Mkuu
adolay,
Nashukuru sana kwa majibu yako murua na ya kutia matumaini Tanzania ni yetu sote wala hakuna kikundi chenye mamlaka na haki dhidi ya wengine, hii migogoro ya kidini ndio baina yetu ndio mtaji mkubwa wa CCM.
Wakati mwingine watu wanaweza kudhani Waislam wote ni CCM hapana watu wanakeleka na dharau na kejeli wanafanyiwa na baadhi ya Pro-Chadema JF Mkuu wangu bahati nzuri humu JF tunajuana kwa michango yetu na misimamo yetu kuna Chadema Great thinkers, kuna Chadema-Kata.
Wakati mwingine sidhani kama Dr Slaa anapendezwa na michango ya wafuasi wake humu JF hata akija kujibu hoja watu wanalipiza kisasi kwa kumjibu hovyo Dr Slaa ndio maana siku hizi umuoni JF yupo zake FB.
Mkuu jaribu kuwa unakemea maovu kutoka kwa wale wote wanaochafua jukwaa na kuvunja umoja wetu.