Darasa la Prof. Kabudi Halikuwa la Lazima!

Darasa la Prof. Kabudi Halikuwa la Lazima!

Prof Kabudi amejibu kuwa Rais Nyerere alifanya hivyo pia! Niliposikia hilo jibu nikajua siasa si mchezo, na sikuamini nilichosikia

Lakini, hata kama Nyerere atatumika kama 'template' bado kuna hoja. Mwl alieleza kwanini alichukua muda kumteua Jaji mkuu. Mwl alikuwa na presidential prerogative ya kumwacha Jaji mzungu. Kwa busara za wakati hakutumia prerogative hiyo kiholela
Aliitumia kwenda kutafuta Jaji kutoka Commonwealth kwa spirit ya matumizi sahihi ya prerogative. Leo Prof na MM hawana jibu kwanini nafasi hiyo nyeti ikaimiwe miezi 5 Nimekubaliana naye kwa sheria kutovunjwa, nimekubaliana naye kwa ''prerogative power''.

Hivi unakumbuka ni lini na kwa njia ipi Nyerere alitoa maelezo ya kuchelewesha uteuzi wa jaji mwafrika baada ya Jaji Ralph Windham?

Nisichokubaliana naye ni matumizi ya prerogative.
Prerogative iliwekwa makusudi ili kumpa uwezo wa kutenda ndani ya Busara

Rais ana prerogative ya kuteua wabunge 10. Kwa kutambua anaweza ku misuse prerogative, sheria ikasema wawepo makundi kadhaa.

Hapa busara zimetumika kuhakikisha Rais kwa jinsia yoyote hatatimiza masharti bila busara

Niliwahi kujadili, katika wabunge 10 Rais anaweza kuteua wote kutoka kwa familia yake na bado hajavunja sheria. Atakuwa ametumia prerogative, lakini je, busara za hilo zina impact gani na ni kwa national interest?

Prerogative ya kuteua kaimu Jaji mkuu ipo, lakini kama zingine imewekewa uzio na sababu zake. Haipo wazi tu kama MM anavyodhani, na asivyoweza kueleza jamvi kama alivyofeli Prof Kabudi

Unaweza usikubaliane na prerogative ya Rais lakini hiyo haiondoi kuwa anayo. Na suala la hekima; ni yeye anayejua hasa kwanini hadi hivi sasa Prof. Ibrahim anakaimu na inawezekana ni hekima hiyo hiyo inayomfanya kuchelewa kuteua mtu wa kudumu.

Ikitokea sababu muhimu nje ya zilizoanishwa kama ya Mwl, umma una haki ya kujua.

Hapo ndipo hoja ya Lissu si kuwa inapata miguu bali inatembea bila kupingwa.
Kabudi hakuweza, MM hadi sasa hajaweza. Pengine anajipanga tumpe muda

Binafsi sijaona sababu ya kwanini atoe maelezo ya kwanini amechelewa kuteua kana kwamba ana muda anaotakiwa awe ameteua! Sasa aelezee nini wakati hakuna sababu ya kuelezea. Kama kuna jambo fulani ambalo lilitakiwa lifanywe na Jaji Mkuu na haliwezi kufanyka na watu wanataka lifanyike basi wanaweza kutaka kujua kwanini hakuna Jaji Mkuu na hapo tunaweza kuuliza Ikulu itoe maelezo na yenyewe bila ya shaka kwa hekima ile ile inaweza kutoa taarifa kwa umma. Sasa hivi sijajua ni kitu gani hasa ambacho kinamhitaji Jaji Mkuu kwa haraka hivyo?

Wapinzani walitoa hoja ya kujadili hali ya usalama wa Taifa.
CCM-wabunge kwa kuelewa mhimili huo nao 'unakaimiwa' wakakataa
Siku tatu baadaye, CCM hao hao wakataka ijadiliwe baada ya matatizo Kibiti

Hii ni hoja nyingine na inahusiana na CCM; sijaona lolote la kushangaza kwa kinachofanywa na wabunge wa CCM. Hii si mara ya kwanza kwao kukwepa kuzungumzia mambo ya msingi au ya muhimu. Au umesahau wakati wa masuala ya wabunge kukamatwa? au hata masuala ya uhaba wa chakula? Kuna partisan politics wakati wote.


Juzi wakati Prof Kabudi anajikanyaga kanyaga walikuwa wanapiga makofi.

Leo ukiwauliza kwanini nafasi hiyo ikaimiwe kwa muda mrefu hakuna anayeweza kueleza, afadhali ya Prof Kabudi alijihifadhi kwa Nyerere, MM anatumia prerogative

La hasha sijatumia prerogative; naona unaweka mkazo sana kwenye hili. Hii ni sehemu moja tu ya hoja yangu isome vizuri. Hoja ni kuwa Rais yuko huru kisheria na Kikatiba kukaimisha nafasi ya Jaji Mkuu na kuijaza kwa wakati muafaka kwa kadiri ambavyo anaona inafaa. Nje ya hapo ni kutengeneza undue duress kwa Rais.


Kuna kiongozi aliteuliwa kwa prerogative, akapitishwa na chama kwa prerogative, na akachaguliwa katika taasisi nyeti kwa prerogative.

Matatizo ya taasisi ni kutokana na kiongozi kufanya kazi kwa 'fadhila' za prerogative

Masuala ya kitaifa yanajadiliwa akitazama 'prerogative' iliyomfikisha hapo. Tunafeli sote

Watu wengi wasichokiona ni umuhimu wa mhimili wa sheria.
Mhimili huo unapopoteza nguvu zake za asili ni hatari

Uchaguzi wa TLS uliingiliwa na serikali, tukasikia kauli zenye mwelekeo wa 'kisiasa'
Pengine hii ni katika kuonyesha misuli ya ''mhimili uliozama zaidi kwenda chini''

Swali, je, hayo ni kwa public interest au ni kwa interest ya mtu au watu?

Hizi ni hoja nyingine; irrelevant kwenye hoja hii.
 
Kama haya ni malalamiko ya Jaji Ibrahim; na kama anaona hawezi kufanya kazi kwa weledi kwa vile anachelewa kuthibitishwa au uwezekano wa kuteuliwa mtu mwingine unaweza kumvuruga mbona si lazima awe Kaimu Jaji Mkuu; anaweza kabisa kumuomba Rais ajiuzulu ili Rais ateue mtu mwingine. Hivi, kwanini unafikiria Jaji Ibrahim na weledi wake wote ni mtu petty sana kuhusu hivi vyeo?



Umejuaje kama Prof. Ibrahim ni mtu wa namna hiyo? kwamba siyo professional enough kuweza kusimamia kiapo chake kwa muda wote ambao anakaimu cheo hicho?

Still argument yako iko based na assumption kuwa kila mteule ni mkamilifu na asiyeyumbishwa!Ngoja nikupe mfano mmoja tu mwepesi,Nape ametumbuliwa kwa kusimamia anachokiamini!Huyu alitendea haki kiapo chake kwenye jambo husika japo aliyemteua hakupendezwa,akamuweka kando!Kabla hata ya kutumbuliwa Nape aliona na akasema anajua gharama ya anachokisimamia!Yuko wapi?Ni mawaziri wangapi wangekuwa tayari kutumbuliwa kusimamia wanachokiamini?Polepole aliupinga sana ukuu wa wilaya mpaka akapendekeza ufutwe kwani kumejaa ukada,alipoteuliwa yeye akanywea!Hii ni mifano tu kuwa madaraka yananoga,hata kama Jaji Mkuu anaona hawezi tenda kazi yake kwa haki na kweli wakati wote,ni wachache sana wanaweza jiuzulu kuepuka hilo!
Niseme tu kwamba,mgongano wa kimaslahi ni vigumu kuepukwa kwenye jambo kama hilo!
 
Hivi kama mmojawapo wa majaji waliopo wanatosha kuwa Jaji Mkuu, kwa nini Rais asimteue moja kwa moja?
 
. Kama Rais hajavunja sheria, hajavunja Katiba, hatumia madaraka vibaya ni kwanini watu wanataka afanye jambo ambalo anapanga kulifanya anyway?
MM kuna mambo matatu, sheria, prerogative na privilege Rais amepewa kisheria

Kuzuia mikutano ya siasa ililamikiwa kwasababu kisheria kwa kupitia katiba, uhuru wa kujieleza
Uhuru huo ukatengenezewa sheria ya msajili wa vyama.

Ni rahisi kusema kuna uvunjaji wa sheria, katiba au la kwasababu yapo maandishi

Prerogative power aliyopewa Rais ni katika mazingira ambayo sheria ima haziwezi kutumika haraka, kusubiri, dharura au vinginevyo.. Prerogative haipo wazi kama inavyodhaniwa.

Kila prerogative imejengewa uzio. Presidential prerogative ina Trust.
Kwamba, mkuu wa nchi amepewa jukumu zito na hiyo tu ni trust.

Prerogative pamoja na conditions inategemea Trust kwasababu ya public interest

Mambo yanayohusu prerogative hayapo kisheria moja kwa moja, yamejengewa uzio tu kwamba asivuke eneo fulani au acheze katika eneo fulani.

Ikitokea nje ya hapo prerogative inageuka kuwa abuse of power na mistrust
Kwa suala la Jaji, sheria imetamka uwepo wa Jaji mkuu na Kaimu jaji mkuu

Kaimu Jaji mkuu imewekwa ili kutoa prerogative kwa public interest si kwa personal interest. Hapa ndipo unapochanganya

Hakuna sheria iliyovunjwa, hakuna katiba iliyokiukwa, kuna kila dalili za matumizi mabaya ya prerogative. Hizo zinabaki kuwa hisia, lakini je, ni za kunyamazia?

Prof Kabudi alieleza Nyerere kwa kuelewa kilichotokea ili kupata public trust na kwamba matumizi ya prerogative yapo salama. Alikuwa na prerogative, haikutosha bila trust

Swali, tunasababu gani za kutumia prerogative kwa miezi 5 ya kukaimu nafasi?

Hatusemi ni makosa, tunauliza kwasababu 'mamlaka inatoka kwa wananchi' kama alivyofanya Mwl. kwa mujibu wa kabudi

Kama hakuna sababu au majibu, kuna kila sababu ya kuamini kuwa prerogative imekuwa ''abused''. Ikiwa hilo si kweli, tupeni sababu zenye mashiko
 
Sijasikiliza hayo ya bungeni na sidhani kama bado nina interest ya siasa za bunge hivi sasa ambazo kwangu naona ni kama zimekosa mvuto!!

Tuje kwenye hiyo hja ya kwamba, kukaimu kwa muda mrefu hakuwezi kumfanya Kaimu Jaji kushindwa kufanya kazi zake sawa sawa!!!

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Rais hana mamlaka ya kumtumbua Jaji wa Mahakama Kuu kirahisi rahisi tu!

Inapotokea sababu ambazo rais anaona Jaji huyu hafai tena kuwa jaji, hata kama ni suala la ukosefu wa maadili, bado Rais anatakiwa kwanza kuunda Tume ambayo itakuwa na Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume, na miongoni mwao angalau nusu wanatakiwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu kutoka nchi za Jumuiya ya Madola!

Tume hii itachunguza tuhuma dhidi ya Jaji kuona kama ni kweli au hapana!

NOTE: Nitapitia katiba ili nione kifungu hicho kinasemaje kwa yakini!!

Kutokana na kifungu hicho cha Katiba, Jaji Mkuu na in fact, Jaji yeyote wa Mahakama Kuu hawezi kuwa na hofu ya kutekeleza wajibu wake kwa kuhofia mamlaka ya uteuzi kwa sababu, anafahamu, hawezi kuondolewa hovyo hovyo au hata kwa makosa ya kubambikiwa!!!

Kaimu Jaji Mkuu kwa nafasi yake hiyo sio Jaji wa kawaida na wala sio Jaji Mkuu ambao wanaweza kulindwa na kifungu hicho hapo juu! Kwahiyo, Rais anaweza kumtoa muda wowote bila maswali kwa sababu, atakachomvua sio Ujaji wala Ujaji Mkuu bali Ukaimu Jaji Mkuu ambao sidhani kama Katiba inatoa ulinzi niliotaja hapo juu!!!

Hoja ndiyo hiyo hapo juuu!!

Na kwa staili hiyo, unaweza kuteua Kaimu Jaji Mkuu kama ilivyo sasa; na ukiona anazingua unamtoa unamweka mwingine nae anakuwa Kaimu Jaji Mkuu!! Sasa hofu isije kwamba, kwa kuhofia kutokuwa na ulinzi wa katiba, basi huenda wengine wanaweza kufanya mambo kwa kuyaridhisha mamlaka ya uteuzi!!

Isitoshe, huyu Kaimu Jaji Mkuu kila wakati atakuwa anaota kuwa Jaji Mkuu na sio kaimu tena!! Kwa namna ya kawaida kabisa; lazima ndoto zake zitaenda sambamba na kuhakikisha hazikeri mamlaka ya uteuzi!!
Ni matumaini yangu kwa mchango wako huu, hata wale wanaotumwa na vyama vyao kushabikia wamekuelewa na watabadiri mtazamo.
 
Hapa ndipo nnapoonaga udhaifu wa watunga sheria wetu, unaweza kuona weakness kama hii haikuwa forecasted wakati wa kupitisha katiba!

Ndio maana hata Mwl Nyerere aliiponda baada ya kuwa nje ya madaraka akabaini tuna katiba mbaya kiasi tukipata rais mwendawazimu anaweza kuitumia vibaya hata kuwa dikteita!
 
Kila prerogative imejengewa uzio. Presidential prerogative ina Trust.
Kwamba, mkuu wa nchi amepewa jukumu zito na hiyo tu ni trust.

Prerogative pamoja na conditions inategemea Trust kwasababu ya public interest

Mambo yanayohusu prerogative hayapo kisheria moja kwa moja, yamejengewa uzio tu kwamba asivuke eneo fulani au acheze katika eneo fulani.

Ikitokea nje ya hapo prerogative inageuka kuwa abuse of power na mistrust
Kwa suala la Jaji, sheria imetamka uwepo wa Jaji mkuu na Kaimu jaji mkuu

Kaimu Jaji mkuu imewekwa ili kutoa prerogative kwa public interest si kwa personal interest. Hapa ndipo unapochanganya

Hakuna sheria iliyovunjwa, hakuna katiba iliyokiukwa, kuna kila dalili za matumizi mabaya ya prerogative. Hizo zinabaki kuwa hisia, lakini je, ni za kunyamazia?

Lakini hizi hisia ni za nani hasa? Rais kweli afanye kazi kwa kujali hisia ya kile mtu mwenye hisia? hadi hivi sasa hakuna kwa kiwango cha kutosha public interests ukiondoa zile zinazoonekaa ni za kisiasa. Kwa mfano, chama cha wanasheria (TLS), Chama cha Majaji wastaafu n.k vikitoa tamko kuonesha kuwa kuna tatizo basi tunaweza tukasema kweli lipo; kwa sababu inaonekana ni kweli suala hili ni kubwa kivile. So far hakuna jambo hilo ukiondoa kile kinachoonekana hoja za kisiasa za kumpinga Magufuli na kumuonesha kuwa hafai ili watu kuhalalisha mitazamo ya kisiasa. Magufuli anaweza akakohoa hadharani na watu wakafanya ni hoja ya kisiasa. Anaweza akajikwaa na watu wakaona ni kwa nini amejikwaa wakati yeye ni Rais!

Suala la Jaji Mkuu na Kaimu Jaji Mkuu hadi hivisasa halina uzito wa kivile ukiondoa kama tukiliangalia kisiasa. Hakuna ambaye anaathirika - niko tayari unisahihishe - kwa Rais kuendelea kuchukua muda wake kabla ya kumthibitisha au kupata Jaji Mkuu mwingine.

Prof Kabudi alieleza Nyerere kwa kuelewa kilichotokea ili kupata public trust na kwamba matumizi ya prerogative yapo salama. Alikuwa na prerogative, haikutosha bila trust

Swali, tunasababu gani za kutumia prerogative kwa miezi 5 ya kukaimu nafasi?

Hatusemi ni makosa, tunauliza kwasababu 'mamlaka inatoka kwa wananchi' kama alivyofanya Mwl. kwa kuujulisha umma kwanini ilitokea vile

Mwalimu aliujulisha umma lini na wapi sababu zake za kuchelewa kupata mrithi wa Jaji Mkuu aliyeachwa na mkoloni? Kulikuwa na malalamiko yoyote kutoka kwa wananchi au taasisi za yeye kuchelewa kuchukua uamuzi huo?

Kama hakuna sababu au majibu, kuna kila sababu ya kuamini kuwa prerogative imekuwa ''abused''. Ikiwa hilo si kweli, tupeni sababu zenye mashiko
Kama ni suala la kuwa mtu anaamini kuwa prerogative imekuwa abused; lakini hana namna ya kuthibitisha kuwa imekuwa abused siwezi kutolea maoni maana masuala ya imani kwa kweli ni ya mtu mwenyewe. Kuna watu wanaamini vitu vya ajabu sana duniani na wengine wako tayari kujitoa mhanga kwa ajli yake au hata kuapa kwa mbingu na na nchi.
 
Kama ni suala la kuwa mtu anaamini kuwa prerogative imekuwa abused; lakini hana namna ya kuthibitisha kuwa imekuwa abused siwezi kutolea maoni maana masuala ya imani kwa kweli ni ya mtu mwenyewe. Kuna watu wanaamini vitu vya ajabu sana duniani na wengine wako tayari kujitoa mhanga kwa ajli yake au hata kuapa kwa mbingu na na nchi.
Mkuu, hatuwezi ku ignore hoja ya kwamba kuna abuse hata kama ni kwa 'imani'

Rais kwa mujibu wa katiba ana prerogative ya kuteua wabunge 10.

Anaweza kuteua watoto wake na mkewe na shemeji yake mdogo wakafika 10.
Hatakuwa amevunja sheria, au katiba

Tuta amini amefanya hivyo kwa imani tu kwamba ana prerogative ambayo ni sahihi

Kwa jicho lingine linalohitaji fikra, atakuwa ame abuse prerogative aliyopewa
Utathibitishaje kuwa haku abuse ikiwa kila kitu kipo sawa?

Utathibitisha kwa kutumia trust and public interest, hivi ni vitu vya 'imani' vyenye impact katika society.

Pili, mtu anaweza kuhukumiwa 'kuua kwa kudhamiria au kutodhamiria'

Dhamira ni kitu tuischoweza kukijua kwani kipo ndani ya mtu
Tunaweza kuthibitisha 'kudhamiria au kutodhamiria' kwa kuangalia mazingira ya tukio

Hili la Jaji kukaimu lina mazingira mzuri tu, kwa kuangalia utaratibu, muda, na ''utangamano wa mihimili'' kauli na mengi tu.
 
Mkuu, hatuwezi ku ignore hoja ya kwamba kuna abuse hata kama ni kwa 'imani'

Rais kwa mujibu wa katiba ana prerogative ya kuteua wabunge 10.

Anaweza kuteua watoto wake na mkewe na shemeji yake mdogo wakafika 10.
Hatakuwa amevunja sheria, au katiba

Anaweza kuwa amevunja sheria ya maadili ya viongozi; na labda sheria nyingine. Prerogative ya Rais kimsingi inazungumzia mambo yale ambayo yamo ndani ya uwezo wa Rais tu. Kuteua Jaji Mkuu ni mojawapo ya mambo hayo. Jinsi anavyomteua n.k yamo ndani ya Katiba na sheria.


Tuta amini amefanya hivyo kwa imani tu kwamba ana prerogative ambayo ni sahihi

Kwa jicho lingine linalohitaji fikra, atakuwa ame abuse prerogative aliyopewa
Utathibitishaje kuwa haku abuse ikiwa kila kitu kipo sawa?

Utathibitisha kwa kutumia trust and public interest, hivi ni vitu vya 'imani' vyenye impact katika society.

Pili, mtu anaweza kuhukumiwa 'kuua kwa kudhamiria au kutodhamiria'

Dhamira ni kitu tuischoweza kukijua kwani kipo ndani ya mtu
Tunaweza kuthibitisha 'kudhamiria au kutodhamiria' kwa kuangalia mazingira ya tukio

Hili la Jaji kukaimu lina mazingira mzuri tu, kwa kuangalia utaratibu, muda, na ''utangamano wa mihimili'' kauli na mengi tu.

Hili linawezekana limo kwa baadhi ya watu; na sidhani kama ni wengi - sina sababu ya kuamini kama watu wengi wanajali hili ukiondoa wanasiasa. Nje ya hapo, rais yupo ndani ya uwezo na madaraka yake na hajafanya lolote lile la kuweza ku sema ama amevunja sheria au ametenda nje ya maslahi ya Taifa. Atamteua Jaji Mkuu mwingine wakati muafaka au atamthibitisha aliyepo. Tusubiri tu bila kulazimika kufikiria mambo 100 ambayo hatuna uwezo wa kuyajua kwa uhakika au hata kuhisi kuwa tuna uwezo wa kuyajua kwa uhakika.
 
"Mzee Mwanakijiji, post: 20890882, member: 118"] hadi hivi sasa hakuna kwa kiwango cha kutosha public interests ukiondoa zile zinazoonekaa ni za kisiasa.
Public interest ni pale inapokuwa na hofu kuhusu 'probabtion' ya Jaji mkuu. Utaratibu wa kumuondoa Jaji mkuu na kumuondoa Kaimu ni tofauti
Hilo linatia shaka na maamuzi ya Kaimu. Inaweza kuwa shaka tu, lakini ni shaka yenye public interest
Kwa mfano, chama cha wanasheria (TLS), Chama cha Majaji wastaafu n.k vikitoa tamko kuonesha kuwa kuna tatizo basi tunaweza tukasema kweli lipo; kwa sababu inaonekana ni kweli suala hili ni kubwa kivile. So far hakuna
Hapa nakubaliana nawe kwasababu hata alipowaambia Wanasheria wamalize kesi atawapa robo ya mapato, wao hawakuona ni jambo la hatari
Alipowaambia mawakili wanaosimama 'wahalifu' nao wawekwe ndani hakuna aliyeona ni jambo lililo kinyume.

Hata alipoingilia uchaguzi kwa mkono wa serikali , walinung'unika tu chini chini.

Chama cha majaji wastaafu kilisema 'kuna nchi zinamatamani ziwe na Rais huyu hata kwa siku' Hii ndiyo kauli tuliosikia.
Magufuli anaweza akakohoa hadharani na watu wakafanya ni hoja ya kisiasa. Anaweza akajikwaa na watu wakaona ni kwa nini amejikwaa wakati yeye ni Rais!.
Kama sikosei ''wainglishi'' wanasema unapokuwa public figure unaoteza baadhi ya mambo na hifadhi yako inakuwa haipo tena

Ndivyo ilivyo kwa viongozi wote duniani hata watu maarufu, si kwake pekee
 
Nimesikiliza kwa makini kile kinachoitwa "darasa" la Prof. Kabudi jana Bungeni kuhusiana na suala la Kaimu Jaji Mkuu na hasa hoja nzima ya kukaimiwa kwa nafasi ya Jaji Mkuu. Inasikitisha kwanza kwamba kuna watu wanasifia kuwa ametoa "darasa" na kwamba watu walikuwa wanamsikiliza kama wanafunzi katika Shule ya Msingi Mtakuja!

Je, ni kweli kile alichokisema watu walikuwa hawakijui? Ni kweli wabunge na wanasheria walioko Bungeni walikuwa hawajui yale yaliyokuwa yanasemwa?

Kuna hoja ya kuuliza swali; kwamba - kwanini Rais amemteua mtu kukaimu Ujaji Mkuu kwa muda wote huu. Swali ambalo halipaswi kuulizwa na tulilikataa wakati ule ni kuhusu mamlaka ya Rais kumteua mtu kukaimu Ujaji Mkuu. Hili liko ndani ya mamlaka ya Rais (Presidential prerogative). Lakini pia swali hili kwa ukubwa wake halipaswi kuulizwa isipokuwa kisiasa (political question) ili watu kupata hoja za kisiasa au ujiko wa kisiasa. Kwamba, mtu anataka kuonesha kuwa Magufuli amekosa mtu wa kuwa jaji mkuu, au kwamba Magufuli ana tatizo na mahakama n.k. Hili si jambo sahihi; wabunge kama wanaona Rais anatumia muda mrefu kujaza nafasi ya jaji mkuu wana uwezo wa kubadilisha sharia na hata Katiba chini ya Ibara ya 100 ya Katiba yetu.

Kama wanataka nafasi ya Jaji Mkuu isikaimiwe indefinitely (kama hoja ya Lissu ilivyoashiria) namna pekee ni kubadilisha Katiba au sheria ili kuweka kikomo kama ilivyo katika baadhi ya nafasi za utumishi wa umma ambapo sheria inasema mtu atakaimu nafasi kwa muda fulani na baada ya hapo basi mtu wa kudumu ateuliwe au aliyekaimu athibitishwe. Wao wabunge (watunga sheria na wanaoweza kufanya mabadiliko ya Katiba) wanaweza kuweka kikomo labda kwa ajili ya mustakabali)

Kama kwa mfano Rais angejaza cheo cha Ujaji siku moja tu baada ya Jaji Othman kustaafu wapo ambao labda wangeweza kuja na hoja ya kwanini amejaza nafasi haraka bila kuonesha tafakari sana au klutumia muda kufanya utafiti wa kutosha! Lakini pia kuna swali ambalo inabidi liulizwe kwa wale wanaolalamikia - kwa Rais kuweka Kaimu Jaji Mkuu ni shughuli gani ya Mahakama Kuu ambayo haiwezi kufanyika sasa hivi kwa vile kuna kaimu Jaji Mkuu au ni kitu gani hakifanyiki katika mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani ambacho kinapaswa kufanywa na jaji mkuu peke yake. Hili ndilo linaweza kuwa hoja ya kwanini inahitajika Jaji Mkuu na siyo Kaimu Jaji Mkuu?

Lakini kung'ang'ania kitu ambacho wote wanajua hakipo - kwamba Rais hajavunja sheria wala Katiba, na kuwa hakuna kikomo cha muda kilichowekwa kwa hoja ya kuwa ni mazoea mapya haitoshi kuwa hoja.

Lakini wapo ambao wanasema kuwa kwa kutomthibitisha Kaimu Jaji basi Kaimu Jaji anaweza asifanye anayotakiwa kufanya kwa kuhofia kuiudhi mamlaka ya uteuzi. hilo si wazo sahihi katika utawala. Unapokaimu nafasi unakuwa na madara yote ambayo unayo kwa mujibu wa kukaimu kwako. Hakuna hoja ya kumridhisha mtu au la. Makamu wa Rais anapokaimu nafasi ya Urais wakati Rais hayupo kwa mujibu wa sharia ana madara yote ambayo ameruhusiwa kuwa nayo kwa mujibu wa Katiba. Na hili ni kweli kwa mtu mwingine yeyote ambaye Rais anaweza kumpa nafasi ya kukaimu jambo lolote kwa niaba yake. Mtu yeyote professional hajali sana kama atamfurahisha mtu au la atafanya kwa mujibu wa madaraka aliyopewa. Mtu ambaye atajali kuwa akifanya jambo Fulani atamuudhi aliyemteua au chombo cha juu hafasi kushika nafasi hiyo.

Somo ambalo Kabudi angepaswa kulitoa na labda wengi wanalihitaji kulielewa ni hili la Presidential prerogatives..
Mazingira ya kukaimu ni kama hakuna wenye sifa ndiyo hutumika lakini hapa mamlaka yametumika vibaya
 
Mazingira ya kukaimu ni kama hakuna wenye sifa ndiyo hutumika lakini hapa mamlaka yametumika vibaya
Hapana bana; hapa tena unadhania vile vile. Hatujui ni kwanini Rais amechukua muda mrefu kujaza nafasi hiyo. kama wapo watu wenye sifa ya kuteuliwa kuwa majaji wa mahakama kuu basi wapo wenye sifa ya kuweza kuwa jaji mkuu. Bila ya shaka kuna sababu nyingine ambazo hatuzijui za kwanini amechelewa kujaza nafasi hii. Sababu hizo zikiondoka au kushughulikiwa bila ya shaka nafasi hiyo itajazwa na mtu wa kudumu. Nje yapo tutakuwa kama wapiga ramli.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Public interest ni pale inapokuwa na hofu kuhusu 'probabtion' ya Jaji mkuu. Utaratibu wa kumuondoa Jaji mkuu na kumuondoa Kaimu ni tofauti

Umepata wapi hili wazo kuwa Kaimu Jaji Mkuu yuko kwenye probabation?

Hilo linatia shaka na maamuzi ya Kaimu. Inaweza kuwa shaka tu, lakini ni shaka yenye public interestHapa nakubaliana nawe kwasababu hata alipowaambia Wanasheria wamalize kesi atawapa robo ya mapato, wao hawakuona ni jambo la hatari
Alipowaambia mawakili wanaosimama 'wahalifu' nao wawekwe ndani hakuna aliyeona ni jambo lililo kinyume.

Haiwezekani shaka ya watu wawili au watatu itoshe kuwa shaka ya "umma" mzima.

Hata alipoingilia uchaguzi kwa mkono wa serikali , walinung'unika tu chini chini.

Chama cha majaji wastaafu kilisema 'kuna nchi zinamatamani ziwe na Rais huyu hata kwa siku' Hii ndiyo kauli tuliosikia. Kama sikosei ''wainglishi'' wanasema unapokuwa public figure unaoteza baadhi ya mambo na hifadhi yako inakuwa haipo tena

Ndivyo ilivyo kwa viongozi wote duniani hata watu maarufu, si kwake pekee

Haya ni mambo mengine; irrelevant kwenye hoja hii.
 
Hapana bana; hapa tena unadhania vile vile. Hatujui ni kwanini Rais amechukua muda mrefu kujaza nafasi hiyo. kama wapo watu wenye sifa ya kuteuliwa kuwa majaji wa mahakama kuu basi wapo wenye sifa ya kuweza kuwa jaji mkuu. Bila ya shaka kuna sababu nyingine ambazo hatuzijui za kwanini amechelewa kujaza nafasi hii. Sababu hizo zikiondoka au kushughulikiwa bila ya shaka nafasi hiyo itajazwa na mtu wa kudumu. Nje yapo tutakuwa kama wapiga ramli.
Lakini mkuu hizo sababu nyingine si ndio hasa wanaohoji wanaona wanayo haki ya kizijua?

Wanataka kujiridhisha kuwa hizo sababu ni zenye mashiko au maslahi ya umma.

Zisiposemwa, ni wazi watu watajaribu kufikiria za kwao.

Hivi ni sahihi kufikiri kuwa Katiba yetu ilikusudia kumpa Rais discretion ya kutoteua Jaji Mkuu na badala kuteuwa Kaimu Jaji Mkuu bila ukomo wowote?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
"Mzee Mwanakijiji, post: 20891553, member: 118"]Umepata wapi hili wazo kuwa Kaimu Jaji Mkuu yuko kwenye probabation?
''Probation''
Haiwezekani shaka ya watu wawili au watatu itoshe kuwa shaka ya "umma" mzima.
Sina takwimu lakini waziri anapojibu mbele ya wabunge 200+hatuwezi kusema ni watu 2
Waziri anapojikanyaga hoja inakuwa kubwa hata kama ni ndogo
Kunapokuwa hakuna majibu bali watu kumtumia Nyerere kama jibu, lipo jambo
Tunapohalalisha prerogative kama holela halali, kuna tatizo
Haya ni mambo mengine; irrelevant kwenye hoja hii
Mkuu si wewe umezungumzia kuhusu TLS na chama cha majaji, nami kikasema ni kweli hatujasikia kauli zao.

Ukasema watu wanamuangalia Magufuli hata akijikwaa, nikajibu si peke yake ni watu wote maarufu. Nimejibu sikuondoka katika mada

Hili la Jaji mkuu kukaimu lina jambo, halina utetezi, Kabudi na darsa ilikuwa aibu
Sijaona mahali pengine panaposhawishi vinginevyo

By the way nakubaliana nawe , next time Kabudi aangalie darsa lisiwe lile tena

Mkuu kwanini neno probation limekupa taharuki?
 
Lakini mkuu hizo sababu nyingine si ndio hasa wanaohoji wanaona wanayo haki ya kizijua?

Wanataka kujiridhisha kuwa hizo sababu ni zenye mashiko au maslahi ya umma.

Zisiposemwa, ni wazi watu watajaribu kufikiria za kwako.

Hivi ni sahihi kufikiri kuwa Katiba yetu ilikusudia kumpa Rais discretion ya kutoteua Jaji Mkuu na badala kuteuwa Kaimu Jaji Mkuu bila ukomo wowote?

Huwezi kuzuia watu kufikiria au kudhania; na huwezi kumridhisha kila anayetaka kumdhania. Kwa mfano, akiamua kumthibitisha Profesa Ibrahim unadhani watu wote wataridhika; si wataanza hoja nyingine "Rais aseme kwnaini alichelewa kumthibitisha wakati alikuwa na sifa zote"? Akitemua mwingine watu watasema kwanini amemuacha Ibrahim ina maana hafai? sasa awe anatoa jibu kwa kila swali la mtu ambaye anataka kujiuzuliza. Unafikiri kutakuwa na ukomo wa maswali?
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Back
Top Bottom