Dar: Mabasi ya Mikoani na nje ya Nchi, yaanza kutumia Kituo kipya cha Mbezi Luis

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,848
15,267

Niko hapa Mbezi Mwisho hatua chache kabisa karibu na stand mpya ya Mbezi baadhi ya Mabasi yaliyotoka mkoani yameshaanza kuingia kituo kikuu cha mabasi Mbezi.

=====

Kituo kipya Cha Mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi Cha Mbezi Luis kimeanza rasmi majaribio leo ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amesema kwa Sasa kituo hicho kinaweza kuanza kutumika Kutokana na miundombinu muhimu ya kituo kuwa Katika Hali mzuri.

Akizungumza wakati wa zoezi la majaribio lililowahusisha Askari wa usalama barabarani na Wadau wa vyombo vya usafiri, RC Kunenge ameshuhudia Mabasi yakiingia na kutoka pasipo usumbufu wowote.

Aidha RC Kunenge amesema kwa Sasa kinachoendelea ni matengenezo madogomadogo ya umaliziaji wa jengo na miundombinu mingine ambapo Hadi Sasa Ujenzi umefikia zaidi ya 90%.

Pamoja na hayo RC Kunenge amesema Ujenzi wa barabara ya kuingia kituoni hapo nao unaendelea vizuri chini ya Wakala wa TANROAD ambapo amewahimiza kuongeza kasi ili wakamilishe mradi mapema.

Hata hivyo RC Kunenge ameongeza kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha maagizo ya Rais Dkt. John Magufuli ya kutaka Ujenzi ukamilike mwishoni mwa mwezi huu yanatimia.
DSC_0646.JPG
DSC_0650.JPG
DSC_0649.JPG
DSC_0652.JPG
DSC_0651.JPG
AQ1I6088(1).jpg
DJI_0059.jpg
DJI_0056.jpg
DJI_0048.jpg
AQ1I6124.jpg
AQ1I6113.jpg
AQ1I6110.jpg
AQ1I6108.jpg
AQ1I6099.jpg
AQ1I6095.jpg
 
Back
Top Bottom