Darasa la saba aukwaa u-DC

Darasa la saba aukwaa u-DC

Je katiba inasemaje kuhusu vigezo vya kuwa mkuu wa wilaya, yawezekana elimu ni kuanzia darasa la saba ndio maana kuna wa darasa la saba mpaka maphd holder.
 
Issue ni kuwa ataweza mudu changamoto za kizazi iki?na elimu yake iyo?
 
.

Utasikia akijisifia darasa la saba la mkoloni equivalent to form Six ya sasa.

inawezekana ikawa kweli fanya utafiti ..hebu fikiria mtu yupo form one lakini hawezi kusoma na kuandika kwa ufasaha...hata wenye digree hawawezi kujieleza kwa mambo ya kawaida tu kwa kiingereza hii nimeiona mwenyewe kwenye michujo ya baadhi ya enteview kwa mfano mtu anulizwa umetoka wapi? kuja hapa anasema nimetoka mwanza swali lingine lina kuja hivi ............explain your journey from mwanza to dar
unatamani umpige

 
tanzania haijalish unajua nin bali unamjua nan. Kwa sasa ukijikomba na ccm hakuna kitakachoshndkana mkuu
 
Darasa la saba ni Elimu tosha kabisa, tupo wengi tu wenye Elimu hiyo na mambo yanakwenda. Tuache ubaguzi, kwani kazi ya Mkuu wa Wilaya ni nini?
 
Sidahni kama ni darasa la saba........kabla ya ubunge alikuwa ofisa TRA......Sidhani pia kama TRA bado in maofisa darasa la saba
 
Who cares?. Katiba mpya itawafuta hawa. CDM 2015 ndio hiyoooooo
 
mhe. kanyunyu una hakika na ulichokiandika? bw. maneno alikuwa mbunge wa jimbo la chalinze katika bunge lililopita na minimum qualification ya ubunge ni elimu ya kidato cha nne, ni vipi angeukwaa ubunge bila kuwa na elimu hiyo. kumbuka huyu aligombea na omary madega kwenye kura za maoni ndani ya ccm mwaka 2005 ambaye kwa vyovyote asingenyamaza angemlipua tu maneno kama kweli ni darasa la saba. bunge lililopita mbunge pekee aliyefahamika kutokuwa na elimu ya kidato cha nne ni samwel chitalilo aliyekuwa mbunge wa buchosa. wapiga kura walimfungulia kesi ya kudanganya kuhusu elimu yake lakini kwasababu ambazo hazijulikani kesi hiyo haikufanikiwa.
 
Sioni kama kuna tatizo hapo! Huenda akafanya vizuri kuliko ambao ni graduates.
 
Mbona mgombea umakamu wa Rais kwa tiketi ya Chadema mwaka 2010 alikuwa darasa la saba?.
.
"MADARAKA HUMBADILISHA MTU, YAPATE KWANZA NDIPO TUJUE TABIA YAKO".

nanii na udokta wake wa atomic anafanya nini? Si ndio maana hata nanii alimshauri awe anafundisha kule nanii? So umakamu si ishu
 
Ndugu wana jamii katika kile kinachoonekana kulipana fadhila ndani ya serikali hii, aliyekuwa mbunge wa chalinze 2005-2010 RAMADHANI A MANENO, alishindwa vibaya kwenye kura za maoni mwaka 2010 baada ya kuwadanganya wapiga kura wake kwamba angejiendeleza kielimu,na hakufanya hivyo, mpaka anateuliwa mkuu wa wilaya ya KIGOMA elimu yake ni DARASA LA SABA_____________TAFAKARI.

JK and Pinda janga la kitaifa, mpaka waondoke 2015 Taifa litakuwa maiti!!! Wanapanda mbegu mbaya sana kwa watawala wajao. Ukabila, udini etc unadhani watu hawaoni wanayoyafanya. Kesho wakinena kuhusu ukabila nani atawasikiliza. Yangu macho!!
 
Cha ajabu kipi hapo! aliweza kazi kawawa ambae aliishia darasa la NNE , na leo hii ni MFANO WA KUIGWA kwa kipengele cha watu wasio mafisadi SISEMI mengine ambayo sikuyapenda kutoka kwake ! itakuwa huyu wa darasa la saba! hebu acheni majungu yenu!
 
mhhh. kazi kwelikweli, kama ni darasa la 7 kwelikweli atakuwa hata ung'eng'e haupandi! na ikitokea wakija wageni kutembelea wilaya yake kutoka ng'ambo atakuwa anawakimbia kama mshikaji wangu fulani ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri na ni standard 7 lever anapatashida sana wakija wageni lazima atakula kona na kumwachia kazi makamu mwenyekiti wa halmashauri ambaye ni form 4 amsaidie kazi


Yes no............... Yes no......You know hahhhaha ...yes......... yah yah nyingiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii kumbe yai bovu.

Kwenye Red: Hivi wote ni form four au unawaonea tu.
 
Huyo ndo JK bana

Jakaya mambo yake yote ni ya mzaha mzaha tu kama alivyosema Lipunba the GUY has never been serious in his life kila kitu ni UPEPO WA KUPITA!! What a loss to my country! Imagine huyu Maneno kwanza ndio alikuwa kampeni meneja wake wakati akiwa mbunge wa Chalinze halafu akaja muachia Ubunge na sasa kabla ya kumaliza muhula wake anamhonga na uDC; haya ni matusi kwa ccm na nchi nzima.
 
Kwani kuna kazi gani ya kumshinda darasa la saba. Hiyo kazi ataiweza. Sijui in job description?

tatizo sio kazi kumshinda nijinsi atakavyo ifanya hiyo kazi kunatofauti kubwa ya msomi na mtu ambaye shule imempitia mbali utendaji wakazi waweza kua mbovu. msomi utamuona ata jinsi anavyoonge tu, shule inasaidia sana kaka.
 
Mimi siangalii mtu kasoma mpaka level gani..ninachoangalia ni ufanisi wa kazi wa mtu na sio elimu. Kuna watu wana busara na akili ya mwongozo au kibiashara na hata darasa la pili hawakumaliza. Mfano mzuri angalia baraza letu la mawaziri...lina madaktari na ma profesa...lakini angalia ufanisi wao wa kazi...utumbo mtupu... tatizo la bongo tunaona kua dr ndio mwisho wa kila kitu...kuna watu wana akili za darasani lakini hawana akili za maisha..huyu jamaa anaweza akafanya kazi huko kigoma mkashangaa.. hao wanaojua english na hata kifaransa wameifikisha wapi hii nchi...
 
U dc ni upambe wa kisiasa kwa hiyo la saba inatosha kama vile kuwa shabiki wa simba au yanga
 
Back
Top Bottom