DAR: Zitto Kabwe(Mb) akamatwa na Polisi akiwa Uwanja wa Ndege akitokea Kigoma

Jamaa si huwa anajigamba anandumba hakamatiki? Au wazee wa Dom na Kigoma wanapimana nguvu, ile nyumba inaweza ikawa imeunguza ndunguli muhimu sana.
 
Mnaojua Sheria hvi kuitwa kwenye Kamati ni lazma ukamatwe na Polis?
 
Ndo taarifa zinavyodai...

======

TAARIFA KWA UMMA

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Zitto Kabwe amekamatwa na Polisi muda huu uwanja wa ndege wa JNIA, Dar es Salaam wakati akitoka Kigoma.

Kwa sasa wanasheria wa chama wanafuatilia kujua sababu za kukamatwa kwake.

Abdallah Khamis
Afisa Habari - ACT Wazalendo

======

UPDATE:

Zitto atasafirishwa kwenda Dodoma kesho tayari kwa kuhojiwa na Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kukamatwa kwa mbunge huyo.

UPDATE 2:

Polisi wanasema madereva wametoka Dodoma usiku huu na gari la Bunge na wanatarajiwa kuingia saa nane Usiku. Zitto kasema haendi na gari Dodoma kwa madereva waliokuja usiku kwani hawaamini kama hawana ndege, yeye yupo tayari kulipa gharama lakini haendi na gari.
Safi sana Zitto.. Umeshtuka mapema......hawa jamaa ni wauaji siku izi..
 
Mnaojua Sheria hvi kuitwa kwenye Kamati ni lazma ukamatwe na Polis?
Yaani kuna vitu vinafanyika ata mtoto mdogo anaweza kushangaa imebaki mwanafunzi akiwa suspension skul cku ya kurudi badala ya kuja na mzazi watakuwa wanatumwa polisi ndo tz yetu tunakoelekea
 
Ila watanzania tunahaha sana. Hii haki mnayoisema kuwa watu wanapigania siku tukiipata nawahakikishieni hatutaona mabadiliko yoyote. Tuna hamu sana ya kufanya mapinduzi lakini hatuna dira kamili.

Tusijifanye wanafiki sana wa kuisema serikali tawala kila kukicha. Ukweli ni kwamba nchi yetu ni masikini na ipo kwenye hali mbaya sana kutokana na uozo wa baadhi ya viogozi hasa wa awamu za nyuma. Tunalilia sana mabadiliko lakini tunasahau ya kwamba ili kuyapata ni lazima tupitie hali ngumu.

Tukiona mambo yanazidi kuwa mabaya kwani 2020 mbali? Tunamtoa tu...
 
mbona makonda alivyohojiwa na kamati ya maadili alichelewa chelewa sana hakukamatwa?
Think twice
 
Siku za hivi karibuni Zitto amebadilika naona atakuwa ameamua kukinywea kikombe wanachokinywea wapinzani wenzake hasa baada ya CCM kutokumjali kama awali.
No simwamini saana huyo Bwn.
Alianzisha ACT kuigawa CHADEMA
ili tushindwe uchaguzi yeye ni pandikizi.
Hafai!
 
Inasikitisha sana ila Mungu amsaidie Zitto arudi salama maana hawa watu wasiojulikana wanaweza mvamia ikawa balaa jingine.
 
Back
Top Bottom