johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,998
- 142,023
Kijana mmoja aliyefahamika kwa Jina la Lucas ametiwa mbaroni na police kwa kutapeli Watu akijifanya ni Mganga wa Kienyeji
Kamanda Muliro amesema Lucas atafikishwa mahakamani kesho
Source: Upendo TV
Mlale Unono 😀😀😀🔥
=====
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limemkamata na kumuhoji kwa kina Mtu aliyejifanya Mganga wa jadi Lucas Salumu Baswege(42), Mkazi wa Kisemvule, Mkuranga kwa tuhuma za kuwanywesha dawa Watu zaidi ya 16 maeneo tofautitofauti dawa inayodhaniwa kuwa ni sumu na kuwaibia.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Muliro Jumanne amesema “Uchunguzi wa awali umebaini Mtuhumiwa huyo alifanya matukio kama hayo maeneo ya Mjimwema Kigamboni, Tuangoma , Kilungule na Ubungo, vitu alivyoiba tayari vimekamatwa na Polisi ikiwemo pikipiki iliyoibwa Tuangoma na simu za mkoni 10 ambazo tayari zimetambuliwa na wenye nazo”
“Jeshi la Polisi pia limemkamata Thomas Mhagama (35) Fundi simu wa Temeke Sandali ambaye amekuwa akishirikiana na Mganga huyo wa jadi kwa kupokea simu za wizi na kuziuza kwa Watu, Watuhumiwa wote watafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo”
Pia soma: Dar: Polisi wamsaka Mganga aliyelewesha Watu 16 wa familia moja kisha kuwaibia