Kama haya ni malalamiko ya Jaji Ibrahim; na kama anaona hawezi kufanya kazi kwa weledi kwa vile anachelewa kuthibitishwa au uwezekano wa kuteuliwa mtu mwingine unaweza kumvuruga mbona si lazima awe Kaimu Jaji Mkuu; anaweza kabisa kumuomba Rais ajiuzulu ili Rais ateue mtu mwingine. Hivi, kwanini unafikiria Jaji Ibrahim na weledi wake wote ni mtu petty sana kuhusu hivi vyeo?
Umepewa hoja zote za kwa sababu gani haipendezi mtu kuwa Kaimu Jaji Mkuu kwa muda wote huo na mtu kama
Pascal Mayalla amekutajia hadi sababu za msingi zinazoweza kumfanya Rais kuteua Kaimu Jaji Mkuu!!
Yote hayo huyataki!!!
Now your turn: Toa sababu moja tu ya msingi yenye busara ndani yake kwanini mtu awe Kaimu Jaji Mkuu muda wote huo!!! Sababu inaweza kuwa na uhalali wa kisiasa au hata kijamii... JUST ONE!
Usituambaie masuala ya kuvunja au kutovunja katiba kwa sababu JPM hana moral authority linapokuja suala la ulindaji wa katiba!!!
Isitoshe, hakuna anayesema JPM amevunja katiba kwenye hilo... sana sana watu wanailaumu katiba kutoa loophole ya Rais kuweza kukaa hata miaka 5 madarakani huku Mahakama ikiongozwa na Kaimu Jaji Mkuu kwa miaka yote hiyo!
Na hivyo, kwa sababu nilizotaja mwanzoni... Rais anaweza kubadilisha Kaimu Jaji Mkuu mara nyingi apendavyo bila kuwapo kwa legal argument kwamba Rais anavunja sheria!!!
Or else, labda ukiri kwamba Rais anatumia ana-take advantage ya mapungufu ya katiba kufanya vile anavyotaka yeye na hivyo kuthibitisha ile kauli ya Hayati Baba wa Taifa kwamba "Katiba hii inampa rais nguvu ya kuwa dikteta!"
Btw, mwanzoni nilikutajia watu walioyakana yale waliyokuwa wanayasimamia hapo mwanzoni kwa sababu tu ya madaraka na nikahitimisha kwamba, unless huyo Ibrahim ni very exceptional lakini nae hana tofaauti yoyote na akina Polepole, Mwakyembe, Kitila Mkumbo na wengine kahaa!!!
Kwavile umehoji kwanini watu waamini Ibrahimu anaweza kuwa cheap guy!! Jibu ni kwamba we make judgement basing on past experience or else, tuambie hapa ni nini kinachomfanya Profesa Ibrahimu awe so exceptional!
I hope post hii utaijibu kwa sababu una kawaida ya kuzikimbia baadhi ya post(hoja) though unaweza kuwa na sababu inayokubalika kwamba "...huwezi kujibu kila post!" hata kama utakuwa unafanya hivyo kwa kusukumwa na jambo lingine!!!