Dar: Watumishi wa Move Tanzania Ltd. Mbaroni kwa kuisababishia Serikali hasara ya Tsh. 563,351,698

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Shauri la Jinai namba 186/2023 - Jamhuri dhidi ya Ernest Odhul Omalla na Juma Salum Gululi ambao ni wamiliki wa Kampuni ya Move Tanzania Ltd, imefunguliwa leo Oktoba 18, 2023 mbele ya Mhe. Richard Kabate (PRM) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Washtakiwa wameshtakiwa kwa kosa la Kughushi, Kuwasilisha nyaraka za uongo, Kujipatia mkopo kwa njia ya udanganyifu, na kuisababishia Serikali hasara ya shs 563,351,698.67/- kinyume na Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16 pitio la Mwaka 2019.

Washtakiwa wamekana makosa yote 16 na kupelekwa mahabusu baada ya kutokukidhi masharti ya dhamana.

Kesi imeahirishwa hadi tarehe 30.10.2023 kwa ajili ya kusoma Hoja za Awali.
 
...Waongee na DPP !!..
 
Mbona watumishi waserikali wanawapaga serikali hasara kubwa na hwakamatwi lakini akitokea mlalahoi kama sisi watu wa hali ya chini tunapelekwa huko huko nakisha kuhukumiwa
 
Back
Top Bottom