DAR: Rais Kabila awasili Tanzania

DAR: Rais Kabila awasili Tanzania

Rais wa jamuhuri ya KIDEMOKRASIA ya Kongo amewasili Tanzania na kupokelewa na Mwenyeji wake Mtukufu John Pombe Magufuli.

Karibu Tanzania Rais Kabila Taifa linakuhitaji ili tudumishe ujirani na urafiki wetu uliodumu kwa muda mrefu na Tunaufurahia Uwezo wako mkubwa wa kuwaongoza wakongo.
Mkuu nimekuelewa sana hapo kwenye capital letters
[emoji12]
 
Hivi Rais Magufuli amekuwa lini mtukufu. Acheni kumkebehi Mungu, Mungu pekee ndiye mtukufu
 
Kwa hiyo mtu pekee Congo nzima wa kudhibiti mate ya wazungu juu ya nchi hiyo ni Joseph Kabila tu? Wewe ni li..pumba kabisa. Suppose akifa leo ingawa hiyo ni mipango ya Mungu ina maana Congo DR inauzwa kwa wazungu papo hapo?
Nani alekwambia kabila ni mkongo?
 
Upo karne mbili za fikra nyuma! Hivi unajua ni mamilioni mangapi ya wazungu mate yanawatoka kwa Congo DRC! You are very naiive!
Hajui.. msamehe bure!!!
Anachokijua yeye ni kile pekee anachoambiwa na mashirika ya habari ya kimagharibi yenye mrengo wa kibeberu...
Yeye kwa akili yake fupi anajua machafuko ndani ya DRCongo yanatokana na wacongo wenyewe kumbe hajui wafansa na washkaji zao waingereza wakisindikizwa na mmarekani wanavyochezesha shere ndani ya ardhi ya congo jinsi watakavyo kwa manufaa yao binafsi...
 
Isingeonesha ungesema pia!
Hawakosagi cha kusema...
Nakumbuka waliwahi pia kuhoji kwanini Magu anakunywa maji wakati anahutubia...

Ni nafuu ya mchawi kuliko watu hawa wa bavicha...
Wana kasoro kubwa sana kichwani..
 
KARIBU SANA RAIS WA KUDUMU WA CONGO TANZANIA

OVA
 
unnamed.jpg


Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila Kabange, amewasili hapa nchini leo October 03 2016 kwa ziara rasmi ya kiserikali ya siku tatu na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Rais Joseph Kabila Kabange amepokea heshima ya kupigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili yake na baadaye kushuhudia burudani ya vikundi vya ngoma.

Hapo kesho October 04 2016 Rais Joseph Kabila Kabange atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli, ataweka jiwe la msingi la jengo la Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na baadaye kushiriki dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 
Kabila ni mgeni wetu maalumu, kwa mara ya kwanza nawaunga mkono TBC kwa hili

DRCongo ni muhimu sana kwa uchumi wa Tanzania. Bandari ya Dar na reli ya kati ya standard gauge zikisafirisha bidhaa za DR Congo tu ni mapato budget yote ya nchi yetu kwa mwaka. Acheni siasa uchwara kwenye uchumi. Kama ni demokrasia mbona hamlaumu China au kama ni uchaguzi mbona Rwanda na Uganda bado tunao kwenye Jumuiya? Waacheni wakongo na siasa zao za ndani.
 
Kama ingekuwa Mwl bado yu hai asingetua TZ, tunaafiki ubadilisha wa katiba Congo?
 
Bwana mkubwa ambaye miaka ile alisoma zanaki jioni, kesho anakwenda port, sehemu ambayo mheshimiwa wetu alikwenda wiki iliyopita na hakuridhishwa na mengi aliyoyakuta.
 
Kabila, kagame... Mu7

Balaa

Hii ni baraka kiuchimi na tuombe uhai 2020 tukutane hapa. Tena JPM amshawishi aingie EAC tuwe na soko kubwa lenye nguvu na tofauti zote za kisiasa tutazimaliza pamoja.
 
Back
Top Bottom