Dar kuingia gizani Mei 31 KUTWA NZIMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dar kuingia gizani Mei 31 KUTWA NZIMA

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Maxence Melo, May 27, 2009.

 1. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #1
  May 27, 2009
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,701
  Trophy Points: 280
  JIJI la Dar es Salaam litaingia kwenye giza nene Mei 31 mwaka huu wakati Shirika la Umeme nchini (Tanesco), litakapozima mitambo ya kuzalisha umeme wa gesi ya kampuni ya SONGAS.

  Taarifa ya Tanesco iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam imesema mitambo hiyo itazimwa kupisha matengenezo ya kawaida katika njia ya kupitishia gesi kwa siku nzima kuanzia saa 10:00 alfajiri hadi saa 12:00 jioni. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kuzimwa kwa mitambo hiyo kutasababisha upungufu wa nishati hiyo kwa megawatti 50 na kusababisha baadhi ya maeneo hayo ya jiji la Dar es Salaam kukosa umeme.

  Maeneo yaliyotajwa kwenye taarifa hiyo kuwa yatakosa umeme ni Wilaya ya Temeke maeneo ya Mwembe Yanga, Tandika Azimio, Tandika sokoni, Kichangani, Temeke Wailes, Temeke Hospital, Maeneo yote ya Yombo, Veternary, Jeje Industry, Petrolube, Tanzania Printers, Metal Product, Kilungule, Tazara flats, Boney M, Vituka, Dovya, Stereo Wiyani Kinondoni maeneo yatakayoathiri ni Kinondoni Kaskazini maeneo ya M.M.I Steel Industries, Mikocheni B, Kawe Beach, Baadhi ya eneo la viwanda pamoja na kiwanda cha Bidco, Kunduchi Mtongani, Salasala, Baadhi ya maeneno ya barabara ya Africana na viwanda vya Raffia Bag na Family Soap. Tatizo hilo pia litawakumba wakazi wa Kinondoni Kusini katika maeneo ya Sinza, Manzese, Tandale, Kijitonyama na Mwananyamala.

  Taarifa imezidi kueleza kuwa wilayani Ilala umeme hautapatikana katika maeneo ya NSSF Water Front, Tanzania Tea Blenders, Polisi Makao Makuu, TRC, Makao Makuu ya DAWASCO, Keko Mwanga, Mtaa wa Lugoda, Baadhi ya maeneo ya Kariakoo kutokea mtaa wa Msimbazi mpaka Lumumba na Ilala Boma. Maeneo mengine ni Ilala Sharif Shamba, Ilala Bungoni, Buguruni Malapa, Buguruni Rozana, Buguruni Sokoni, Sehemu ya barabara ya Mandela kuanzia Buguruni mpaka Tabata Dampo, Tabata Liwiti, Tabata Bima, Tabata Mawenzi, Tabata Kimanga na Tabata Kisukuru. Maeneo hayo ni na Makoka, Kiwalani kwa Gude, Jet Club, Kipawa, Mtaa wa Azikiwe, Mtaa wa Kisutu, Hospitali ya Hindu Mandal, Jengo la Haidery Plaza, Mnazi Mmoja sehemu ya barabara ya Morogoro kuanzia Mtaa wa Kisutu mpaka mtaa wa Samora yatakosa umeme kuanzia saa 10 alfajiri hadi saa 6:00 mchana.

  Tanesco imesema umeme utakatika kuanzia saa 6:00 mchana hadi saa 12:00 jionii katika Mtaa wa Muheza, Mtaa wa Msimbazi, Mtaa wa Nkrumah mpaka Mtaa wa Samora, Upanga Mashariki, Sea View, Kituo cha Polisi cha Salender Bridge, Mitaa ya Uhuru, Magila, Lumumba, Mahiwa na Livingstone. Imesema pia umeme utakatika sehemu ya barabara ya Bibi Titi kuanzia barabara ya Morogoro, Ally Hassan Mwinyi, DIT, Business College, Hospitali ya Regency, Viwanda vya Zenufa, Mukwano, Bakhresa, Murzah Oil, Vingunguti, sehemu ya Kiwalani, baadhi ya maeneo ya barabara ya Nyerere kuanzia TAZARA mpaka Metrol Steel Kiwalani, Segerea, Kinyerezi na Bunyokwa.

  "Hali ya umeme itarejea kama kawaida mara baada ya matengenzo hayo kukamilika," imesema taarifa hiyo na kuwaomba radhi wateja.
   
 2. J

  Jafar JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2009
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tunashukuru - lakini pia wametoa tahadhali kupitia magazeti mengi tu ili wengi wapate ujumbe. Kwa tanesco hiyo hesabu ni saa 24 bila umeme.
   
 3. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Wakazi wa Magomeni hatutakuwa gizani au ni macho yangu yananidanganya?

  Kama ndivyo asante Yesu.
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  May 27, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Miafrika bana....yaani muda wote huu hawakujiandaa na plan B ya kuhakikisha siku hiyo watakuwa wanatumia umeme wa dharura...
   
 5. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 910
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Mkuu, umesahau kwamba plan B ilikuwa ni kununua mitambo ya dowans! Mlivyopiga kelele basi na wao wakazira. LIWALO NA LIWE!
   
 6. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  mkuu ile plan B yao ilikuwa ni kuzima umeme kwa kisingizio chochote kile na hamna la kuwafanya
   
 7. K

  Kifimbocheza JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 496
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  NI Jumamosi 30th May 2009 (Saturday) na sio 31st May 2009 (Sunday)
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  May 27, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Halafu Miafrika tuna akili.....heheheheheheheheeee
   
 9. M

  Masatu JF-Expert Member

  #9
  May 27, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  And all this after 48 years of so called "independence"
   
 10. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #10
  May 27, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  NN
  yaani we acha tu.
  Wacha niwahi kijiwe cha kahawa naweza kuambulia choroko leo
   
 11. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #11
  May 27, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Are you not the same guy advocating CCM day in day out?? Are you now suprised? I am ashamed I have not done enough to vote everybody out!! Incompetence, incompetence, kila idara, sina uhakika na majumbani!!!
   
 12. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Nilijua wewe Lizungu kumbe nawe ni Riafrica.
   
 13. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #13
  May 27, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Kaaaaazi kweli kweli. Vitakuwa visa weeeeeee mpaka tununue mitambo ya Dowans. Yangu macho na masikio!!!! Jamani hiyo yaweza kuwa maintanance ya 48 hours. Kama huna plan B nyumbani kwako basi maliza samaki wote na nyama ndani ya freezer, utalia.
   
 14. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #14
  May 27, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hawakawii kuanza kukata leo karibia na mpira ila hawatatupata maana wengine tumeshatayarisha majenereta
   
 15. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #15
  May 27, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mie nikafikiri kutakuwa na total solar eclipse ambayo sikuijua!
   
Loading...