kuwapeleka wale makaburu Tanesco kwa escort ya FFU? na sasa mbona hampigi kelel kwa LUKUVI? si mwalimu wa shule ya msingi huyu jamaa?
 
hilo halina ubishi huyu juha namfahamu vizuri mno mtoto wa magomeni mapipa kwa bi mjumbe ambaye ni mamayake mzazi hana elimu yoyote ilikuwa kila siku yuko kijiweni maskani pale mapipa kwa shoeshine paschal... hata kuandika jina lake ni kazi labda siku za karibuni kajifunza kuandika... huyu jamaa ni mkwele na ni raiki mkubwa wa jk kabla ya jk kuwa mheshimiwa sana,, ni mtaaramu wa dili za sangoma,, yeye kuwa mkuu wa wilaya ni Fadhila za baba riz1 kwani jamaa amefanya kazi sana ya kutafuta waganga. huyu jamaa hawafai kwa lolote huko mwisho wa reli hata mwanzo wa reli. yaani kwa hilo nimezidi kumdharaau jk,,, kuchagua jitu jinga kama hili.
 
Ndugu wana jamii katika kile kinachoonekana kulipana fadhila ndani ya serikali hii, aliyekuwa mbunge wa chalinze 2005-2010 RAMADHANI A MANENO, alishindwa vibaya kwenye kura za maoni mwaka 2010 baada ya kuwadanganya wapiga kura wake kwamba angejiendeleza kielimu,na hakufanya hivyo, mpaka anateuliwa mkuu wa wilaya ya KIGOMA elimu yake ni DARASA LA SABA_____________TAFAKARI.

kwani kusimamia watu wakalime badala ya kulewa mchana inahitaji degree?
 
Ndugu wana jamii katika kile kinachoonekana kulipana fadhila ndani ya serikali hii, aliyekuwa mbunge wa chalinze 2005-2010 RAMADHANI A MANENO, alishindwa vibaya kwenye kura za maoni mwaka 2010 baada ya kuwadanganya wapiga kura wake kwamba angejiendeleza kielimu,na hakufanya hivyo, mpaka anateuliwa mkuu wa wilaya ya KIGOMA elimu yake ni DARASA LA SABA_____________TAFAKARI.

Kwani yule mgombea mwenza wetu 2010 alikuwa darasa la ngapi? maana huyu ndio alitakiwa awe Raisi kama Dr angeshinda Uraisi na kwa bahati mbaya akapitiwa na Fardhi A'in.!!!
 
wapendwa,

mh Maneno namfahamu personally.

siyo kweli kuwa ni darasa la saba. nilikutana naye na kumfahamu akiwa mbunge wa chalinze na nilithibitisha kuwa wakati huo alikuwa pia akisona chuo cha ustawi wa jamii akichukua bachelor of HRM na alimaliza masomo yake mwaka 2009. ningemwelewa mleta hoaj kama angesema kuwa hakumaliza chuo kwa sababu yoyote ile. ila ile tu kupata adfmission choni ni wazi alikuwa na quolifications za kujiunga na chuo ambazo ni form six or equivalent. yeye aliingia ISW kwa hiyo diploma ya CBE amabayo inakubalika

nachukua fursa hii kumpongeza mh maneno kwa kuteuliwa kuwa mkuu mpya wa wilaya ya kigoma. kuteuliwa kwake katika nafasi hii muhimu ni matunda ya juhudi zake za kujiendeleza bila kukata tamaa licha ya majukumu makubwa ya kibunge aliyokuwa nayo na ni uthibitisho wa imani aliyonayo mh rais j. kikwete kwake binafsi. napenda kuchukua fursa nyingine kumtakia kila la heri katika utekelezaji wa majukumu yake mapya na naamini kabisa kuwa atafanikiwa kusukuma mbele gurudumu ola maendeleo akishirikiana na wananchi wa kigoma.

nawatakia majadiliano mema

Ni kweli kabisa jamaa ana bachelor degree ni social work kwa tuwe tunaandika vitu tulivyo na uhakika.

ni HRM mpendwa

sina uhakika na uwezo wake wa kuongoza lkn kuhusu chuo Ni kweli kabisa jamaa ana bachelor degree ni social work na sio darasa la saba tuache upotoshaji kwa hyo tuwe tunaandika vitu tulivyo na uhakika.

siyo social work, ni HRM mpendwa

siyo degree mkuu alimaliza diploma pale CBE hata magazeti yalipublish nnayo nakala hapa ya mwananchi!

hiyo diploma ya CBE ndiyo entry qualification aliyoingilia institute of social work kusomea bachelor of HRM

mbarikiwe sana wapendwa,

Glory to God!
 
Ndugu wana jamii katika kile kinachoonekana kulipana fadhila ndani ya serikali hii, aliyekuwa mbunge wa chalinze 2005-2010 RAMADHANI A MANENO, alishindwa vibaya kwenye kura za maoni mwaka 2010 baada ya kuwadanganya wapiga kura wake kwamba angejiendeleza kielimu,na hakufanya hivyo, mpaka anateuliwa mkuu wa wilaya ya KIGOMA elimu yake ni DARASA LA SABA_____________TAFAKARI.


Kwenye chama mbona wako wengi sana na hata wengine hilo la saba hawana wamejaliwa kuongea tu. CCM mtaji wake ni wa wajinga
 
Ndo maana amepelekwa KIGOMA,,,,,NO CHALLENGES OVA THERE
Weee, jamaa ni wabishi kule balaa...

Wasiwasi wangu jamaa anaweza kugoma kuhamasisha ujenzi wa shule za sekondari kwa kuona wivu watoto watamzidi elimu.
 
mhhh. kazi kwelikweli, kama ni darasa la 7 kwelikweli atakuwa hata ung'eng'e haupandi! na ikitokea wakija wageni kutembelea wilaya yake kutoka ng'ambo atakuwa anawakimbia kama mshikaji wangu fulani ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri na ni standard 7 lever anapatashida sana wakija wageni lazima atakula kona na kumwachia kazi makamu mwenyekiti wa halmashauri ambaye ni form 4 amsaidie kazi
penye red hayo ni mawazo mfu hivi mtu akiongea kingereza ndo msomi?kwa hiyo wale chokaraa wa mitaani uganda wanaongea kiingereza nao ni wasomi?
 
No efficiency argument in politics, as long as you are a true core member and loyal to the regime that is most important qualification for the inside posts.
 
mhe. kanyunyu una hakika na ulichokiandika? bw. maneno alikuwa mbunge wa jimbo la chalinze katika bunge lililopita na minimum qualification ya ubunge ni elimu ya kidato cha nne, ni vipi angeukwaa ubunge bila kuwa na elimu hiyo. kumbuka huyu aligombea na omary madega kwenye kura za maoni ndani ya ccm mwaka 2005 ambaye kwa vyovyote asingenyamaza angemlipua tu maneno kama kweli ni darasa la saba. bunge lililopita mbunge pekee aliyefahamika kutokuwa na elimu ya kidato cha nne ni samwel chitalilo aliyekuwa mbunge wa buchosa. wapiga kura walimfungulia kesi ya kudanganya kuhusu elimu yake lakini kwasababu ambazo hazijulikani kesi hiyo haikufanikiwa.

Sidhani ni hivyo, kwa sasa yupo Jah People wa Njombe na Prof. wa tiba za asili Maji Marefu. Sifa ni kujua kusoma na kuandika kiswahili au kiiigereza if I m not wrong
 
Back
Top Bottom