Mambo huweza nitinga, niisakapo riziki,
Mkahisi nawatenga, mkahisi siwataki,
Juweni nasaka mpunga, ili niishinde dhiki,
Niwapo kimya wapendwa, msidhani siwapendi.
Najua mnaumia, kwani hamwishi lalama,
Nami ninawasikia, huku moyo kiniuma,
Najaribu kuzuia, kwa maneno ninasema,
Niwapo kimya wapendwa, msidhani siwapendi.
Salamu kweli muhimu, daima kukumbukana,
Huleta mashamshamu, nayo mapenzi kufana,
Ukimya unayo sumu, kama utazidi sana,
Niwapo kimya wapendwa, msidhani siwapendi.
Nipo nanyi ndugu zangu wana JF, hakika nitakuja Dar siku hiyo ya MKODOBWE
Nyie nimewaweka MMU kwa masaa 24 hata hamnishukuru?
Nimewakamataaaajeeee??
mmhhh ni wewe au kuna mtu kaiba password??azam coke tena.
Eti si utanipitia??tukae wote kama siku ile sawa??
Mi nawaogopa watu kama wakina Asprin maana hakawii.
Sasa basi mpendekeze na id zenu zote ...
Maana kama Asprin yeye ndo Mwanamalundi na wale wote wenye mtazamo huo sitaki kuwatag mtaje na id zenu zote...
Umeingia mkenge kwenye "afadhari" siyo? Fita ni Fita Mura!!babu unataka kujiongezea cv??
Ule si mwandiko wako...we taja tu zile id zako za siku zote
Fita ni Fita sichaenda kumuona bhaana... si umeona mufua irivhobhigha kwa wingi?Shikamoo babu...ulienda kumuona fitanifita mura??
Mie tena.....
Mambo huweza nitinga, niisakapo riziki,
Mkahisi nawatenga, mkahisi siwataki,
Juweni nasaka mpunga, ili niishinde dhiki,
Niwapo kimya wapendwa, msidhani siwapendi.
Najua mnaumia, kwani hamwishi lalama,
Nami ninawasikia, huku moyo kiniuma,
Najaribu kuzuia, kwa maneno ninasema,
Niwapo kimya wapendwa, msidhani siwapendi.
Salamu kweli muhimu, daima kukumbukana,
Huleta mashamshamu, nayo mapenzi kufana,
Ukimya unayo sumu, kama utazidi sana,
Niwapo kimya wapendwa, msidhani siwapendi.
Nipo nanyi ndugu zangu wana JF, hakika nitakuja Dar siku hiyo ya MKODOBWE
Afu unajua navyokumisi au unanichezea tu?Na watu wote waseme Ameeeeeen!!!!
Afu unajua navyokumisi au unanichezea tu?
Wajukuu ni mali ya babu!!:becky::becky:Babu itabidi ukae mbali na wajukuu!
Wewe unatuchukia, Mimi nimeshatambua,
Vikao wavikimbia, Kazi unasingizia,
Hakika watubania, Nduguzo watukimbia,
Kimya chako cha mashaka, Nduguzo watuchukia
Surayo watubania, Kutingwa wasingizia,
Kila mara wakimbia, Vikao vya jumuia,
Kazi wazisingizia, watukimbia jamaa,
Kimya chako cha mashaka, Mduguzo watukuchukia.
Sababu waturushia, Tena za kuongopea,
Surayo twatamania, wewe unaifichia,
Kwanini watuchukia, tena unatukimbia?
Kimya chako cha mashaka, Mduguzo watukuchukia.
Na Babu ODM
Kaunta ya Juu, Mfalme Nyota,
Fyatanga Bar
Boko Basihaya.
Nakala: Mtambuzi, gfsonwin, lara 1, amu, Paloma, Jiwe Linaloishi, cacico, snowhite, Madame B, Fidel80, Naniliyu, Zion Daughter KakaKiiza, Ruttashobolwa, Superman naaaaa........... well well well charminglady, Nicas Mtei.
Mtumie majina ya JF bana.
Kwa mfano labda wewe jina lako ni Kayanda Muyago, ambalo ndilo litakalotokea kwenye Tigo Pesa, inabidi unitumie SMS ukitaja jina ID yako ya JF.......
Daaaaa! Nimegundua Mtambuzi utatugundua wengi maana majina halisi yatatokea! Sasa itabidi nikutumie kwa kupitia wakala aiseee! SMS itafuata baada ya hapo.
Babu Asprin hata mie nakukumbuka sana, hasa kile kitambaa chako ulichotupia "Ki-Tupac style" siku ile pale Brajec kilinikoshajeeeeee!!!!!!
Hope utaja nacho WHITE PARTY make nacho ni cheupe.........